Askari wa Usalama Barabarani Zenj akiongoza magari katika barabara ya makutano ya Malindi na Darajani ili kupunguza msongamano wa magari katika makutano ya barabara hiyo inakuwa na msongamano wakati wa mchana na kusababisha mlolongo mkubwa wa magari, eneo hilo lilikuwa na taa za kuongozea magari kwa sasa karibu kipindi kirefu huduma hiyo imaharibika na bila kufanyiwa matengenezo ya taa hizo. Katika mji wa Zenj taa hizo ziko katika sehemu mbili ya barabara zetu na kwa sasa zote hazitoi huduma ya kuongoza magari kwa kuharibika na bila kufanyiwa matengenezo.
↧