Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Wanafunzi vyuo vikuu wageuka omba omba

$
0
0
Na Kadama Malunde,Shinyanga

KUCHELEWA kutolewa kwa fedha za kujikimu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu ambao wako katika mazoezi ya vitendo mkoani Shinyanga, kumesababisha baadhi yao kugeuka ombaomba  na wale wa kike kuwa hatarini kuuza miili yao.

Wanafunzi hao wamekosa a fedha za kulipia kodi za nyumba wanazopanga na huduma zingine muhimu ikwemo chakula na matibabu.

Akizungumza na waandishi wa habari  mjini Shinyanga , Waziri wa Sheria na Katiba wa serikali ya wanafunzi ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) cha Dar es Salaam, Kasanzu Luganga,alisema tangu waanze mazoezi kwa vitendo miezi miwili iliyopita hakuna fedha iliyotumwa na serikali na kusababisha kuishi katika mazingira magumu.

Alisema kutokana na changamoto hiyo, imesababisha baadhi ya wanafunzi kushindwa na kukatisha mazoezi kwa vitendo huku wengine wakigeuka ombaomba kwa watu, ili wapate fedha za chakula na kujikimu.

“Katika mkoa wa Shinyanga kuna wanafunzi kutoka vyuo vikuu saba ambavyo ni SAUT Mwanza,Tumaini Makumila cha Iringa,Mtakatifu Stephano Moshi,Jodani cha Morogoro, Kampasi ya SAUT ya Tabora na IFM,hivi vyote hakuna aliyelipwa fedha za kujikimu ambazo kila mwezi ni shilingi 620,000  na ziko kisheria lakini tunasikitika serikali ndiyo inakuwa ya kwanza kuharibu,”alisema.

Aliwataja wanafunzi walioacha mazoezi na kurudi makwao kuwa ni Simon Daniel aliyekuwa akifanya mazoezi wilayani  Kahama (TRA), Alikana Elick aliyekuwa akifanya mazoezi wilayani Bariadi na yeye  ambaye alikuwa akifanya mazoezi (NHIF) mjini Shinyanga.


Naye Gabriel Ndogani mwanafunzi wa mwaka wa pili chuo cha IFM, aliiomba serikali kutoa kipaumbele kwa wanafunzi  walioko vyuoni na kuondoa changamoto zinazowakabili.


“Jambo la kujiuliza kamafedha zilitengwa shilingi  bilioni  6.6 za mafunzo  sasa zimekwenda wapi? basi hata Wabunge wa Bunge Maalumu la katiba serikali iwakope na wao wacheleweshewe malipo,maana mara nyingi tunaoteseka ni sisi, tunafanya kazi kwa tabu na mazingira magumu huku wao wakineemeka,” alisema.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>