Aliyekuwa Naibu wa Waziri wa Habari utamaduni na michezo katika Serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais mstaafu Amani Karume, Mahmoud Thabit Kombo ameongoza katika kura za maoni za kumtafuta mgombea Uwakilishi wa jimbo la kiembe Samaki ambalo limekuwa wazi baaada ya Mwakilishi wake Mansoor Yussuf Himid kuvuliwa uanachama katika chama chake cha CCM.
Mahmoud Thabit Kombo amepata kura 476 na hivyo kuwapita wagombea wengine kupitia CCM na sasa anangoja maamuzi ya wananchi siku ya uchaguzi.
Pichani Mahmoud Thabit Kombo alipokuwa akisaini kitabu cha wageni tarehe 27/11/2013 huku akisindikizwa na marehemu kaka yake Sir Jecha Thabit Kombo (kulia) aliyefariki karibuni.