Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Wahamiaji Haramu Zaidi ya 1,000 Waondoka Karagwe.

$
0
0
Na Mbeki Mbeki, Karagwe
WAHAMIAJI haramu zaidi ya 1,000 wameondoka katika wilaya ya Karagwe mkoani Kagera na kurejea makwao.

Kwa nyakati tofauti jana baadhi ya wahamiaji haramu kutoka katika vijiji mbalimbali vya wilaya hiyo walionekana wakipakia mizigo yao na familia zao na kuelekea katiia mipaka ya Tanzania na Rwanda.

Wakizungumza na waandishi wa habari katika eneo la Omurushaka wakati wakisubiri magari ya kampuni ya Nchambi's (NBS) kuelekea wilaya ya Ngara, walisema wamelazimika kuondoka ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza endapo serikali italazimika kutumia vyombo vya dola.

Mmoja ya wahamiaji hao Joseph Nzeyimana alisema watakao athirika zaidi ni wahamiaji wenye mifugo kwani hakuna mtu atakaye ruhusiwa kuingia nchini Rwanda akiwa na wanyama hivyo watalazimika kuuza mali zao kwa gharama ndogo.

Nzeyimana alisema kuna idadi kubwa ya Wanyarwanda walioingia nchini katika kipindi cha mwaka 1994 na kuwa wahamiaji waliorudishwa nchini kwao katika operesheni ya 2006 walirejea Tanzania baadae.

Hata hivyo, alisema zoezi hilo linaweza kuwa gumu kwa kuwa kuna wahamiaji haramu wameolewa na kuzaa na Watanzania.

Hivi karibuni Rais Kikwete alitoa siku 14 kwa wahamiaji haramu kurejea makwao pamoja na majambazi kujisalimisha kabla ya operesheni kuwa itakayowahusisha wanajeshi kuanza.

Alisema katika mikoa ya Kagera, Geita na Kigoma kuna ongezeko kubwa la wahamiaji haramu ambao wamechangia ongezeko kubwa la ujambazi.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali mstaafu, Fabian Massawe alisema mkoa unasadikiwa kuwa na wahamiaji haramu 52,000.

Alisema operesheni ya kuwasaka itaanza hivi karibuni na itahakikisha raia wote wasio Watanzania wanarudishwa makwao.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>