Mkufunzi wa mafunzo ya kupiga picha yanayofanyika Jengo la ZBC, Karume House Mitsuhiro Hayao Matsuda kutoka Japan akitoa maelezo kwa washiriki (hawapo pichani) kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo.
Mkurugenzi mstaafu wa Idara ya Habari Maelezo Yussuf Omar Chunda akifungua mafunzi ya miezi sita ya wapiga picha yanayofanyika jingo la ZBC, karume House Mnazimmoja akisisitiza jambo kwa washiriki
Mratibu wa mafunzo ya kupiga picha Faki Mjaka akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo hayo yanayofanyika Jengola ZBC, Karume House
Washiriki wa mafunzo ya kupiga picha yanayofanyika Jengo la ZBC, Karume House wakimsikiliza mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo hayo.

Picha ya pamoja ya mgeni rasmi wa mafunzo ya kupiga picha, mkufunzi na washiriki wa mafunzo hayo.
(Picha zote na Makame Mshenga Maelezo-Zanzibar).
Na Miza Othman - Maelezo Zanzibar
Washiriki wa mafunzo ya kupigaji picha wametakiwa kufuatilia kwa karibu mafunzo hayo na kumpa ushirikiano wa karibu mkufunzi ili kutimiza lengo la kufanyika mafunzo hayo.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mstaafu wa Idaraya ya Habari Yussuf Omar Chunda wakati akifunguwa mafunzo hayo katika jengo la television, Karume House, Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar.
Amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwapatia taaluma zaidi watendaji wa kada ya habari ili waweze kutekeleza wajibu wao kwa ufanisi mkubwa zaidi.
Amesema Serikali imeleta mtaalamu kutoka Japan kutoa mafunzo ya upigaji picha na kuwajengea uwezo wapiga picha wa Taasisi za Serikali na binafsi ili kuwajengea uwezo mkubwa wapiga picha wa Zanzibar.
“Iwapo mtafuatilia mafunzo hayo kwa ukaribu mtafaidika nyinyi wenyewe na kutoa picha bora katika magazeti mbali mbali ya hapa nchi na nje ya nchi,” alisema Chunda.
Amewataka washiriki wa mafunzo hao kuitumia vizuri nafasi waliyopata na kuhakikisha wanashiriki kikamilifu mafunzo hayo na baadae kuyafanyikazi kwa faida yao na taifa kwa jumla.
Mkufunzi wa wa mafunzo ya upigaji picha Mitsuhiro Hayao Matsuda kutoka Japan amewahakikishia washiriki kwamba atafanya kila analoweza kuwajengea uwezo na utaalamu zaidi wa kupiga picha na kuwa wapiga picha bora.
Mafunzo hayo ya miezi sita yanafanyika siku mbili kwa wiki na yanashirikisha waandishi na wapiga picha kutoka Idara ya Habari, Shirika la Utangazaji (ZBC) Shirika la Magazeti Zanzibar, Vyombo vya Habari binafsi na wapiga picha wa kujitegemea waliopo Zanzibar.