Na Ali Issa Maelezo
Rais mstaafu wa awamu ya sita wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Amani Abeid Karume amesema utengenezaji wa miundo mbinu ya Barabara ndio njia moja wapo ya kuinua Uchumi wa Nchi na kupelekea wananchi wake kuwa na kipato kizuri na kujikwamua na hali ngumu ya kimaisha.
Hayo ameyasema jana huko Zanzibar Beach Resrt Mzizini Mjini Unguja katika kongamano la sherehe za kutimiza miaka kumi wa mfuko wa barabara, sambamba na uzinduzi wa kitabu cha mfuko huo hotellini hapo.
Amesema nchi nyingi duniani zimepiga hatua kubwa za kimaendeleo na kuinua uchumi wa nchi zao kutokana na njia na ujenzi mkubwa wa kujenga Barabara.
Amesema hali hiyo ni ili zifanya nchi kusonga mbele ,hivyo mfuko huo nao hakuna budi kulifikiria ipasavyo.
Amesema iwapo na Zanzibar itafikia huko uchumi wake utakuwa kwa ubora jambo ambalo lina paswa kuigwa.
Nae katibu mkuu wizara ya fedha Khamis Mussa alisema barabara ni nafasi maalumu ya kuunganisha uchumi kwani wananchi hupata frusa ya kuweza kusafirisha mali zao kwa urahisi na kuyafikia mahitaji kwa haraka.
Aidha alisema kua mfuko wa barabara ulianzishwa kwa malengo maalum ikiwa ni pamoja wa kuangalia ubora wa barabara ,kutafuta mapato ya ujenzi wa barabara na kuangalia matumizi bora ya matumizi ya fedha zinazotolewa na wahisani na walipa kodi wa nchi hii.
Kongamano hilo la siku moja litajadili changamoto zinazoikumba mfuko huo na mafanikio yalio patikana kwa miaka kumi na kutafuta njia za utatuzi wa changamoto zinazoikumba mfuko huo.
Kongamano hilo limewashirikisha wajumbe mbali mbali kutoka Tanzania bara na Zanzibar wakiwemo mawaziri makatibu wakuu na wajumbe wa Baraza la wawakilishi.