Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Article 3

$
0
0
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
       Zanzibar                                                                                                               28.11.2014
---
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein leo amewaapisha viongozi mbali mbali katika hafla iliyofanyika Ikulu mjini Zanzibar.

Viongozi walioapishwa katika hafla hiyo ni Bwana Khamis Jabir Makame ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja ambapo kabla ya uteuzi wake huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini ‘B’ Unguja,  Luteni Kanali Mstaafu Haji Makungu Mgongo ambaye ameapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini ‘B’ Unguja ambapo kabla ya hapo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja.


Bwana Hassan Khatib Hassan ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete, Bibi Khadija Bakari Juma ambaye ameapishwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Bibi Madina Mjaka Mwinyi ameapishwa kuwa Naibu Katibu Mkuu (Taaluma) Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali.

Wengine ni Dk. Said Seif Mzee ambaye anakuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko, Dk. Juma Yakout Juma, ameapishwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo.

Hafla hiyo, ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wakiwemo  baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe. Said Hassan Said, Mkuu wa  Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Meja Mstaafu Kasim Tindwa, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali pamoja na Washauri wa Rais wa Zanzibar na viongozi wengine wa Serikali.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>