Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Mahafali ya Kituo cha Zanzibar Interfaith Center.Kwa Vijana wa Dini mbalimbali Zanzibar.

$
0
0
Muumini wa dini ya Kiislam akisoma dua kabla ya kuaza kwa hafla hiyo ya kukabidhiwa vyeti vyao baada ya kumaliza mafunzo yao, katika kituo cha Interfaith center shangani Zanzibar.
Muumini wa dini ya Kikristo akiomba kwa kupitia madhehebu ya dini yake kabla ya kuaza kwa hafla hiyo ya kukabidhiwa vyeti vyao baada ya kumaliza mafunzo yao, katika kituo cha Interfaith center shangani Zanzibar.
Mratibu wa Kituo cha Interfaith Center Ndg. Daniel Nygaard Madsen. akitowa maelezo ya kituo hicho na kutowa nasaha zake kwa wakufunzi wa kituo hicho baada ya kumaliza mafunzo yao ya mwezi mmoja ya kujifunza lugha ya kingereza, upigaji wa picha za videi na mnato jumla ya vijana 18 wameshiriki katika mafunzo hayo kutoka dini tafauti za kiislam na kikristo.
Shekh, Jabir Haidar akitowa nasaha zake katika mahafali hayo ikiwa baada ya kumaliza mafunzo yao yeye akiwa mmoja wa mwalimu aliyetowa mafunzo katika kituo hicho,
Baba Askofu Michael Hafidh akizungumza na Vijana wa dini tafauti wakati wa kufunga mafunzo yao yaliotolewa na kituo cha Zanzibar Interfaith Center Shangani Zanzibar,na kuwataka kutumia mafunzo hayo kujiajiri na kukuza amali katika visiwa vyetu na kukuza ushirikiano wa dini hizi mbili katika kuendeleza amani katika visiwa vya Zanzibar.
Wahitimu wa Kituo cha Interfaith Center wakimsikiliza Shekh Jabir Haidar akitowa nasaha zake kwa vijana hao walioshiriki mafunzo hayo kudumisha mahusiano ya pande mbili za dini Zanzibar kupitia mafunzo haya, mafunzo hayo yamewashirikisha Vijana 18 kutoka Dini mbalimbali Zanzibar. 
Wahitimu wa Kituo cha Interfaith Center wakimsikiliza Baba Askofu Micheal Hafidh akitowa nasaha zake kwa Vijana walioshiriki mafunzo hayo kudumisha mahusiano ya pande mbili za dini Zanzibar kupitia mafunzo haya, mafunzo hayo yamewashirikisha Vijana 18 kutoka Dini mbalimbali Zanzibar.  
Shekh. Jabir Haidar akimkabidhi Kitabu chenya mafundisho kwa Waumini wa Dini ya Kiislam na Kikiristo Mwanafunzi Hafsa Iddi, baada ya kumaliza mafunzo yao ya mwezi mmoja kujifunza nadharia kwa Vijana kuachana na vishawishi, mafunzo hayo yametolewa na Kituo cha Zanzibar InterFaith Center, kilioko shangani Zanzibar. Baada ya kukabidhiwa Cheti chake na Baba Askofu wa Kanisa la Mkunazini Unguja Askof Michael Hafidh.
Baba Askofu Micheal Hafidh akimkabidhi cheti mwanafunzi Bi Kristabella Salome, baada kuhitimu mafunzo kwa Vijana wa Dini tafauti Zanzibar, yaliotolewa na Kituo cha Zanzibar InterFaithCenter, kinatowa mafunzo ya kujitegemea kwa Vijana kujiajiri kuachana na kujishughulisha na vitendo viovu kuweza kujitegemea kupitia mafunzo hayo. 
Baba Askofu Micheal Hafidh akimkabidhi cheti mwanafunzi,Ndg.Azizi Ali,baada kuhitimu mafunzo kwa Vijana wa Dini tafauti Zanzibar, yaliotolewa na Kituo cha Zanzibar InterFaithCenter, kinatowa mafunzo ya kujitegemea kwa Vijana kujiajiri kuachana na kujishughulisha na vitendo viovu kuweza kujitegemea kupitia mafunzo hayo. 
Baba Askofu Micheal Hafidh akimkabidhi cheti mwanafunzi NdgKhamis Rashid,baada kuhitimu mafunzo kwa Vijana wa Dini tafauti Zanzibar, yaliotolewa na Kituo cha Zanzibar InterFaithCenter, kinatowa mafunzo ya kujitegemea kwa Vijana kujiajiri kuachana na kujishughulisha na vitendo viovu kuweza kujitegemea kupitia mafunzo hayo. 

Mratibu Elimu wa Kituo cha Zanzibar Interfaith Center Ndg Lusungu Mbilinyi, akitowea nasaha zake kwa wahitimu wa mafunzo hayo baada ya kukabidhiwa vyeti vyao na Baba Askofu Micheal Hafidh. wakati wa mahafali hayo yaliofanyika katika kituo hicho shangani Zanzibar.
Mratibu wa Kituo cha Vijana cha Zanzibar Interfaith Center Ndg Philip Eliah, akitowea nasaha zake kwa wahitimu wa mafunzo hayo baada ya kukabidhiwa vyeti vyao na Baba Askofu Micheal Hafidh. wakati wa mahafali hayo yaliofanyika katika kituo hicho shangani Zanzibar.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>