Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Dk Shein : Zanzibar ina mengi ya kujifunza kutoka Uholanzi

$
0
0
Na Said Ameir , Ikulu
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein emeeleza kuwa ushirikiano mzuri kati ya Zanzibar na washirika wa maendeleo unaifanya Serikali na wananchi kuongeza ari na jitihada zaidi katika kutekeleza mipango ya taifa ya maendeleo.
 
Dk. Shein amesema hayo jana alipokuwa akizungumza na Balozi mpya wa Uholanzi nchini bwana Jaap Fredericks aliyefika Ikulu kujitambilsha.
 
“lengo la dira yetu ya maendeleo ya 2020 ni kuifanya Zanzibar kuwa nchi yenye uchumi wa kati. Tunajitahidi huku jitihada zetu zikitiwa shime na washirika wetu ambao wamekuwa bega kwa bega nasi kuhakikisha tunalifikia lengo hilo”alisema Dk. Shein.
 
Alieleza kuwa Zanzibar haina budi kujifunza kutoka kwa washirika wake wa maendeleo kama nchi ya Uholanzi ambayo imepiga hatua katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
 
Katika kuimairisha uhusiano kati ya Uholanzi na Zanzibar Dk. Shein amemueleza Balozi huyo kuwa Zanzibar inazo fursa nyingi za uwekezaji hivyo angependa kuona ushiriki zaidi wa wawekezaji kutoka nchi hiyo wanawekeza nchini ili kuharakisha maendeleo ya uchumi kwa manufaa ya nchi zote.
 
“tuna kila sababu za kuimarisha na kuundeleza uhusiano wetu na fursa ya uwekezaji ni njia mojawapo ya kupanua maeneo mengine ya ushirikiano kwani utatoa fursa kwa watu wetu kushirikiana kwa karibu zaidi” Dk. Shein aliongeza.
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali na wananchi wa Uholanzi kwa misaada mbalimbali ambayo imekuwa ikiitoa kwa Zanzibar na Tanzania kwa jumla.
 
Dk. Shein alimhakikishia Balozi Frederick kuwa Serikali na wananchi wa Zanzibar watampa ushirikiano unaostahiki ili aweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo nchini kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake.
 
Kwa upande wake Balozi huyo mpya ya Uholanzi bwana Fredericks amesema jukumu lake wakati wote atakaokuwa nchini ni kuhakikisha anaimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya nchi yake na Tanzania kwa kuangalia maeneo zaidi ya ushirikiano.
 
“Serikali yetu imedhamiria kushirikiana na Serikali na watu wa Tanzania kuongeza maeneo zaidi ya ushirikiano” alisema Balozi Fredericks na kutaja baadhi ya maeneo hayo kuwa ni pmoja na  uchumi, biashara na nishati.
 
Wakati huo huoRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein leo amewaapisha Makatibu Wakuu wawili waliteuliwa jana kufuatia mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri na Watendaji Wakuu wa Wizara.
 
Waliopishwa leo ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Khamis Mussa Omar na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma Bibi Fatma Gharib Bilal. Baadhi ya  Mawiziri na Makatibu wakuu waliapishwa jana mara baada ya uteuzi kufanyika.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>