MRATIBU wa kituo cha huduma za sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Fatma Hemed Khamis akielezea umuhimu wa mafunzo ya kuwakumbusha sheria za ajira Zanzibar, wahitimu wa wasaidizi wa sheria wa majimbo kdahaa kisiwani humo, ambao wamepatiwa taaluma hiyo na ZLSC, kulia ni Afisa Mipango wa kituo hicho sheikh Khalfan Amour na kushoto ni mtoa mada mwanasheria Omar Hemed (picha na Haji Nassor, Pemba)
WASAIDIZI wa sheria wa majimbo kadhaa kisiwani Pemba, ambao ni wahitimu wakimsikiliza mtoa mada ambae ni Afisa Mipango wa kituo cha huduma za sheria Pemba Safia Saleh Sultan (hayupo pichani), kwenye mafunzo ya kuwakumbusha sheria za ajira Zanzibar, mafunzo yaliofanyika kituoni hapo (picha na Haji Nassor, Pemba)
MWANASHERIA Omar Hemed akiwasilisha mada juu ya haki za binaadamu, mbele ya wahitimu wasaidizi wa sheria wa majimbo kadhaa kisiwani Pemba, yaliondaliwa na kituo cha huduma za sheria Pemba, kulia ni afisa mipango wa kituo hicho, sheikh Khalfan Amour na katikati ni Mratibu wa ZLSC Pemba, Fatma Hemed Khamis (picha na Haji Nassor, Pemba)