Huduma ya taa mpya na za kisasa za solar katika makutano ya barabara ya mkunazini kwa khamis machungwa na michezani zimeeza kazi baada ya kukamilika kwa ufungaji wake na kutowa huduma kwa watumiaji wa barabara hiyo na baadhi ya madereva kupata shida katika matumizi yake wakati wa kuruhusiwa kupita baada ya kuwaka taa ya kijani,
Eneo hili lilikuwa na taa hizo na kuharibika kwa muda mrefu bila ya huduma hiyo ikiwemo na makutano ya barabara ya malindi bado taa hizo kuweka katika eneo hilo baada ya taa hizo kutokuwepo kwa muda mrefu sasa.Inabidi na eneo lile kufanyiwa utaratibu wa kuweka taa hizo kupunguza msongamano wa magari katika eneo hilo wakati wa saa kwenda kazini na kurudi magari huwa mengi ikizingatiwa wakati huo hutowa huduma ya usafiri kwa wananchi wengi wanaotoka safari pia hutumia njia hiyo.