Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

ZJMMC ya Kwanza Kukitangaza Kichina Nchini.

$
0
0
Khamisuu Abdallah na Madina Issa
MKUU wa Chuo Cha Uandishi wa bahari Zanzibar (ZJMMC) Saleh Yussuf Mneno amesema kuwa Chuo hicho kimeweza kupiga hatua za maendeleo katika kukuza lugha ya kichina kwa wanafunzi wa Zanzibar pamoja na kuitangaza lugha hiyo hapa nchini.

Kauli hiyo ameitoa katika hafla fupi ya kumuaga mkurugenzi wa mwanzo wa darasa la kichina Xu Shuang (Khadija) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa chuo hicho Vuga wilaya ya Mjini Unguja.

Alisema chuo hicho kimekuwa cha mwanzo kuitambulisha lugha hiyo kwani imekuwa ikikitangaza kutokana na wanafunzi wengi kulipenda somo hilo na kulifanyia kazi.

Aidha alifahamisha kuwa lugha hiyo imeweza kuwaletea mafanikio mengi ikiwemo kwa walimu kuweza kusoma elimu ya juu nchini China pamoja na mwanafunzi wao kwenda kwenye Radio ya CRI kwa ajili ya kazi maalum.

Hata hivyo mkuu huyo alimtaka Khadija kuwa kiongozi mzuri wa kwenda kukitangaza chuo hicho kwani imani yao ni kufanya kazi kwa pamoja na nchi ya China kwani wamekuwa wakiwasaidia katika nyanja tafauti Tanzania.

Nae mkuu wa Taaluma wa Chuo hicho, Rashid Omar Kombo alisema kwa upande wa taaluma wamefaidika kwani wanafunzi wapatao 350 wameweza kufaidika na lugha hiyo.

Alisema lugha hiyo ni muhimu kwa taifa la Watanzania kwani imeweza kukitangaza chuo chao sehemu mbalimbali.

Sambamba na hayo Rashid alisema kuwa Chuo hivi sasa kinajivunia ushirikiano wa China kupitia CRI na darasa la CONFUCIUS hivyo ameomba iendelee kufungua kurasa nyengine za kujenga mashirikiano zaidi.

Nae Mkurugenzi Xu Shuang (Khadija) alikipongeza chuo hicho kwa ushirikiano wao mzuri tokea afike na alisema kuwa amefarajika kwa kuwepo katika darasa hilo kwani ameweza kupata ushirikiano mzuri.

Aidha aliahidi kuwa balozi mzuri kwa nchi ya China kwani nchi ya Zanzibar imekuwa wakarimu na waelewa wa kufanya kazi kwa bidii zaidi.

Hata hivyo aliwataka wanafunzi hao kuendelea kujifunza lugha hiyo ili iweze kuwasaidia kujua lugha mbalimbali.

Xu Shuang (Khadija) ni mwalimu wa kwanza kwa Zanzibar kufundisha lugha ya kichina ambae alifanya kazi yake hapa Zanzibar kwa muda wa miaka miwili katika chuo cha Uandishi wa habari (ZJMMC).

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>