Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

NIDA Ikiwa katika zoezi la kukabidhi Vitambulisho kwa Wananchi.

$
0
0
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Ofisi ya Zanzibar Ndg Vuai Mussa, akizungumza na waandishi swa habari wa Vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar, akizungumzia mafanikio ya Uandikishaji wa Vitambulisho kwa Wananchi wa Zanzibar walivyojitokeza kwa wingi na kuitikia wito huo na wakati wa uchukuaji pia walijitokeza kwa wingi, Wakati wa zoezi hilo la ugawaji katika Mkoa wa Kaskaszini na Kusini Unguja wamejitokeza kupata vitambulisho vyao na Sasa wanaingia katika Wilaya ya Mji kugawa Vitam,bulisho hivyo kwa Wananchi kila zoni utaratibu wa Ugawaji vitambulisho hivyo itakuwa kwa muda wa siku tatu. Na kusema Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini wamejitokeza kwa wingi kuchukua vitambulisho vyao Wananchi 30 wamepata vitambulisho hivyo na kati ya Vitambulisho 42,000, katika mkoa huo. Website.www.nida.go.tz 
Afisa wa Habari wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Tanzania Ndg Said Mohammed, akifafanua jambo na kutoa taarifa ya zoezi hilo kwa waandishi wa habari Zanzibar.
Waandishi wakifuatilia maelezo ya Mkurugenzi wa Vitambulisho vya Taifa wakati wa mkutano wao na mkurugenzi katika Ofisi za Mamlaka ya Vitambulisho Zanzibar
Waandishi wakiwa katika ukumbi wa mkutano Ofisi za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Zanzibar

Mwandishi wa habari akiuliza swali kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa wakati wa mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake kilimani Unguja. 
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Ofisi ya Zanzibar, Ndg Vuai Mussa akifafanua jambo wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusiana na zoezi la kuandikisha Vitambulisho kwa Wananchi na kueleza Mamlaka imekadiria kuandikisha Wananchi 682,202,na baadae tukachukua alama ya kibailojia kwa wananchi 573,007 hii ni sawa na asilimia 83.99%, kwa hivi sasa, na kujibu tayari wameshazalisha Vitambulisho 475,614, hii ni sawa asilimia 83.0% ya Wananchi waliochukuliwa alama za Kibailojia
Zoezi hilo limemaliza katika mikoa ya Kaskazini na Kusini Unguja na sasa Wanaaza katika Mkoa wa Mjini Magharibu wakiazia Wilaya ya Mjini.  
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano na Mkurugenzi wa Vitambulisho akitowa tadhimini ya mafanikio kwa kiasi kikubwa kuandikisha Wananchi katika Vitambulisho vya Taifa Tanzania. 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>