Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Balozi Seif akutana na Kamisha Mpya wa Polis Zanzibar

$
0
0
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na  Kamishna Mpya wa Polisi Zanzibar  Bwana Hamdan Omar Makame aliyefika Ofisini kwake katika jengo la Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mbweni kujitambulisha rasmi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.
Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame akibadilishana mawazo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif hapo Ofisini kwake Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
 
Na Othman Khamsi Ame, OMPR
 
Jeshi la Polisi Nchini limetakiwa kuongeza ushirikiano wa karibu zaidi na Ofisi ya Mkurugenzi Mashtaka ili kuona imani ya wananchi  kwa jeshi hilo inaendelea kubakia wakati wote hapa Nchini.
 
Wito huo umetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akizungumza na Kamishna Mpya wa Jeshi la Polisi Zanzibar Kamishna Hamdan Omar Makame aliyefika kujitambulisha rasmi  hapo  katika Ofisi yake iliyopo kwenye jengo la Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
 
Balozi Seif  alisema wananchi wamekuwa wakilalamikia matatizo yanayojitokeza kwenye kesi mbali mbali zinazowahusu baadhi ya watu ambazo huleta athari ndani ya jamii  na baadhi yake hufifia bila ya  wahusika kutiwa hatiani kwa madai ya kukosekana kwa ushahidi.
 
Alisema hali hiyo ikiachiliwa kuendelea ambayo iko chini ya dhamana ya uwajibikaji wa vyombo hivyo viwili inaweza kuleta sura mbaya na matokeo yake itafikia wakati wananchi kujichukulia hatua mikononi mwao.
 
“ Tumeshuhudia matukio mbali mbali yenye kutia wasi wasi kwa  jamii katika maeneo yao vikiwemo vitendo vya mauaji, udhalilishaji, ujambazi na hata hili lililoibuka la watu kumwagiwa tindi kali. Lakini matokeo yake uchunguzi huo hufifia bila ya jibu muwafaka wanalolipata wananchi “. Alisisitiza Balozi Seif.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliutaka Uongozi wa Jeshi hilo kuzidisha mashirikano yake na wananchi pamoja na taasisi zote ili kuona  usalama wa raia na mali zao unaendelea kupatikana hapa nchini.
 
Balozi Seif alimueleza Kamishna huyo mpya wa Polisi Zanzibar kwamba Ofisi yake kwa vile ndiyo inayoratibu masuala yote ya Muungano hapa Zanzibar itakuwa tayari wakati wote  kumpa ushirikiano utakaomuwezesha  kutekeleza vyema jukumu alilokabidhiwa na Taifa  yeye na askari wake.
 
“ Ofisi yangu ndio iliyopewa jukumu la kuratibu masuala yote yanayohusu mambo ya Muungano kwa hapa Zanzibar. Hivyo nakuhakikishia kwamba mlango wa Ofisi yangu utakuwa  wazi wakati wowote unapopata tatizo la kiutendaji usione tabu kunifuata “. Alisisitiza Balozi Seif.
 
Hata hivyo Balozi Seif alimueleza Kamishna Hamdan Omar Makame   kwamba  ipo  changa moto hasa wakati wa muelekeo wa uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015 jambo ambalo jeshi hilo linapaswa kujipanga mapema katika kuhakikisha amani ya jamii inaendelea kuwepo Nchini.
 
Mapema Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame  alimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba atatekeleza vyema majukumu aliyokabidhiwa na Taifa katika misingi ya haki na uadilifu.
 
Kamishna Hamdan  aliyepewa jukumu la  kusimamia Kamisheni ya Polisi Zanzibar alieleza kwamba anachokitarajia katika  muda wote wa utumishi wake ni kupata ushirikiano wa karibu kutoka pande zote mbili zile za viongozi pamoja na raia wa kawaida.
 
Kamanda Hamdan Omar Makame  alipandishwa cheo na Jemedari Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete na kuwa Kamishna wa Polisi Tarehe 3/12/2013  na baadaye kuteuliwa kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar.
Nafasi hiyo ya Ukamishna Zanzibar ilikuwa ikishikiliwa na Bwana Mussa Ali Mussa ambaye kwa sasa ameteuliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Kamishna wa Polisi Jamii.
 
 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>