Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Misaada zaidi yapokelewa kusaidia kuhamasisha Vugu vugu la michezo

$
0
0
 Naibu Waziri wa Fedha wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Saada Mkuya akizungumza na  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati alipowasilisha mchango wake wa shilingi milioni 3,000,000/- kusaidia kufufua vugu vugu la michezo ndani ya maadhimisho ya kutimia miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali akipokea na kushukuru mchango uliotolewa na Naibu Waziri wa Fedha wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Saada Mkuya wa kusaidia kufufu vugu vugu la michezo hapa Nchini.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
 
 
Na Othman Khamis Ame, OMPR
 
Naibu Waziri wa Fedha wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  Saada Mkuya alisema juhudi na michango ya jamii bado inaendelea kuhitajika katika kuona Zanzibar inapata nguvu za ziada katika kurejea kwenye hadhi yake ya michezo Kimataifa.
 
Alisema  hilo linawezekana kutekelezwa vyema na jamii kwa vile kundi kubwa la Watu hasa Vijana na wasomi tayari wana  taaluma, Maarifa na uwezo wa kutosha kupitia Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 katika kuunga mkono suala hilo muhimu.
 
Naibu Waziri wa Fedha Saada alisema hayo wakati akikabidhi shilingi Milioni 3,000,000/- kama mchango wake binafsi kwa ajili ya kusaidia uhamasishaji wa Vugu vugu la michezo mbali mbali ndani ya maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayoendelea kufanyika nchini kote.
 
Mchango huo aliukabidhi kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo nyumbani kwake Mtaa wa Mazizini nje kidogo ya Mji wa Zanzibar na kushuhudiwa pia na Mwenyekiti wa Kamati ya kuhamasisha  Vugu vugu la michezo Zanzibar Mama Asha Suleiman  Iddi pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar { BTMZ } Sharifa Khamis.


Alisema matunda ya Mapinduzi ya Mwaka 1964 ndio yaliyowawezesha watu wengi hapa nchini kupata Taaluma na hatimae uwezo ambao umefikia wakati na  wajibu wa kusaidia mambo na harakati za kijamii hapa nchini.
 
“ Sisi wenyewe tumesomeshwa na Serikali katika hatua ya msingi hadi kufikia vyuo vikuu. Ukweli Serikali imefanya juhudi za  kuwekeza hasa katika sekta ya Elimu na sasa ina haki na wajibu wa kutumia matunda hayo “. Alisisitiza Naibu Waziri huyo wa Fedha wa SMT Saada Mkuya.
 
Akipokea mchango huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Zanzibar inastahiki kurejea katika zama zake za kuwa eneo maarufu  la vugu vugu ya michezo mbali mbali ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki na Dunia kwa ujumla.
 
Balozi Seif alisema historia ya Zanzibar inaonyesha wazi kwamba jamii ilikuwa ikipenda kushiriki mishezo mbali mbali ambayo kwa sasa imekuwa ikitajwa kama kumbu kumbu.
 
Aliishauri Jamii kushirikiana pamoja katika kuona Nyanja hii inafufuka na kurejea katika hadhi yake ya kawaida kwa kuwaandaa Vijana ambao ndio walio wengi kupenda kushiriki katika michezo hiyo.
 
“ Kama hatukuanza mapema kuwashika vijana hivi sasa kupenda kushiriki michezo tunaweza kujikuta asilimia kubwa ya vijana hao wanatumbukia katika vitendo viovu na kupoteza maadili yao “. Alifafanua Balozi Seif.
 
Naye kwa upande wake  Mwenyekiti wa Kamati ya kuhamasisha  Vugu vugu la michezo Zanzibar Mama Asha Suleiman alisema  Vijana lazima waungwe mkono katika kuona malengo yao waliyoyaweka katika kuendelea michezo yanatimia.
 
Mama Asha alimpongeza Naibu Waziri huyo wa Fedha wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mchango wake ambao utasaidia nguvu za kufufua vugu vugu la mishezo hasa ile ya ndani hapa Zanzibar.
 
Aliendelea kutoa wito kwa wananchi na washirika wa michezo ndani na nje ya nchi licha ya kuanza kijitokeza lakini sio vibaya  kuendelea kuchangia zaidi nguvu zao ili kufikia lengo lililokusudiwa.

 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>