Utekelezaji wa sheria, uadilifu na kujituma kwa bidii
Na Bakar Mussa - Beijing, China .
Utekelezaji wa Sheria za Nchi, Uadilifu na kujituma kwa bidii kwa Wananchi na Viongozi wa China ndio siri kubwa ya mafanikio ya Kimaendeleo Nchini humo.
Hayo yalielezwa na Profesa , Liu Juinjie, kutoka Skuli ya Chama cha Kikomunisti cha China huko katika Hoteli ya Yongan , Mjini Beijing China , wakati alipokuwa akiwasilisha mada ya Mfumo wa Kisiasa nchini humo na Uzoefu wa Wananchi katika kujiletea maendeleo yao .
Alisema kuwa kumekuwepo Utii wa Sheria bila ya kuwepo mtu aliejuu ya Sheria za Nchi , kumepelekea nchi hiyo kupiga hatuwa kubwa ya Kimaendeleo ya Uchumi na Viwanda na kuwa miongoni mwa Mataifa tajiri Duniani.
“ Hakuna mtu aliejuu ya Sheria katika Nchi yetu ya China , hususana katika suala la kujiletea maendeleo na ndio nchi yetu tukawa tunapambana na Vitendo viovu vinavyo rejesha nyuma maendeleo yetu ikiwemo Rushwa “ alisema Profisa, Liu.
Profesa Liu Junjie alifahamisha kuwa kutokana na usawa huo mbele ya Sheria za nchi uliopo China , ndio Wananchi wake wanashikamana pamoja na kuwa bega kwa bega na Viongozi wao wa Serikali katika harakati za maendeleo chini ya Mfumo wa Chama Kimoja cha Kikomunisti
“ Mfumo wetu wa Chama kimoja tunaoendelea nao ni mzuri na unatufaa nchini kwetu kwa vile hatuna migogoro katika Uongozi wa Nchi , kwa vile Wananchi wetu na Viongozi wao daima wanashikamana lengo likiwa ni maendeleo mbele,” alieleza Profesa huyo.
Alisema kuwa Nchi ya China ambayo kwa sasa inakisiwa kuwa na zaidi ya Watu 1.3 Bilion,i itaendelea kuwa nchi ya Kimaendeleo kwa vile bado wanamkubuka Wasia wa Muasisi wa Chama hicho cha Kikomunisti , Hayati Mao Dztung, ambaye aliiwezesha Nchi hiyo kuwa na maendeleo ya haraka.
Hivyo alifahamisha kuwa China imekuwa ikipiga hatuwa kubwa ya Kimaendeleo siku hadi siku na kuleta mabadiliko ya kweli na haraka tafauti na nchi nyingi Duniani na kuiwezesha kuwa na marafiki wengi ambao wanasaidiana nao katika mambo mbali ya Kimaendeleo ya kila Sekta.