Rais waJamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa Ibada maalum ya mazishi Baba wa Demokrasia wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela iliofanyika kijijni kwao Qunu , Eastern Cape , Afrika Kusini Desemba 15, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) kwa hotuba ya kusisimua aliyoitoa wakati wa mazishi Baba wa Demokrasia wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela kijijni Qunu, Eastern Cape, Afrika Kusini leo Desemba 15, 2013. Kushoto ni Mwenyekiti wa SADC na Rais wa Malawi Mhe. Joyce Banda. Rais Kikwete alialikwa kuzungumzia sifa za mapambano ya ukombozi ya Mzee Madiba ambapo Tanzania ndiyo ilikuwa ni nchi yake ya kwanza kusaidia mapambano yote ya ukombozi kusini mwa Afrika.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na wageni wengine akitoka katika hema maalumu lililotumika kwa shughuli za mazishi Baba wa Demokrasia wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela kijijni Qunu , Eastern Cape , Afrika Kusini leo Desemba 15, 2013. Wa tatu kulia ni Mrithi wa kiti cha Ufalme wa Uingereza Prince Charles.(PICHA NA IKULU)