Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Mbuzi 120 wakamatwa wakisafirishwa kwa magendo

$
0
0
Na Madina Issa
MBUZI 120 wamekamatwa maeneo ya pwani ya Kizingo baada ya kupitishwa katika bandari bubu isiyoruhusika kisheria.

Mbuzi hao hivi sasa wamekabidhiwa Udara ya Mifugo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi ili kujulikana kama wapo salama.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake Muembemadema, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam, alisema tukio hilo lilitokea Septemba 27 majira ya saa 3:00 usiku katika bahari ya Kizingo wilaya ya majini Unguja.

Alisema watu hao walikamatwa wakati wakiwashusha mbuzi hao katika bandari hiyo kwa madai boti yao waliyokuwa wamepakia imeharibika na ndipo walipoona washushie maeneo hayo.

Aliyataja matukio mengine ni kuchomwa kisu na kupigwa mapanga vijana  wawili ambapo mmoja ni mkaazi wa Mwembeshauri na mwengine ni mkazi wa Amani wilaya ya mjini  Unguja.

Alisema tukio la kupigwa kisu kijana Jamali Abdallah Mohammed (18) limetokea Septemba 25 mwaka huu majira ya 3:30 Mwembeshauri na kujeruhiwa katika sehemu zake za siri ambapo mtuhumiwa alitambuliwa kwa jina la Munawir Abdulla mkaazi wa Muembeshauri.


Alisema kijana huyo alifikishwa hospitala ya Mnazimmoja kwa matibabu zaidi na hali yake inaendelea vizuri huku jeshi la polisi linaendelea na upelelezi juu ya tukio hilo.

Tukio jengine lilitokea Septemba 24 saa 1:00 usiku Miembeni ambapo Omar Yasir Juma (18) mkaazi wa Amani alishambuliwa na watu wawili ambao hawakufahamika  kwa kupigwa panga sehemu ya kichwa na mdomoni pamoja na kunyang’anywa simu nne aina ya Nokia na fedha taslimu shilingi 15,000 pamoja na vocha za Zantel zenye thamani ya shilingi 60,000.


Aliwataka wananchi kuwa waangalifu na kufuata sheria bila ya kushurutishwa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>