Mkurugenzi wa Elimu ya Msingi na Maandalizi Zanzibar Uleid Juma Wadi, akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mafanikio ya miradi ya ujenzi wa Madarasa ya Skuli Zanzibar yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika miradi hiyo, mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Eimu Mazizini
Waandishi wakifuatilia maelezo ya Mkurugenzi Uleid alipokuwa akizungumza na Waandishi.Jengo la Skuli ya Sekondari la Kiembesamaki Unguja
Sehemu ya ngazi ya Wanafunzi waliokuwa na mahitaji maalumu isiwe kikazo kwa kufika katika skuli hii kupata elimu ya sekondari
Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Mpendae Mbarouk Habibu, akizungumza na waandishi wa habari
Wanafunzi wa Kidatu cha Tano wakiwa katika darasa wakifanya mazoezi
Jengo la Skuli ya Mpendae ambalo linatarajiwa kufunguliwa katika sherehe za Mapinduzi hivi karibuni, jengo hili lina uwezo wa kuchukuwa Wanafunzi 800, hutowa Elimu ya Kidatu cha kwanza mpaka cha Sita, kwacsasa kuna wanafunzi wa Kidatu cha Tano wanapata elimu yao wakiwa jula yta Wanafunzi 62.
Darasa la Computer katika skuli ya Sekondari ya Mpendae. Afisa wa Elimu akizungumza na Waandishi wa habari waliotembelea miradi ya ujenzi wa skuli za Sekondari Zanzibar jumla ya skuli 19 zikiwa katika mrai huo tayari zimeshamaliza ujenzi wake na kutowa huduma na kufunguliwa rasmin katika sherehe za mapinduzi kutimia miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar.
Chumba cha Maabara ya Chemistry ya Skuli Mpya ya MpendaeWaandishi wa Habari wa Vyombombalimbali Zanzibar na Tanzania wakiwa katika ziara ya kutembelea miradi ya Ujenzi wa Majengo ya Skuli za Sekongari Unguja na Pemba, kupitia mkopo wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, wakiwa katika skuli ya Mpendae Unguja.