NAFASI ZA KAZI
Latif Primary School ni skuli mpya ya kisasa inayotarajiwa kuanza kwa muhula wa kwanza wa masomo mwaka 2014 inatangaza nafasi za ajira kwa ngazi zifuatazo.
1 Mwalimu Mkuu
Sifa za mwombaji
· Awe angalau na Diploma ya Ualimu.
· Awe si chini ya umri wa miaka 35
· Awe na uzoefu wa angalau miaka miwili katika nafasi ya Uwalimu mkuu, mkuu wa idara au nafasi yoyote ya uongozi katika elimu.
· Awe na uzoefu wa kusomesha usiopungua miaka 5
· Mwombaji mwenye diploma ya uongozi (management) atakuwa na kigezo cha nyongeza (added advantage)
· Awe ni mwenye tabia njema na mwenye kuheshimika
· Awe na uwezo wa kutumia computer hasa program za Microsoft Office
· Awe na uwezo wa kuzungumza,kusoma na kuandika Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha
2 Walimu wa kawaida (darasa la kwanza mpaka la tatu)
Sifa za mwombaji
· Awe angalau na Diploma ya ualimu msingi kati ya masomo ya Kiswahili English, Hesabati, Kiarabu, Dini, au Mazingira.
· Awe si chini ya umri wa miaka 25
· Awe na uzoefu wa kusomesha usiopungua miaka miwili
· Awe na uwezo wa kuzungumza,kusoma na kuandika Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha
· Uwezo wa kutumia computer utapewa kipaumbele
3 Msimamizi wa ofisi
Sifa za mwombaji
· Awe angalau na Diploma ya uhasibu
· Awe si chini ya umri wa miaka 25
· Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka miwili
· Awe na uwezo wa kuzungumza,kusoma na kuandika Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha
· Uwezo wa kutumia computer ni lazima
Jinsi ya kutuma maombi
· Barua za maombi ziambatanishwe na maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) pamoja na picha mbili za Passport size za hivi karibuni moja iandikwe jina nyuma
· Kwa urahisi wa mawasiliano, waombaji waonyeshe anwani na namba za simu za kuaminika, na barua pepe kama anayo
· Maombi yote yaambatane na nakala za vyeti vya kidato cha nne na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
· Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 9 Disemba 2013 saa 11 jioni
· Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na mwombaji anaweza kuwasilisha maombi yake kwa mkono kwa kufika jengo la skuli liliopo Malindi nyuma ya msikiti wa Ijumaa wa malindi karibu na Pyramid Hotel.
· Pia yanaweza kutumwa kwa njia ya posta au barua pepe kupitia anuani ifuatayo.
Mwenyekiti wa kamati
Latif Primary School
SLP 860
Zanzibar
Barua pepe almdrasatullatif@gmail.com
Nambari za simu : 0777 416 723 au 0772 000 550
NAFASI ZA MASOMO
Pia skuli hii inapenda kuwatangazia wananchi kuwa inaanza kupokea maombi ya wanafunzi wa darasa la kwanza mpaka la tatu kwa masomo ya msingi kwa muhula mpya wa mwaka 2014.
Latif Primary School ni skuli mpya na ya kisasa iliyopo Malindi, Zanzibar. Ni skuli Inayozingatia maadili ya Kiislamu na pia yenye kutoa elimu ya kisasa ikiwemo masomo ya computer
Fomu za uandikishaji zinapatikana katika jengo la skuli.
Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana nasi kupitia simu nambari 0777 416723 au 0772 000 550. Pia kwa kupitia barua pepe: almdrasatullatif@gmail.com
Pia unaweza kufika katika jengo la skuli liliopo Malindi nyuma ya msikiti wa Ijumaa wa Malindi karibu na Pyramid Hotel