Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Dk Shein awataka Madaktari kutoka China kuzingatia huduma za kinga

$
0
0
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na madaktari kutoka Jimbo la Jiangsu Nchini China waliofika Ikulu Mjini Zanzibar kusalimiana na
Rais,ma daktari hawa wataungana na Madaktari wazalendo katika kutoa  huduma katika Hospitali za Serikali Unguja na Pemba

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na madaktari kutoka Jimbo la Jiangsu Nchini China waliofika Ikulu Mjini Zanzibar kusalimiana na Rais,madaktari hawa wataungana na Madaaktari wazalendo katika kutoa huduma katika Hospitali za Serikali Unguja na Pemba

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na madaktari kutoka Jimbo la Jiangsu Nchini China waliofika Ikulu Mjini Zanzibar kusalimiana na Rais,madaktari hawa wataungana na Madaaktari wazalendo katika kutoa huduma katika Hospitali za Serikali Unguja na Pemba

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwa katika picha ya pamoja na madaktari kutoka Jimbo la Jiangsu Nchini China waliofika Ikulu Mjini Zanzibar kusalimiana na Rais,madaktari hawa wataungana na Madaaktari wazalendo katika kutoa huduma katika Hospitali za Serikali Unguja na Pemba

Baadhi ya Madaktari kutoka Jimbo la Jiangsu Nchini China waliofika Ikulu Mjini Zanzibar,wakimasikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipozungumza na madaktari hao leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

Said Ameir, Ikulu
Serikali imetoa wito kwa wataalamu wa afya kutoka China waliopo nchini  kuangalia pia suala la kinga ya maradhi mbalimbali badala ya kutilia mkazo zaidi suala la tiba wakati wanapokuwa nchini.
 

Wito huo umetolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein wakati alipokuwa akizungumza na timu ya 25 ya wataalamu wa afya kutoka Jamhuri ya Watu wa China waliomtembelea Ikulu leo.
 

Timu hiyo ya wataalamu 21 wakiwemo madaktari bingwa iliwasili nchini mwezi Juni mwaka huu ambayo inatarajiwa kukaa nchini kwa miaka miwili inatoka Jimbo la Jiangsu China ambako wataalamu wa afya kutoka jimbo hilo wamekuwa wakija Zanzibar kufanyakazi tangu mwaka 1964.
 

“Msijishughulishe tu katika kutoka huduma za tiba badala yake muangalie pia suala la kinga ambalo ni muhimu katika kuimarisha afya za wananchi”aliwaambia wataalamu hao huku akiwataka kuvitumia vyombo vya habari vikiwemo vya Serikali kuelimisha jamii juu ya kinga ya maradhi mbalimbali.

 

Dk. Shein amesema timu hiyo ya 25 ya wataalamu wa kichina ina umuhimu wa kipekee kwa kuwa pamoja na kutoa huduma kwa wagonjwa lakini pia imekuja kutekeleza mipango maalum wa kusimamia ujenzi wa kituo cha uchunguzi wa maradhi ya njia ya chakula katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja Unguja na kituo cha kuhudumia wagonjwa waliopata ajali huko katika hospitali ya Abdalla Mzee Pemba.
 

“Vituo hivyo ni vipaumbele kwetu kwa kuwa vitapunguza gharama kwa serikali ya kuwapeleka wagonjwa nje ya Zanzibar kwa matibabu na wakati mwingine hata kwa uchunguzi”alisema Dk. Shein.

Alibainisha kuwa hivi sasa wagonjwa wengi wenye matatizo ya nija ya chakula hulazimika kupelekwa Dar es Salaam au hata nchi za nje hivyo kukamilika kwa kituo hicho kutakuwa faraja kwa Serikali na wananchi.
 

Kwa upande wa kituo cha watu wanaopata ajali huko Pemba alisema ni muhimu kwa kuwa kumekuwepo na ajali nyingi kisiwani humo hususan katika msimu wa uchumaji karafuu hivyo kujengwa kwa kituo hicho kumekuja wakati muafaka.
 

Dk. Shein aliwahakikishia wataalamu hao kuwa Serikali itafanya kila jitihada kuhakikisha mazingira ya utendaji kazi yanaimarishwa ili wataalamu hao waweze kutoa huduma kwa wananchi ambao alisema si wageni kwa wataalamu wa afya toka China.
 

“Miaka 49 sasa wataalamu wa kichina wanafanya kazi hapa hivyo hatuhitaji kuwatambulisha kwa wananchi kwa sababu wanawafahamu vyema utaalamu wenu, uwezo na umakini wenu katika kuwahudumia” alieleza Dk. Shein.
 

Rais wa Zanzibar aliwaeleza wataalamu hao kuwa uhusiano wa Tanzania na China ni wa hali na mali na kwamba Zanzibar na Tanzania kwa jumla imejivunia uhusiano huo ambao umekuwa na manufaa kwa pande zote.
 

“Nilipokutana na Rais wa China mwezi Machi wakati wa ziara yake nchini Tanzania na tulipokutana tena Beijing wakati nilipofanya ziara nchini China mazungumzo yetu yalijikita katika kusisitiza dhamira ya nchi zetu kuendeleza na kuimarisha uhusiano wetu” alieleza Dk. Shein.
 

Dk. Shein alielezea ujio huo wa timu ya 25 ya wataalamu wa afya toka China alibainisha kuwa mara tu baada ya mapinduzi ya mwaka 1964 China ikiwa nchi ya pili kuyatambua Serikali ya nchi hiyo ilituma timu ya kwanza ya wataalamu wa afya kufanyakazi Zanzibar hadi leo imefikia timu ya 25.
 

Wakati huo huo timu ya wataalamu wa afya kutoka China imesema imejidhatiti kuwahudumia wananchi ili kuhakikisha inatoa mchango wake ipasavyo katika kuimarisha afya nchini.
 

Kauli hiyo imetolewa na kiongozi wa timu hiyo Dk. Lui Ya Ping wakati alipokuwa akitoa salamu za wataalamu hao kwa Rais.
 

“Tumejidhatiti kufanya kazi kwa bidii kuwahudumia wananchi kwa kuwa tunaamini kufanya hivyo tutakuwa tumetimiza wajibu wetu uliotuleta humu nchini” alieleza Dk Lui.
 

Aliongeza kuwa tangu kuwasili kwao miezi miwili iliyopita wamekuwa wakifanya kazi wakati wote na wamekuwa wakishirikiana vyema na wataalamu wenyeji katika kutoa huduma.
 

“Kulingana na hali ya sasa ya hospitali tumewasilisha mpangokazi wetu kwa Wizara ya Afya hapa pamoja na hospitali na kwa viongozi wetu huko China”alieleza Dk. Lui na kuongeza kuwa, katika kipindi watakachokaa Zanzibar, lengo lao ni kufanya kitu ambacho kitakuwa cha manufaa kwa Zanzibar  kwa miaka mingi.
 

Alisema ujumbe kutoka Idara ya Afya ya Jimbo la Jiangsu utawasili nchini mwezi Novemba mwaka huu kwa ajili ya kuangalia utekelezaji wa ujenzi wa vituo vilivyoelezwa katika mpango huo.

Dk. Lui ambaye ni mtaalamu wa maradhi ya moyo alisema wakati wakiwa hapa watasaidia pia kutoa mafunzo kwa watalaamu wa afya wa humu nchini.
 

Kati ya wataalamu hao 21, kumi na mbili wanafanyakazi katika hospitali ya Mnazi Mmoja Unguja na wengine 9 wanafanyakzi huko Hospitali ya Abdalla Mzee Pemba.

Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Afya Dk. Sira Ubwa Mamboya na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk. Saleh Jidawi.

   

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>