Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Balozi Seif Ahudhuria Mahafali ya 26 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania

$
0
0
Mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyopo Bungo Kibaha Mkoa wa Pwani kwa ajili ya mahfali ya 26  ya chuo hicho.Aliyesimama ni Mkuu wa Chuio Kikuu Huria cha Tanzania ambae pia ni Waziri wa Katiba na Sheria Tanzania Dr. Asha – Rose Migiro.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akiwa na Mwenyeji wake Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Dr. Asha-Rose Migiro wakiliongoza Gwaride kulingia kwenye uwanja wa Mahafali ya 26 ya chuo kikuu huria cha Tanzania yaliyofanyika Makamu Makuu yake Bungo Kibaha, Mkoa wa Pwani.
Balozi Seif akisalimiana na baadhi ya wahitimu wa shahada, stashahada na vyeti wa chuo Kikuu huria cha Tanzania ambao wametokea  Zanzibar .
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wa pili kutopka kulia wakiokaa akiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu wa Chuo Kikuu huria cha Tanzania waliosimama nyuma pamoja na Uongozi wa Chuo hicho.
Waliosimama wa pili kutoka kulia ni Mbunge wa Jimbo la Dole Muhitimu Mh. Silvester Mabunda. Kushoto ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Profesa Samuel Wangwe, kulia ya Balozi ni Mkuu wa Chuo ambae pia ni Waziri wa Katiba na Sheria Dr. Asha-Rose Migiro na Makamu Mkuu wa bChuo hicho Profesa Tolly Mbwette.(Picha na Hassan Issa OMPR)


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewahimiza Watanzania kuitumia  fursa  inayotolewa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania     { CKHT } katika kujipatia Taaluma  huku wakiendelea na shughuli zao za kazi,ajira binafsi au kifamilia kama kawaida.

Alisema wakati chuo hicho cha umma kinapotoa nafasi nzuri zaidi kwa Watanzania kupanua wigo wao wa elimu ya juu ni vizuri kwa wananchi kuitumia nafasi hiyo mapema bila ya kufanya ajizi.

Balozi Seif alieleza hayo wakati akizungumza na walimu na wahitimu wa Vyeti, Stashahada na Shahada  wa Mahfali ya 26 ya chuo Kikuu Huria cha Tanzania { CKHT }yaliyofanyika huko Bungo Kibaha Mkoa wa Pwani.

Alisema wanafunzi wengi wasio na uwezo wa kulipia ada katika vyuo vya mabweni wanaweza kukaa kwa muda mrefu kupata elimu hiyo endapo wataamua kusubiri Serikali au mashirika ya dini na watu binafsi kujenga vyuo  na mabweni hayo.

Balozi Seif  alisisitiza kwamba njia pekee ya Taifa kutaka wananchi wake wajikomboe kimaisha kutokana na ujinga, maradhi na umaskini ni kuwawezesha kupata elimu ya juu iliyo bora na yenye gharama nafuuu popote pale walipo katika eneo la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alitoa mfano wa uendeshaji wa Serikali za Mitaa unavyoimarika kila siku kutokana na wafanyakazi wengi kuhitimu elimu ya juu kupitia mfumo uliowekwa na chuo kikuu huria cha Tanzania.

Alisema mifumo mengine ya elimu inahitaji mwanafunzi kukaa darasani, ama kuacha kazi na wakati mwengine kuwa mbali na familia yake  kwa muda mrefu wakati uwezo wa kufanya hayo upo kwa kutumia chuo hicho Kikuu huria cha Tanzania.

“ Kama kiongozi wa Kitaifa, mimi mwenyewe ni shuhuda mkubwa wa jinsi ambavyo tumejionea shughuli za uendeshaji wa Serikali za Mitaa unavyoimarika siku hadi siku kutokana na wafanyakazi wengi ambao wanahitimu chuoni hapa ”. Alisema Balozi Seif.

Aliupongeza Uongozi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kwa mchango wake mkubwa wa kuwainua wanyonge  wenye fani tofauti hapa nchini ambazo zinahitajika katika maendeleo ya Taifa.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuahidi Uongozi wa Chuo hicho kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaunga mkono nia ya chuo hicho ya kuanzisha Chuo Kikuu kishiriki kipindi kufupi kijacho ili kufikia dira ya 2015 -2025 ya chuo ilivyolenga.

Alisema juhudi za makusudi zitawekwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikia a na Serikali za Mikoa katika kuona eneo la ujenzi wa chuo hicho kikuu kishiriki linapatika Visiwani Zanzibar.

Akigusia ushiriki wa wanafunzi wanawake katika chuo hicho balozi Seif  alisema idadi ya wasichana bado ni ndogo ikionyesha takwimu ya wanafunzi 1569 mwaka 2012/2013 ikipanda kidogo na kufikia 1668 mwaka 2013/2014  ikilinganishwa na wanafunzi wanaume waliofikia 3107 mwaka 2013/2014 na kupanda hadi  wanafunzi 3056 mwaka 2013/2014.

Balozi Seif aliwapongeza wanawake kwa kuongeza idadi yao licha ya kwamba bado takwimu yao iko chini. Hivyo juhudi za ziada watalazimika kuziongeza ili kujiweka tayari katika mfumo wa Uongozi Kijinsia.

Alifahamisha kwamba hata idadi ya watumishi wanawake katika chuo hicho bado inaonekana wachache ikionyesha idadi ya walimu wanawake 130 kati ya walimu wote 374 ikionyesha theluthi moja tuu ya walimu hao wanawake.

“ Hivi kwa utaratibu huu hiyo asilimia hamsini hamsini inayotarajiwa  ukweli itafikiwa ? ”. Aliuliza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi  Seif Ali Iddi.

Mapem,a Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Profesa Samuel Wangwe alisema juhudi mbali mbali za kuimarisha huduma za chuo zitaendelea kuchukuliwa ili kiwe miongoni mwa vyuo vikuu maarufu Duniani.

Profesa Wangwe alisema azma ya chuo hicho ni kuongeza idadi ya wanafunzi watakaokuwa  chachu ya ongezeko la wataalamu kitaifa na kimataifa.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa Baraza la Chuo Kikuu Huria cha Tanzania alieleza kwamba zipo changamoto zinazosumbua wana taaluma wake akizitaja baadhi yake kuwa ni pamoja na ukosefu wa Kampuni ya uchapaji vitabu ambavyo pia hutumiwa na vyuo vyengine vikuu pamoja na  upungufu wa wafanyakazi wa taaluma kwenye Mikoa mbali mbali hapa nchini.

Alimpongeza Waziri wa Katiba na Sheria Tanzania Dr. Asha Rose Migiro kwa kuchaguliwa kluwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Akitoa salamu kwa niaba ya wawakilishi waq vyuo mbali mbali vikuu wa kitaifa na Kimataifa Mwenyekiti wa Baraza la Elimi Afrika kutoka Nchini Zim,babwe Profesa Primos Prasha alisema elimu huria na ya masafa ndio njia pekee itakayolivua Bara la Afrika katika wimbi la ujinga.

Profesa Prismo ameupongeza ushirikiano mzuri uliopo kati ya vyuo vikuu huria vya Zimbabwe na Tanzania ambao una lengo la  kusaidia jamii za Waafrika kujikomboa kielimu.
Jumla ya wahitimu elfu 3,404 kutoka nchi mbali mbali Duniani wa fani tofauti wametunukiwa shahada, stashahada na vyeti kwenye mahafali hayo  na kukifanya chuo hicho kutoa wasomi elfu 21,503 tokea kuanzishwa kwake mwaka 1992.

Shahada, Stashahada na vyeti hivyo vimetolewa  kutokana na fani za uzamivu ya udaktari wa falsafa, shahada za uzamili ya sheria, shahada ya uzamili katika sheria za teknolojia ya habari na mawasiliano.

Nyengine ni shahada ya uzamili ya elimu ya sanaa katika utalii pamoja na shahada ya uzamili ya elimu katika kiswahili.

Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kilichoanzishwa mwaka 1992 kimekuwa kikipokea wanafunzi kutoka mataifa mbali mbali Duniani wengi wao wakitokea nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki { EAC } pamoja na Nchi za Mashariki nas Kusini mwa Afrika { SADC }.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>