Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango wa Taifa wa Huduma za Fedha, wenye lengo la Kusimamia na kutatua ufumbuzi wa changamoto zinazozorotesha huduma za fedha nchini. Hafla hiyo imefanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
Malkia Maxima wa Uholanzi, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango wa Taifa wa Huduma za Fedha wenye lengo la Kusimamia na kutatua ufumbuzi wa Changamoto zinazozorotesha huduma za fedha nchini. Hafla hiyo iliyohudhuriwa pia na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dkt. Mohammed Gharib Bilal imefanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam,
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) , Prof. Benno Ndulu, akisaini mfano wa cheti cha Mpango wa Taifa wa Huduma za Fedha wenye lengo la kusimamia na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazozorotesha huduma za fedha nchini. Wanaoshuhudia nyuma (katikati) ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kulia kwake ni Malkia Maxima wa Uholanzi (kushoto) ni Naibu Waziri wa Fedha Sada Mkuya Salumu. Hafla hiyo imefanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati) Malkia Maxima wa Uholanzi na Naibu Waziri wa Fedha, Sada Mkuya Salumu, wakiwa wameshikilia Mpango wa Taifa wa Huduma za Fedha baada ya kuzinduliwa leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania.
Baadhi ya wadau wa Sekta za Fedha waliohudhuria uzinduzi huo wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, alipokuwa akihutubia, wakati wa uzinduzi