Ndege ya Serekali ya Oman ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, iliomchukuwa Waziri wa Habari wa Oman Dkt. Abdulmonam Al Hasani, na maofisa wa Wizara hiyo kuhudhuria Kongamano la Kimataifa la Historia ya Ustaarabu wa Kiislam,litakalofanyika kesho katika hoteli ya kitalii ya Lagema Nungwi.
Viongozi wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar na Balozi wa Oman Tanzania wakiwa katika uwanja wa ndege wa Zanzibar kuupokea Ujumbe wa Oman unaoshiriki katika Kongamano hilo lilliloandaliwa kwa Ushirikiano wa nchi tatu Zanzibar , Oman na Uturuki.
Waziri wa Habari wa Oman Dkt. Abdulmonam Al Hasani, wa kwanza kulia, akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume na Maofisa wa Wizara yake katikati Muhannad Al Raisi na Khalifa Al Darmaki.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Aki Juma Shamuhuna, akimsalimia Waziri wa Habari wa Oman Dkt. Abdulmonam Al Hasani, alipowasili uwanja wa ndege wa Zanzibar kwa ajili ya kuhudhuria kongamano la Historia ya Ustaarabu wa Kiislam.
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo, Said Ali Mbarouk, akisalimiana na mgeni wake Waziri wa Habari wa Oman, Dkt. Abdulmonam Al Hasani.alipowasili uwanja wa ndege wa Zanzibar kwa ajili ya kuhudhuria Kongamano la Kimataifa la Historia ya Ustaarabu wa Kiislam.Waziri wa Habari wa Oman Dkt. Abdul Monam Al Hasani, akiwa na wenyeki wake alipowasili Zanzibar
Mwenyekiti wa Nyaraka na Kumbukumbu wa Oman Dkt. Hamad Mohammed Al Dhiwiyan, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Ali Juma Shamuhuna, Waziri wa Habari wa Oman Dkt. AbdulMonam Al Hasani na Waziri wa Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Said Ali Mbarouk, wakiwa katika ukumbi wa VIP uwanja wa ndege wa Zanzibar baada ya kuwasili kwa Waziri huyo kuhudhuria Kongamano kesho katika hoteli ya Lagema Nungwi.
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Mhe, Said Ali Mbarouk, akizungumza na Waziri wa Habari wa Oman Dkt. AbdiulMonam Al Hasani, alipowasili Zanzibar leo kwa ajili ya kuhudhuria Kongamano la Historia ya Ustaarabu wa Kiislam linalotarajiwa kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein. kesho katika hoteli ya Lagema na kuwasilishwa mada 62.
Mwenyekiti wa Nyaraka na Kumbukumbu ya Oman Dkt. Hamad Mohammed Al Dhiwiyan, akizungumza na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Ali Juma Shamuhuna.
Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Maandali\ya Maandalizi ya Kongamano hilo Nd. Abdalla Mzee, akizungumza na Waandishi wa habari kukamilika kwa Kongamano hilo na matayarisho yote kukamilika na kuwasilishwa kwa Mada 62 naZanzibar kutowa Mada 4 zitakazowakilishwa na Jaji Mkuu Zanzibar Omar Makungu, Mada kuhusi Mahakama ya Kadhi Zanzibar kuazishwa kwake Zanzibar miaka hiyo.Dkt. Issa Haji Zidy , Dkt Amina Ameir Issa na Mwalimu Amour Abdalla Khamis.