kundi la Utandawazi wakiwa kwenye moja ya tamasha hilo la Sanaa Bagamoyo, mwaka jana.
NA ANDREW CHALE, BAGAMOYO
KUNDI maalufu la ngoma asili la Utandawazi Theater Group ‘Matwigachallo’ jioni ya kesho wanatarajiwa kuwasha moto wa aina yake kwenye tamasha la Kimataifa la 33 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, lililoanza Septemba 22 mwaka huu kwenye viunga vya chuo hicho.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa tamasha hilo, Abmic
am Bafadhil ‘Bura’ alieleza kuwa, kundi hilo ambalo kwa sasa limejizolea umaalufu mkubwa ndani na nje ya Tanzania, linatarajiwa kutoa burudani ya ngoma za asili sambamba na watoto wadoigo wanaotia fola kwa sasa katika sanaa hiyo ya utamaduni, Watoto wadogo Gozibet Bwere (4) na Nyambuli Aginess Muganga (5).
“Kundi la Utandawazi ‘Matwigachallo’, la Ukerewe, litawasha moto kwa burudani ya aina yake, pamoja na watoto wao wadogo wenye uwezo na kipajimkikubwa cha kuimba, kucheza na kupiga ngoma” alieleza Bura.
Na kuongeza kuwa, watoto hao wamekuwa maalufu kwa sasa hasa katika sherehe za Kitaifa na Kimataifa kwa kupata kuonyesha uweo wao hivyo kwa uwepo wao kwenye tamasha hilo, itatoa fursa kwa watu mbalimbali kuwaona.
Mbali na kundi hilo la Utandawazi, pia kutakuwa na Umoja Culture Flying Carpet ambao wataonyesha michezo mbalimbali ya sarakasi, ngoma, muziki na michezo mingine kibao.
Aidha, Jumamosi kutatanguliwa na mahafali ya 25 ya Chuo hicho huku wahitimu wa 37 wakitarajiwa kutunukiwa vyeti vyao, ambao Wanawake 11 na wanaume 26.