Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Ng’ombe mwenye mimba akutwa amechinjwa

$
0
0
Na Husna Sheha
NG’OMBE mmoja ambae alikuwa na mimba ya miezi saba amekutwa amekatwa mapaja na kuchukua nyama katika eneo la Selemu Tumbotupu wilaya ya Kaskazini ‘B’ mkoa wa kaskazini Unguja.

Ng’ombe huyo alikutwa na raia mwema wakati akiwa anapita akielekea kondeni  kwake.

Mwandishi wa gazeti hili alifika eneo la tukio na kumkuta ng’ombe huyo akiwa amekatwa katwa mapaja yote manne na kuchukua nyama.

Baadhi ya wafugaji walisema matukio ya kuchinja ng’ombe na kuondoka na nyama yamekuwa yakiripotiwa mara kwa mara lakini hayafikishwi vituo vya polisi.

Mkuu wa kituo cha polisi Mfenesini, Idrissa Mwazini Makame alikiri kupokea taarifa za kuuawa ng’ombe huyo ambapo baadae alifukiwa katika tukio lililoshuhudiwa na mahakama.


Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Kaskazini Unguja, Salma Khamis, aliishauri jamii kushirikiana na jeshi la polisi kuwafichua wahalifu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>