Makamo mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Makunduchi (Makunduchi Development Organization - MDO) ndugu Mohd Simba ametowa wito kwa wasomi kutoka Makunduchi kuungana na Jumuiya yake katika dhamira ya kuigeuza Makunduchi kuwa kijiji cha ICT.
Ndugu Simba ameyasema hayo katika mahafali ya kwánza ya kituo cha ICT cha Makunduchi ambacho kinaendeshwa na jumuiya hiyo.
Amesema ili malengo hayo yafikiwe ni lazima wananchi wa Makunduchi wajiunge kwa pamoja na kukipatia kituo hicho misaada inayohitajika kama vile kompyuta pamoja na walimu wenye sifa. Kwa kuanzia kituo hicho kinatoa mafunzo ya cheti lakini mipango imo mbioni kituo hicho kutoa mafunzo ya kiwango cha diploma na kuendelea.
Hivi karibuni kituo cha ICT cha Makunduchi ambacho kipo kwenye jengo la klabu ya Jamhuri ya Makunduchi kimejiunga na huduma za mtandao ambao gharama zake umelipiwa Waziri Kiongozi Mstaafu ambaye pia ni waziri wa ulinzi, ndugu Shamsi Vuai Nahodha. Jumuiya ya MDO imeundwa na vijana waliomaliza shahada ya kwanza katika vyuo vikuu mbali mbali. Miongoni mwa malengo yao ni kurejesha hadhi ya Makunduchi kwa upande wa elimu.