Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Vipaji vya soka viendelezwe - Ushauri

$
0
0
Na Mwajuma Juma 

AFISA Mtendji wa Kamati ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara Silas Mwakibinga amesema kuwa Zanzibar kuna vipaji vingi vya soka ambavyo kuimarika kwake vinahitaji kuendelezwa. 

 Akizungumza na waandishi wa habari juzi Mwakibinga alisema kuwa vipaji hivyo vya vijana kwa Zzanzibar vinaonekana vimeanzia tokea utotoni jambo ambalo lipaswa kushughulikiwa kwa kina ili kuweza kufikia malengo yake ya kuwa na soka bora katika Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla. 

“Mimi ni mara yangu ya kwanza kuja visiwani Zanzibar lakini kwa uono wangu nimegunduwa kuwa kuna vipaji ambavyo naamini vikiendelezwa vijana wenu watafikia hatua kubwa kisoka”, alisema. 

Alisema kuwa mfano hai ni kule kuona kuwa wachezaji wengi wa Zanzibar walioko Tanzania Bara wanaonekana kuwa wachezaji wazuri ambao wamesajiliwa katika vilabu tofauti. 


 Hivyo alisema kuwa ili kuona vipaji hivyo vinaendelezwa ni jukumu la waandishi wa habari kuelezea mazuri zaidi katika mpira wa miguu ili kuweza kuwavutia wafadhili. 

 Alisema kuwa waandishi wa habari wananafasi kubwa ya kukuza soka la Zanzibar ambalo kufanikiwa kwake litaweza kuipa sifa kubwa Zanzibar kitaifa na kimataifa. 

 “Habari zenu ndio zitakazowavutia wafadhili lakini zikichafuwa itakuwa vigumu kupatikana”, alisema. 

 Hivyo alishauri viongozi wanaoongoza soka kujaribu kuwa na ripoti nzuri za kiutendaji ambazo nazo zitakuwa ndio chachu ya kuweza kupata kwa wafadhili wengi ili kuimarisha mchezo huo visiwani Zanzibar

Mwakibinga alisema kuwa kila kitu kinahitaji fedha ili kuweza kufanya vizuri na vilabu vya Tanzania Bara vimekuwa vikipata ufadhili mkubwa katika ligi yao na kuvifanya kuifanya kuwa bora ligi yao.

 “Ligi ya Tanzania Bara imepanda kiwango chake kutokana na vilabu kuvuna fedha nyingi na wala tusifikie pahala tukadanganyana fedha ndio kila kitu katika kuleta ubora wa kitu”, alisema. 

 Hivyo aliwataka viongozi wa ZFA kujaribu kuandaa mipango madhubuti ambayo yatawawezesha kuiboresha ligi yao iweze kuwa bora zaidi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>