Mhe Hamad Yussuf Masauni akihutubia na kutowa nasaha zake kwa Wanafunzi na Walimu waSkuli ya Rainbow wakati wa mahafali ya skuli hiyo kwa Wanafunzu wanaomaliza masomo yao ya Awali na kujiunga na Elimu ya Msingi na Mchipuo katika skuli mbalimbali Zanzibar na kuwataka kutumia elimu na mafunzo walioyapata kupitia Skuli ya Rainbow kuyatumia na kufaidika katika elimu yao huko wanakokwenda kuendelea na masomo yao.
Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Rainbow akisoma risala ya skuli yaombele ya mgeni rasmin Mbunge wa Kikwajuni Mhe. Hamad Yussuf Masauni katika mahafali ya Skuli yao yaliofanyika katika ukumbi wa skuli ya Haelisalasi.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe. Hamad Yussuf Masauni akimkabidhi cheti mwanafunzi wa Skuli ya Rainbow wa darasa la Maandalizi baada ya kumaliza elimu ya maandalizi na kujiunga na darasa la anza. Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe. Hamad Yussuf Masauni akimkabidhi cheti mwanafunzi wa Skuli ya Rainbow wa darasa la Maandalizi baada ya kumaliza elimu ya maandalizi na kujiunga na darasa la kwanza.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe. Hamad Yussuf Masauni akimkabidhi cheti mwanafunzi wa Skuli ya Rainbow wa darasa la Sita aliemaliza masomo yake ya msingi na kujiunga na Michipuo.
Wanafunzi wa Skuli ya Rainbow wakicheza ngoma ya kingazija wakati wa mahafali hayo.
Mbunge wa Kikwajuni Hamad Yussuf Masauni na Viongozi wa Skuli ya Rainbow,wakifuatilia maonesho hayo
Vazi la Kanga za KisutuVazi la Harusi huvaliwa wakati wa ndoa
Vazi la Kingazija hilo
Wakiwa katika Vazi la Kiafrika
Wakiwa katika Vazi la Kihindi
Wakionesha Vazi la Kimanga na Kiarabu katika maonesho ya mavazi
Wakiwa katika Vazi la Shela la Biarusi
Warembo wa Mavazi wakionesha mavazi mbalimbali katika mahafali hayo
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Hamad Yussuf Masauni akimkabidhi zawadi mwanafunzi wa maandalizi baada ya kushiinda mchezo wa kudaka mpira
Watoto wa skuli ya Rainbow wakionesha mchezo wa kuhesabuWanafunzi wa darasa la sita wanaomaliza masomo yao ya msingi katika skuli ya Rainbow wakionesha mchezo wa mafundisho ya Elimu ya Afya
Jeshi la skuli ya Rainbow likionesha ukakamavu wao katika sherehe za skuli yao zilizofanyika katika ukumbi wa skuli ya Haeli.
Wazazi wakipata picha za kumbukumbu kwa watoto wao wakati wa michezo katika mahafali hayo. kuweka kumbukumbu .
Hawa ndio Vinara wa Usafi kwa Mwaka huu wa 2013 katika Skuli ya Msingi ya Rainbow waliochukuwa nafasi ya kwanza kwa usafi wa mazingira kuazia masomo yao hadi mavazi wanapokuwa skuli hadi kuondoka, Miss Rahma Seif na Mr Husam Husein Mazrui.
Mhe. Masauni akiwa na Miss na Mr Rainbow wa mwaka huu 2013,waliofanya vizuri masomo yao na usafi wa mavazi na katika masomo yao Miss Rahma Seif na Mr. Hussam Husein Mazrui.wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Hamad Yussuf Masauni.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe. Hamad Masauni akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Skuli ya Rainbow na Wanafunzi wa Maandalini na Std 6 waliomaliza Masomo yao.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe. Hamad Yussuf Masauni akiwa katika picha ya pamoja na Walimu na Wahitimu wa Skuli ya Rainbow.
Wahitimu wa Skuli ya Rainbow ya Kisimamanjongoo Elimu ya Maandalizi wakiwa na Vyeti vyao baada ya kutunikiwa na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhe. Hamadi Yussuf Masauni, mahafali hayo yamefanyika katika ukumbi wa Skuli ya Haele Salasi.