Usiku wa Oktoba 21 ni siku yangu muhimu sana kwani, ndiyo niliyozaliwa. Hii ilikuwa ni majira ya saa 3 usiku katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ni mwaka 1985.
Leo nina furaha isiyo kifani kwa kuweza kusherehekea siku yangu hii ya kuzaliwa… hakika Mungu ni mkuu nawashukuru nyote kwa kushirikiana nami bega kwa bega katika kipindi chote cha maisha yangu nawatakia kila lakheri pia.
Najivunia kua mtanzania ila ndani ya miaka hii yote nakumbuka mengi na nimepitia mengi ikiwemo milima na mabonde machozi na jasho la damu.
Kwa kifupi, mpaka kufikia leo tokea 1985, lakini hapo hapo natimiza miaka 14 ya mateso katika uhai wa kuishi pekee yangu (kujitegemea) ni hakika naeleza nimepitia mateso makubwa huku kubwa kuliko ni la kuishi katika maisha ya mtoto wa mitaani (Street children) lakini Mungu alikua nami na wasamalia wema wakanitoa huko na sasa nipo hapa nilipo.
Hivyo basi leo nawashukuru nyote kwa kua nami bega kwa beka kwa kipindi hiki na kijacho shukrani ziwafikie wote wakiwemo kwa uchache Bosi wangu, Ansbert Ngurumo, (Freemedia Ltd), Mohamed Dewji (MB-Singida mjini), famlia ya Mnyanga, Simtoe, Mtweve, Munaar, Wafanyakazi wote wa Freemedia Ltd * Tanzania Daima na Sayari, wafanyakazi wenzangu na wanachama wa kikosi cha maafa na uokoaji Tanzania Red cross, Shyrose Bhanji, Agustino Chale (baba mkubwa) Living Faith Church, familia ya Monga, wanafunzi wote Gilman Ruthinda primary LY 2002, wanafunzi Sekondar- Mbalizi High na Meridian High ... bila kuwasahau wanafunzi wa Royal Collage of Tanzania, Red Cross Tanzania First Aids Collage na wengine wengi nyote nawashukuru sana I say I love all..and Blogger nyote nawashukuru