STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 25.11.2014
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa Zanzibar ina Mamlaka yake kamili na yeye ndie Rais na kuwashangaa wanaodai Mamlaka ya Zanzibar hii leo.
Hayo aliyasema leo katika Mkutano kati yake na viongozi wa Mashina na Maskani za CCM za Wilaya ya Kati Unguja, Mkutano uliofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Tamarind Uroa, Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Dk. Shein aliwashangaa wanaodai Mamlaka ya Zanzibar kwani Zanzibar inamamlaka yake kamili kwani ina nguzo zake tatu muhimu ikiwemo Mahakama Kuu ya Zanzibar, Serikali ambayo yeye ndie Rais pamoja na Baraza la Kutunga Sheria ambalo ni Baraza la Wawakilishi kwa hapa Zanzibar.
Alisema kuwa zipo alama mbali mbali zinazoonesha kuwa Zanzibar ina Mamlaka yake kamili zikiwemo Bendera, Wimbo wa Taifa, na nyenginezo na kusisitiza kuwa yoyote anaejiita msomi ni lazima aheshimu taratibu za nchi yake, viongozi wake pamoja na wananchi kwa jumla.
Aidha, Dk. Shein alieleza kuwa Serikali ya Mamlaka Kamili Zanzibar haiji kwa sababu tayari Zanzibar ina Mamlaka yake kamili na kinachofanyika hivi sasa ni upotoshwaji tu kwa wananchi.
Pamoja na hayo, Dk. Shein alisema kuwa Katiba iliyopendekezwa ni ya Mfumo wa Serikali mbili hivyo aliwataka wapinzani wasiwapotoshe wananchi na kusisitiza kuwa maelezo yake juu ya Katiba hiyo atayasema wakati wa Kampeni ukifika ambao utakuwa ni muda wa siku 30.‘Waamuzi wa kuamua ni Wazanzibari wote”,alisema Dk. Shein.
Ameeleza kuwa ametiwa moyo na mahudhurio makubwa aliyoyapatavyama wanataka kuviondosha lakini mawe, tunaijua historia ya nchi yetu kabla hutajatawaliwa hadi pale kutawaliwa na wakoloni wakiwemo Sultani wa Oman.
“Mapinduzi ya Januari 12, 1964 ndipo palipoanza ukombozi na ndio yalioikomboa Zanzibar na kufika hapa tulipofika hadi leo.... CCM haitokuwa tayari kuwarejesha watu walioko nje ya Zanzibar, Wazanzibari wenyewe wako macho”,alisema Dk. Shein.
Makamu Mwenyekiti huyo wa CCM Zanzibar aliwatanabahisha WanaCCM kwa wale waliokuwa na ndoto za kuirejesha Zenj Empire ambayo ilikuwepo wakati wa ukoloni na baada ya Mapinduzi ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964 Serikali ikaunda Baraza la Manispaa liliopo hivi waondoshe ndoto zao hizo za mchana.
Dk. Shein alieleza kuwa Mabalozi wana dhamana kubwa sana na kuwataka kuzingatia nafasi, Katiba na Utaratibu uliowekwa na chama chao na kuwataka wawajibu wale wote wanaokibudhudhi chama hicho pamoja na na Serikali iliyopo madarakani majibu sahihihi na yenye umakini na busara.
Aidha, Dk. Shein aliwataka viongozi hao kuwapitia wanachama wao pamoja na wale wasiokuwa wanaCCM, na kusisitiza kuwa kiongonzi hanuni na badala yake huwajali wanachama wote wanaomuunga mkono na wasiomuunga mkono ili kuwavutia waingie katika chama chake.
Alisisitiza kuwa CCM inawajali sana Mabalozi wake licha ya kuwepo uchache wa nyenzo za kufanyia kazi lakini chama hicho hakiko tayari kukiachia chama chengine kuiongoza nchi.
Aidha, Dk. Shein alitumia fursa hiyo kueleza mafanikio ya Muungano huku akisisitiza kuwa kamwe Muungano huo hautovunjia na kuelezaa kuwa ataendelea kuuulinda Muungano wa Serikali mbili kama alivyoahidi wakati wa Kampeni za uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Dk. Shein aliwataka wananchi kutouchezea Muuungano uliopo na wasidhanie kuwa Katiba haipo na kuwataka kuheshimu Serikali iliyopo huku akisisitiza kuwa vyama vingi vimekuwja kuimarisha demokrasi na si kuja kukashifu serikali.
Sambamba na hayo, Dk. Shein aliwataka wapinzani kutumia busara kwa serikali iliopo madarakani na kusisitiza kuwa Katiba ipo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ipo, hivyo heshima ni lazima iwepo kwa madhumuni ya kuendeleza nchi.
Aliwataka wanaCCM kuweka mazingira mazuri ya kushinda uchaguzi kama inavyoeleza Katiba ya CCM kuwa ni lazima kushinda uchaguzi kwani hakuna historia wala rekodi ya CCM kushindwa uchaguzi.
Aliwahakaikishia WaCCM kuwa uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2015 utakuwa uchaguzi huru na wa haki pamoja na kuwa uchaguzi wa amani na salama, na kuwahakikishia wananchi kuwa kila mmoja atapata nafasi ya kumchagua kiongozi anaemtaka.
Aliwataka kuwashajiiisha vijana kwenda kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Kupiga kura ili wawe na haki ya kupiga kura huku akiwataka wazee na wazazi kuwasomesha vijana wao ili waelewe jinsi nchi ilivyokuwa hapo kabla, ilivyo hivi sasa na itakavyokuwa hapo baadae.
Kwa upande wa kilimo, Dk. Shein alisema kuwa katika awamu ya saba, ruzuku, mbegu bora, dawa, pembejeo na masuala mengine ya kilimo na kueleza kuwa Serikali imefidia kwenye kilimo na tayari yapo matrekata mapya 20 na hivi sasa Serikali ina nia ya kuingiza matrekta 50 mapya kwa ajili ya kuimarisha sekta hiyo.
Alisema kuwa CCM ni chama kikubwa na sio kama vyama vyengine na ndicho kilichoikomboa Tanzania na katika ukanda mzima wa Afrika ndio miongoni mwa chama kinachoendelea kuongoza Dola hadi leo.
Nae Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai akimkaribisha Dk. Shein katika mkutano huo alieleza kuwa wanaCCM, viongozi na wananchi wote wa wilaya kati walitoa pongezi kwa Dk. Shein kwa kusimamia amani na usalama wao hasa aple palipojitokeza watu wachache kutaka kuvuruga amani.
Alieleza kuwa kumekuwa na upotoshwaji wa makusudi kutoka kwa wapinzani kuwa Katiba iliyopendelezwa inawakandamiza Wazanzibari jambo ambalo sio la kweli na kuaeleza kuwa Katiba hiyo ina maslahi kwa Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla.
Vuai alieleza juu ya upotoshwaji unaoenezwa hivi sasa kuwa Katiba inayopendekezwa haimpi Mzanzibari hata Unaibu Spika wakati Ibara ya 150 kifungu kidogo cha nne, kinaeleza kuwa Spika na Naibu Spika watachaguliwa kutoka sehemu zote za Jamhuri ya Muungano endepao Spika atatoka sehemu moja Naibu atatoka upande mwengine wa Jamhuri ya Muunganao ambapo Katiba ya 1977 haikuonesha hayo.
Aidha Naibu Katibu Mkuu huyo wa CCM Zanzibar alieleza juu ya Katiba iliyopendekezwa katika Kifungu cha Uhusiano na Uratibu wa mambo ya Muungano ambacho kinaeleza shughuli za Tume ya Usimamia na Uratibu wa mambo ya Muungano na si kama inavyopotoshwa hivi sasa.
"Wao waache watoe kejeli sisi tunasonga mbele katika kuimarisha miradi ya maendeleo na kuimarisha uchumi wa nchi.... kamwe Muungano hautovunjika",alisema Vuai.
Katika risala yao viongozi hao walieleza furaha yao walioyonayo kwa kuona na kufaidika na matunda ya Dk. Shein katika utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi wa CCM ya mwaka 2010-2015 katika maendeleo kwenye sekta mbali mbali za afya, elimu, na miundombinu ikiwa ni pamoja na kufunguliwa kwa kituo cha afya Ghana na kupatiwa huduma bora katika kituo cha afya Mwera.
Aidha, walieleza kuwa kufunguliwa skuli ya Chekechea ya Cheju, skuli ya Uzini Sekondari, Ujenzi wa barabara unaoendelea katika kijiji cha Umbuji, mradi wa barabara ya Jumbi-Koani, Jendele-Unguja Ukuu pamoja na nyumba za makaazi ya wananchi Mpapa na usambazaji wa maji katika Shehia ya Dunga Bweni.
Mbali na mafanikio hayo, makubwa waliyoyaeleza viongozi hao pia, walieleza changamoto kadhaa zinazowakabili katika uendelezaji na uimarishaji wa chama hicho ambapo Makamo Mwenyekiti aliahidi kutekelezwa hatua kwa hatua kwa mashirikiano ya pamoja kati yake na viongozi pamoja na wanachama wa chama hicho.
Walimuhakikishia Dk. Shein kuwa CCM itashinda kwa kishindo katika uchaguzi Mkuu ujao na kuahidi kupiga kura ya na kumuahidi kuwa wataendelea kushirikiana nae katika kutekeleza na kuleta maendeleo na kumuhakikishia kuwa CCM itaendelea kuwa imara katika Mkoa wao.
Viongozi hao pia walipata fursa ya kutoa michango, mawazo pamoja na kuuliza masuala mbali mbali kwa Dk. Shein kwa lengo la kuimarisha na kukiendeleza chama chao huku wakimpongeza kwa umahiri wa anaoonesha katika kuongoza Serikali ya Umoja wa Kitaifa sambamba na utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk