Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Ujumbe wa Ijumaa

$
0
0

Mtume Swalla Allaahu ‘Alayhi Wasallam amesema

 كفى بالمرء كذبا أن يحدث بكل ماسمع (رواه مسلم)     

Yatosha kwa mja kuwa muongo akiwa ni mwenye kuhadithia kila analolisikia.  Muslim

Muumini wa kweli hutakuwa kuwa na hadhari ili asije kupigwa muhuri wa kuwa miongoni mwa wazushi. Kwani yanayosemwa kuna yaliyo kweli na mengini si kweli. Hivyo ikiwa kila tutakalosikia tutalisema tunaingia katika hatari ya kuwa miongoni mwa wanaosema uwongo.

Mwenye akili hufahamu kwamba si kila analolisikia linapaswa kuhadithiwa.

Ndugu zangu katika imani, tukiletewa habari yoyote ile kabla ya kuamua kuisambaza ni wajibu kwetu kuipima na kuiweka kwenye mizani kama inafaa kuhadithiwa kwani habari yaweza kuwa ni kweli na sahihi lakini haina faida wala maslahi kuhadithiwa. Inaweza kuwa ni ya uongo na haifai kabisa kuhadithiwa kwa kuweza kuleta fitna na migongano.

Inaweza kuwa ni ya kutungwa na hivyo kutuingiza katika kundi la wanaosambaza  uwongo na uzushi katika jamii.

Hivyo ni wajibu kwetu kuizingatia kwa mazingatio makubwa hadithi hii ya Mtume wetu na Ruwaza yetu Swalla Allaahu ‘Alayhi Wasallam hasa kwa tunaotumia mitandao iwe ya simu au ya intaneti, iwe ya blog au kwenye facebook, iwe ya twitter au instagram, iwe ya whats up au skype na mengineyo.

Tujichunge sana na kutuma au kusambaza habari tu pasi na kuzingatia mafundisho ya Mtume wetu Swalla Allaahu ‘Alayhi Wasallam.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles