Uwanja wa FNB ulimiminika watu mbali mbali mashuhuri duniani wakiwemo viongozi wa kitaifa kutoka nchi zisizopunguwa 100. Wote hawa wamekuja kuomboleza kifo cha kiongozi maarufu hapa duniani rais wa kwanza mwafrika Nelson Mandela. Viongozi mbali mbali walitoa hotuba akiwemo Rais wa Marekani Barack Obama ambaye alifuatana na mke.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, balozi Seif Ali Iddi alikuwa miongoni mwa viongozi wa ngazi ya juu waliohudhuria Maombolezi ya Kitaifa. Hapa anajitayarisha kuingia uwanjani akiongozana na mkewe mama Asha, Rosemary, mbunge mstaafu ambaye pia ni mtoto wa baba wa Taifa mwalimu Nyerere pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, ndugu Kinana.
Hivi ndivyo ilivyokuwa katika mji ya Afrika Kusini katika kipindi hichi cha msiba wa Nzee Mandela ulinzi umeimarishwa katika Uwanja uliofanyika Ibada maalum ya Kitaifa kuuombea Mwili wa Mze Mandela.