Afisa vituo vya kulelea watoto yatima Idara ya Ustawi wa Jamii Zanzibar Lahdad Haji Chum akichangia katika mjada wa nini tufanye kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na (ZAPHA +) katika ukumbi wa zamani wa Radio Zanzibar
Maryam Charles Samwel mmoja ya vijana wanaosaidiwa kimasomo na (ZAPHA +) akizihamasisha Jumuiya nyengine kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na (ZAPHA +) katika ukumbi wa zamani wa Radio Zanzibar uliopo Rahaleo Mjini Unguja.
Baadhi ya washiriki wa warsha ya siku moja iliyojadili mchango wa jamii katika kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu, huko katika ukumbi wa zamani wa Radio Zanzibar uliopo Rahaleo Mjini Unguja.
Mwezeshaji wa warsha Bw. Mwalimu Wilson-olesira alie simama akizungumza na washiriki wa warsha ya kujadili mchango wa jamii katika kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu, katika ukumbi wa zamani wa Radio uliopo Rahaleo Mjini Zanzibar. Warsha hiyo ya siku 1 imeandaliwa na (ZAPHA +).
(Picha na makame Mshenga-Maelezo
Mkurugenzi Ofisi wa Elimu Maandalizi Msingi wa Vyuo vya Qur-an Zanzibar amesema suala la kubuni mbinu shirikishi kwa wadau na wanajamii ndilo ambalo litasaidia kutoa huduma endelevu kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Hayo yalielezwa katika warsha ililoandaliwa na Jumuiya ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi Zanzibar {ZAPHA PLUS} ililoshirikisha taasisi za serikali na jumuia za binafsi zinazoshughulikia watoto wanaoishi katika mazingira magumu iliofanyika katika ukumbi wa zamani wa Redio Zanzibar.
Aidha alisema lengo kuu ni kuona changamoto zinazowakabili pamoja na kujua ni jinsi gani watoto wataweza kusaidiwa na kupatia haki zao za msingi ikiwemo kivazi, elimu, malaji pamoja na huduma za kiafya.
Kwa upande wa washiriki katika kongamano hilo walisema kuwa wanahitaji mashirikiano ya pamoja katika jumuiya mbali mbali’ wanakamati, masheha wa shehiya na wanajamii kiujumla ili kufikia lengo la kuwakomboa watoto wanaoishi katika mazing ira magumu.
“Watoto wanaoishi katika mazingira magumu tuwakomboe vipi?”walisema washiriki.
Pia mmoja wa washiriki hao Dadi Ali Chum alifahamisha ipo haja ya kujua takwimu ya watoto ambao wanaishi katika mazingira magumu ili kuweza kuzisaidia familia zao.
Jumuia ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi inahusika na kutetea na kuhimiza huduma bora za tiba kushiriki katika mapambano dhidi ya ukimwi kutoa ushauri nasaha na lishe, elimu ya unyanyapaa kwa wanajamii kuhusu watoto wanaoishi na HIV/AIDS pamoja na kufanyakazi na watoto hao kwa lengo la kuwapa elimu ya stadi za maisha
Jumuia imeweza kuwasaidia watoto 749 wakiwa wanawake 386 nawanaume 360 kwa Unguja na Pemba katika kuwasaidia na hali ngumu za maisha.
Nae mratibu wa jumuiya hiyo Mussa Tano Juma alisema kuwa jumuia imeandaa vipindi mbali mbali kwa jamii ili kufanikisha maendeleo ya watoto hao.
Jumuia hiyo imeanzishwa mwaka 1994 ikiwa na wanachama 26 ikiwa na klabu moja ya watoto, na hadi sasa imefanikiwa kuwa na klabu kumi.