Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

JK amlilia Dk. Shija

$
0
0
Na Mwandishi wetu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, ameelezea huzuni na masikitiko yake kuomboleza kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Nchi za Jumuia ya Madola (CPA), Dk. William Shija.

Dk. Shija aliyefariki dunia Jumamosi asubuhi mjini London, Uingereza, ambacho ndicho kilikuwa kituo chake cha kazi, alisomea na kuwa mhadhiri wa uandishi wa habari kabla ya kuwa Mbunge wa Sengerema kwa miaka 15 mfululizo na Waziri Mwandamizi wa serikali katika Wizara mbali mbali.

Katika salamu zake kwa Sekretarieti ya CPA, Kanda ya Afrika, Rais Kikwete, alisema amestushwa na kifo cha Dk. Shija ambacho kimeinyang’anya Afrika na dunia, na hasa Tanzania na Jumuia ya Madola, mtumishi mwadilifu na mwaminifu, ambaye alitoa maisha yake kwa utumishi wa umma.

“Alikuwa kiongozi mfano katika nafasi zote za umma alizozishikilia. Aliifanya kazi yake ya uhadhiri wa uandishi wa habari kwa ufanisi mkubwa na aliwapa utumishi uliotukuka wananchi wake wa Sengerema katika nafasi yake ya Ubunge. Dk. Shija alitumainiwa katika nafasi zote nyingi na za uandamizi za uwaziri wa serikali,” alisema.



“Nawatumieni salamu za dhati ya moyo wangu kuomboleza kifo cha Dk. Shija na naungana nanyi katika kumlilia. Kupitia kwenu, nawatumia wajumbe wote wa CPA na Sekretarieti ya Chama hicho pole nyingi kwa kuondokewa na kiongozi na mtendaji wao mkuu. Aidha, naomba pia mniwasilishie pole zangu kwa wana-Sengerema ambao Dk. Shija aliwatumikia kwa uaminifu na kwa miaka mingi,”alisema.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>