Ujumbe wa wadi za Makunduchi umeondoka leo kwenda Kiruna, Sweden kwa ziara ya kikazi ya siku nne. Ujumbe huo wa watu saba (wawili wakiwa hawapo kwenye picha) unaongozwa na afisa tawala wa wilaya ya Kusini, ndugu Abdallah Ali Kombo, (watatu kutoka kushoto). Wajumbe wengine kutoka kushoto ni ndugu Moh'd Simba, ndugu Mohamed Muombwa, ndugu Mwatima Hassan na Hafsa Makame. Wakiwa Sweden watatembelea viazio vya maji, sehemu za utalii pamoja na kutiliana saini mradi wa majaribio wa maji. Wadi za Makunduchi zinakabiliwa na uhaba wa maji. Manispaliti ya Kiruna na wadi za Makunduchi zimekubaliana kushirikiana katika masuala ya elimu pamoja na utalii unaojali mazingira.
↧