Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Kamati ya Muungano yapata suluhisho za kero 10 za Muungano

$
0
0
Na Janet Josiah
 
KAMATI ya pamoja ya kushugulikia masuala ya muungano wa Serikali ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imefanikiwa kutatua hoja 10 kati 19.
Hoja zilizotatuliwa ni suala la ongezeko la gharama za umeme kwa asilimia 21.7 kwa wateja wa Tanzania Bara na Zanzibar asilimia 168 ambalo kamati hiyo imeafikiana na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kufanyiwa marekebisho ya viwango vya bei.
Msemaji wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Siglinda Chipungaupi, alisema juzi kuwa pamoja na kufanyiwa marekebisho ya bei pia deni la Shirika la Umeme la Zanzibar (Zeco) litapatiwa ufumbuzi.
Hoja nyingine zilizotatuliwa ni utekelezaji wa sheria ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Zanzibar, sasa imefanyiwa marekebisho kupitia sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali ‘Written Laws Miscellaneous Amendments’ namba 8 ya mwaka 2006 ambapo sasa inafanya kazi sehemu zote mbili.

Chipungaupi alisema pia hoja ya ushiriki wa Zanzibar katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo iliwasilisha miradi ya maendeleo ya kiuchumi kwa ajili ya kuijumuisha katika miradi ya kikanda inayotekelezwa katika jumuiya ya Afrika Mashariki nayo ilipita.
Hoja ya mgawanyo wa mapato yatokanayo na msaada kutoka nje, alisema mazungumzo yalifanyika baina ya SMT na SMZ yalifikia muafaka kwamba fomula ya asilimia 4.5 itumike katika kuhakikisha kwamba SMZ inapata fungu lake.
Pamoja na hizo, hoja nyingine zilizokubaliwa ni za uvuvi katika ukanda wa uchumi na bahari kuu, Uwezo wa Zanzibar kukopa ndani na nje ya nchi ambapo makubaliano yaliafikiwa kwamba wizara zinazoshughulikia masuala ya fedha SMT na SMZ ziandae utaratibu na muongozo.
Hoja ambazo bado zipo katika mazungumzo ni suala la kodi ya mapato na zuio, Utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asili, Ushirikiano wa Zanzibar na Taasisi za Nje, ajira kwa watumishi wa Zanzibar katika taasisi za muungano na mfuko wa maendeleo wa jimbo kwa SMZ.
Zingine ni malalamiko ya wafanyakazi kutozwa kodi mara mbili, hisa za SMZ zilizokuwa kwenye bodi ya sarafu ya jumuiya ya Afrika Mashariki, tume ya pamoja, usajili wa vyombo vya moto, kuimarika ushirikiano kwa masuala yasiyo ya muungano na kujenga udugu miongoni mwa Watanzania
 
Chanzo - Tanzania Daima

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>