Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all 36244 articles
Browse latest View live

WAKUU WA MIKOA YA MBEYA NA RUKWA WAMTEMBELEA MTOTO ALBINO ALIYEKATWA KIGANJA.

$
0
0
Na Mbeya Yetu.                                                                                                                 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro aliongozana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhandisi Stella Manyanya walifika Hospitalini  baada ya mtoto huyo kufikishwa kwa ajili ya matibabu zaidi.

Mtoto huyo mkazi katika kijiji cha Ikonda kata ya Chitepa wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa alihamishiwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya baada ya kukatwa kiganja chake akitokea kituo cha Afya cha Kamsamba wilayani Momba mkoani hapa.

Akizungumza kwa masikitiko makubwa mama wa mtoto huyo, Prisca Shaban(28) alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa saba usiku alipokuwa anarudi ndani akitokea nje kujisaidia alivamiwa na mtu ambaye hakumfahamu na kisha akamsukumia ndani kabla ya kumpiga kichwani kwa rungu na kisha kupoteza fahamu.

Alisema akiwa amepoteza fahamu mtu aliyekuwa amemvamia ndipo alipata nafasi ya kuingia ndani na kutekeleza adhma yake ya kumkata kiganja mtoto huyo ambaye ni mmoja kati ya  watoto watatu wenye ualbino katika familia hiyo na kuondoka nacho.

Alisema wakati hayo yakitokea mumewe aliyemtaja kwa jina la Cosmas Lusambo alikuwa amekwenda kulala nyumbani kwa mke mdogo kwani ilikuwa zamu ya kwenda kulala huko kwa usiku huo lakini baada ya kusikia mayowe ya kuomba msaada alikwenda kuungana na familia yake na kumpeleka mtoto kituo cha afya cha Kamsamba kutokana na kuwa jirani na kijiji chao.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya, Akizungumza baada ya kumtembelea Baraka katika wodi ya watoto kwenye hospitali ya rufaa kanda ya Mbeya, alioneshwa kusikitishwa na tukio hilo na kuahidi kulifanyia kazi ili wahusika wapatikane na kuchukuliwa hatua.

Alisema ni tukio ambalo linasikitisha ambalo linazidi kuendeleza vitendo vya aibu kwa kuwafanyia ukatili wa kinyama albino kwa ujinga wa watu wachache wanaowadanganya watu kuwa viungo vyao ni bahati ya kuleta utajiri.

Mhandisi Manyanya mbali na kuzungumza na familia ya waathirika wa janga hilo pia aliongoza sara fupi ya kuwaombea albino hospitalini hapo alionesha pia kusikitishwa na mwenendo wa mashitaka ya watu waliofanya ukatili dhidi ya albino akisema mahakama zimekuwa na milolongo mirefu inayokatisha tama wadau wa kupinga ukatili huo.

Mkuu huyo wa mkoa alishauri pia kuangaliwa upya kwa sheria inayohusu masuala ya hukumu za kifo akisema ikibidi inapaswa kubadilishwa ili iweze kutoa haki kwa watu wanaofanya ukatili dhidi ya wenzao.

Alisema sheria ya sasa kumtaka rais pekee kuwa mtu wa mwisho kutoa uamuzi kunyongwa kwa mtu aliyehukumiwa inakosa nguvu ya kutekelezwa kutokana na majukumu mengi aliyonayo na kushauri kuwa ni vyema vyombo vya sheria vipewe mamlaka ya mwisho ya kutekeleza adhabu hiyo. 

Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya, Dk. Mpoki Ulisubisya akiwaongozwa Wakuu wa Mikoa ya Mbeya na Rukwa kuelekea Wodini kumjulia hali Mtoto Baraka aliyekatwa kiganja cha mkono wa kulia na watu wasiojulikana kijijini kwao juzi.
Wakuu wa Mikoa ya Mbeya na Rukwa wakimjulia hali Mtoto Baraka aliyekatwa kiganja cha mkono wa kulia na watu wasiojulikana kijijini kwao juzi.
Mtoto Baraka aliyekatwa kiganja cha mkono wa kulia na watu wasiojulikana kijijini kwao juzi akiwa amelala kitandani akiendelea kupatiwa matibabu.
Wakuu wa Mikoa ya Mbeya na Rukwa sambamba na viongozi wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya wakiwa wameinamisha nyuso zao huku wakisali kuwaombea watu wenye ulemavu wa ngozi ili wasipate madhara baada ya kumtembelea  Mtoto Baraka aliyekatwa kiganja cha mkono wa kulia na watu wasiojulikana kijijini kwao juzi.
Mama mzazi wa mtoto Baraka,Prisca Shabani akiwa na jeraha kichwani baada ya kupigwa na watu waliomkata kiganja mtoto wake, akiwa anawasikiliza wakuu wa mikoa ya Mbeya na Rukwa waliomfika kuwajulia hali katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya wanakopatiwa matibabu.

Magazetini Bongo Tz leo

Dkt.Bilal Akutana na Makamu wa Rais wa Shirika la Simu la Vietnam

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Makamu wa Rais wa Shirika la Simu Vitnam (VIETTEL) Hoang Son, wakati Makamu huyo alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Machi 9, 2015 kwa mazungumzo akiwa ameongozana na ujumbe wake. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Makamu wa Rais wa Shirika la Simu Vitnam (VIETTEL) Hoang Son (wa pili kushoto kwake)  na ujumbe wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Viettel Global, Tao Duc Thang, Mshauri wa Viettel Tanzania, Francis Mndolwa na  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Nguyen Thanh Quang, wakati Makamu huyo alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Kampuni ya Viettel, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika leo Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Machi 9, 2015 kwa.( Picha na OMR)

Katuni na Ujumbe wake huoooooooooooooooo

Balozi Seif Awaagiza Watendaji Hospital ya Mnazi mmoja kuacha Tabia ya Kuyafumbia Macho Matatizo.

$
0
0
Na Othman Khamis OMPR
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewaagiza  watendaji wa Hospitali Kuu ya Mnazi mmoja kuacha  tabia ya kuyafumbia  macho matatizo yanayoibuka katika utendaji  wao wa kazi na badala yake waiarifu Serikali Kuu ili hatua za dharura zichukuliwe katika kuyakabili matatizo hayo.
 
Alisema kuendelea kuyaacha matatizo hayo yasambae mbali ya  kuchafua mazingira lakini pia yanaweza kusababisha maambukizi ya maradhi na kuwaongezea wagonjwa mtafaruku unaoweza kuepukika.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa agizo hilo alipofanya ziara ya ghafla kuangalia hali ya usafi sehemu ya vyoo vya  wodi ya wagonjwa wa Kifua Kikuu katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar.

Ziara hiyo ya Balozi Seif  imekuja kufuatia Taarifa za Shirika la Utangazi Zanzibar      { ZBC } zilizoelezea hali isiyoridhisha katika sehemu hizo ambayo ilileta mtafaruku kwa Wagonjwa waliolazwa kwenye wodi hiyo.

Balozi Seif alisema yeye kama Kiongozi  Mkuu wa shughuli za Serikali atakuwa tayari wakati wowote kutoa msaada  au ushauri wake katika kutanzua matatizo ambayo Viongozi wa  Taasisi hiyo wameshindwa kuchukuwa hatua.


Alisema Wagonjwa pamoja na wananchi wamekuwa  wakilalamikia kero, changamoto na  hata matatizo yanayowakabili katika kupata huduma za afya kwenye  Hospitali ya Mnazi Mmmoja ambayo yamekuwa yakisababishwa na baadhi ya watendaji wazembe.

“ Msifikie pahala mkawa na tabia ya kuvilaumu  vyombo vya Habari kwa kuwapasha Habari Wananchi  juu ya uzembe mnaoendelea kuufanya katika maeneo yenu ya Kazi “. Alionya Balozi Seif.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alielezea kwamba Vyombo vya Habari vitaendelea kuwa na haki  na wajibu wa kutoa Taarifa kwa umma matukio ya uzembe unaofanywa na baadhi ya watendaji hao.

Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alifanya ziara ya kuwafariji wananchi wa Jimbo la Kwamtipura ambao nyumba zao zimeathirika kwa upepo mkali uliovuma ghafla juzi na jana mchana.

Balozi Seif ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Maafa Zanzibar alipata wasaa wa kuziangalia Nyumba sita za wananchi hao ambazo baadhi yake zimeezuka kabisa mapaa yake.

Sheha  wa Shehia ya Kwamtipura Bwana Machano Salum Khamis { Mbonga } alimueleza Makamu wa ili wa Rais Kwamba upepo huo uliovuma juzi na jana mchana umeezua baadhi ya mapaa nyumba sita ambazo nyengine zimepata athari na kuta zake.

Sheha Machano alisema uongozi wa Shehia ulikutana na waathirika hao kuanza kufanya tathmini ya hasara ya nyumba zilizopatwa na maafa hayo na kuchukuwa hatua za dharura  za uhifadhi wa familia hizo.

Naye Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipuira Mh. Hamza Hassan Juma alisema Uongozi wa Kamati ya Jimbo la Kwamtipura , wananchi na familia zilizopatwa na maafa hayo zilishirikiana pamoja katika kujaribu kurejesha hali ya kawaida ya mazingira ya nyumba hizo.

Mh. Hamza alisema hatua hiyo iliyochukuliwa ya  dharura kwa pamoja imeweza kuleta  faraja  kwa familia hizo kurejea katika mazingira ya hali ya kawaida.

Akizungumza na familia za waathirika wa maafa hayo ya upepo katika skuli ya Maandalizi ya Kwamtipura Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif aliwataka Wananchi hao mkuwa na subira katika kipindi hichi cha maafa.

Balozi Seif aliyeambatana na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi na kugawa sadaka kidogo kwa familia za maafa hayo alisema ameshtuka mara baada ya kusikia tukio hilo lililoleta hasara kubwa kwa familia hizo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  amewashukuru Wananchi na watu wenye uwezo kwa moyo wao waliouonyesha  katika kujaribu kusaidia familia hizo wakati wa tukio hilo.

Alisema linapotokeza tatizo miongoni kwa mmoja kati ya jamii ni vizuri tatizo hilo likawa na watu wote katika kulitafutia ufumbuzi wa pamoja na si vyema kwa baadhi ya watu kufurahia majanga yanayowapata wenzao kwa sababu tu za itikadi za kisiasa.

Nailsea Dental Firm Sends Supplies to Zanzibar

$
0
0

 

Sample News BigA Nailsea dental firm has sent hundreds of pounds worth of dental supplies to help an oral health project in Zanzibar.
 
Iqbal Fazal, the managing director of Dental Saver and owner of Smilesaver Dental Care, has sent a 20ft container filled with supplies over to Zanzibar in a bid to provide local people with basic dental care. The project is run by Health Improvement Project Zanzibar, a charity that was set up by consultant Ru MacDonagh. The charity has already built two medical centres.
 
Mr Fazal, who is originally from Kenya, was inspired to join forces with the charity after talking to his family GP, Dr John Rees, who has worked tirelessly with Mr MacDonagh to make a difference in Zanzibar.
 
Healthcare in Zanzibar is extremely basic and life expectancy is just 49 years old. The ratio of doctors to people is 1:50,000, which is significantly lower than the UK ratio of 1:400.
 
Mr Fazal has historical links with Zanzibar. Both his grandfather and uncle were orphaned there and the project has gained even greater importance and relevance since he was informed of this by his mother.
 
Mr Fazal has been working to fill the container for the last two years and it finally set sail to Zanzibar on Friday 7th March.
 

Balozi Seif Awatembelea Wananchi walioathirika na Upepo Kwamtipura

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa pamoja na watendaji wa wodi ya wagonjwa wa Kifua Kikuu alipofanya ziara ya ghafla katika Hospoitali Kuu ya Mnazi mmoja kuangalia hali ya usafi wa vyoo kwenye Wodi hiyo.Kulia ya Balozi Seif ni Mhandisi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Yahya Makame Ameir.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa pamoja na watendaji wa wodi ya wagonjwa wa Kifua Kikuu alipofanya ziara ya ghafla katika Hospoitali Kuu ya Mnazi mmoja kuangalia hali ya usafi wa vyoo kwenye Wodi hiyo.Kulia ya Balozi Seif ni Mhandisi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Yahya Makame Ameir.
Balozi Seif akiangalia hasara ilizozikumba baadhi ya nyumba zilizoathirika kwa upepo katika Jimbo la Kwamtipiura Mjini Zanzibar.Kulia ya Balozi Seif ni Sheha wa Shehia ya Kwamtipura Bwana Machano Salum Khamis, Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura Mh. Hamza Hassan Haji  na kushoto yake ni Mbunge wa Jimbo hilo Mh. Kheir Khamis. 
Balozi Seif alionyesha masikitiko yake wakati akiiangalia moja ya nyumba zilizopatwa na maafa ya upepo iliyopo pembezoni mwa skuli ya Msingi ya Kwamtipura.
Balozi Seif akiwafariji baadhi ya wananchi wa Jimbo la Kwamtyip[ura ambao Nyumba zao zimepata maafa ya Upepo mkali uliovuma juzi na jana mchana.
Balozi Seif akimkabidhi vyakula va baadhi ya Vifaa Sheha wa Shehia ya Kwamtipura Bwana Machano Salum Khamis kwa ajili ya kuwafariji wananachi  waliopatwa na janga na maafa ya upepo Kwamtipura.Kulia ya Balozi Seif ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi.
Balozi Seif akimkabidhi vyakula va baadhi ya Vifaa Sheha wa Shehia ya Kwamtipura Bwana Machano Salum Khamis kwa ajili ya kuwafariji wananachi  waliopatwa na janga na maafa ya upepo Kwamtipura.Kulia ya Balozi Seif ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi.(Picha na – OMPR)

Accounts Assistant/Cashier Looking for a Job

$
0
0
Hello
My name is Joseph Jotham. I am a Tanzanian young man aged 26. I hold a Bachelor degree in Banking and Finance from Institute of Finance Management (IFM). I am applying for a job in your esteemed company as an Accountant, Cashier, Credit Officer, Marketer and general administration as it may be available.
I am a hard-working and dedicated individual and I believe that my qualifications, skills and experience will add value to your organization. I am a fast learner who is willing to learn and eager for new professional challenges. From me you can expect passion and total dedication to the job.  I am immediately available and I will appreciate the opportunity to be invited for an interview.
Attached, please find my CV for your consideration. Looking forward to speaking with you, I thank you in advance.
Sincerely,
Joseph

0755-954 289


JOSEPH JOTHAM
P. O. Box 12957, Dar es Salaam
Mobile Phone: 0755-954 289

PERSONAL PARTICULARS
Date of Birth               :       4th August, 1988
Place of birth               :       Mbeya                                                    
Gender                                    :       Male
Nationality                  :      Tanzanian
Marital Status              :       Single
Current Residence      :       Dar es Salaam

EDUCATION BACKGROUND

Name of Institution
Years
Awards
Institute of Finance Management (IFM)
2010-2013
Bachelor of Banking and Finance

Sangu High Secondary   
School, Mbeya
2007-2009
Advanced Certificate for Secondary Education
Exams (ACSEE)
Sangu High Secondary   
School, Mbeya
2003-2006
Certificate for Secondary Education Exams
(CSEE)

WORK EXPERIENCE
Jan-Dec, 2014             Mbeya Cement Distributors and General Supplies Ltd
                                    Position: Accounts Assistant
                                    Duties and responsibilities:
·         Receiving payments and issuing receipts
·         Maintaining books of accounts of various branches
·         Posting entries and maintain transactions into journal
·         Processing invoice for payments to suppliers
·         Performing Cash and Bank Reconciliation
·         Performing Debtors/Creditor reconciliation
·         Preparation of monthly expenses report to management.
·         Preparing Profit & Loss, Balance Sheet and Cash flow statements
·         Creating stock orders from warehouse and supplying to clients
·         Performing stock reconciliation from branches

Aug-Dec, 2013           Bayport Finance Ltd
                                    Position: Credit Officer
                                    Duties and responsibilities:
·         Conducting promotions and marketing campaigns
·         Promoting and maintaining good business image of the company
·         Informing customers about various loan products and their terms
·         Informing clients of their loan repayment schedule and credit status
·         Maintaining and developing good relations with customers
·         Communicating with customers through visitations and by phone
·         Receiving and processing loan applications from customers
·         Scrutinizing forms and other documents submitted by customers

Aug-Oct, 2012            National Bank of Commerce (NBC), Mlimani City Branch
                                    Position: Customer Service Officer (Field Training)
                                    Duties and responsibilities:
·         Assisting customers to open new bank accounts
·         Providing customers with information about NBC products
·         Selling/cross-selling NBC products using a consultative approach
·         Providing customers with information on loan applications
·         Handling and resolving various queries from customers

OTHER SKILLS AND ATTRIBUTES
  • Self-motivated, creative, out-going and highly motivated
  • Excellent interpersonal, team work and multi-tasking skills
·         Ability to maintain records and prepare quality reports
·         Ability to work in a busy environment under little or no supervision
·         Fast leaner and with good judgment.

HOBBIES AND INTERESTS
Traveling, making new friends, reading newspapers and magazines and surfing the internet.
REFEREES:
Olympia Mfaume
Assistant General Secretary
TANESCO
P.O. Box 9024, Dar es Salaam
Mobile: 0754-553 126

Frank Kinkutta
General Merchant
FMK Company Ltd
P.O. Box 70507, Dar es Salaam
Mobile: 0754-285 118

Kain Patrick
Human Resources Officer
Akiba Commercial Bank
P.O. Box 669, Dar es Salaam
Mobile: 714-145 499




Taarifa kwa Vyombo vya Habari

$
0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA YA SHUGHULI ZA MKUTANO WA KUMI NA TISA WA BARAZA LA NANE LA WAWAKILISHI UTAKAOANZA TAREHE 11 MACHI, 2015

Mkutano wa Kumi na Tisa wa Baraza la Wawakilishi la Nane la Zanzibar unatarajiwa kuanza kesho siku ya Jumatano tarehe 11 Machi, 2015, saa 3.00 kamili asubuhi.

Shughuli za mkutano huo zitakuwa kama ifuatavyo:-
1.      Maswali  na Majibu:
Maswali 77 yatajibiwa kwenye mkutano huu.
2.      Miswada ya Sheria:
Miswada Minne (4) ya Sheria itawasilishwa na kujadiliwa,
Miswada yenyewe ni:-
(i) Mswada wa Sheria ya Kuweka Masharti ya Usajili na Usimamizi wa Wathamini na Mambo Mengine Yanayohusiana na Hayo.
(ii) Mswada wa Sheria ya Kuanzisha Kamisheni ya Ardhi na Mambo Mengine Yanayohusiana na Hayo.    
(iii) Mswada wa Sheria ya Kufuta Sheria ya Miradi ya Maridhiano Namba 1 ya 1999 na Kutunga Sheria Mpya kwa ajili ya Kuanzishwa na kuendesha mashirikiano baina ya Sekta ya Umma na Binafsi na Mambo Mengine Yanayohusiana na Hayo.
(iv) Mswada wa Sheria ya Kuanzisha Baraza la Sensa ya Filamu na Utamaduni Zanzibar na Mambo Mengine Yahayohusiana na Hayo.

3. Kuwasilisha mbele ya Baraza, Sheria ya Kura ya Maoni Nam. 11 ya 2013 ya Jamhuri ya Muungano kwa Mujibu wa Kifungu 132(2) cha Katiba ya Zanzibar.

4.  Taarifa za Serikali (Mawaziri) kuhusu Utekelezaji wa Maagizo ya Kamati za Kudumu za Baraza la Wawakilishi Mwaka 2013 /2014.

5. Ripoti za Kamati za Kudumu za Baraza la Wawakilishi za Mwaka 2014/2015.

6.   Taarifa ya Kamati Teule ya Upotevu wa Nyaraka.

7. Hoja ya Mjumbe kuhusu Ucheleweshaji wa Vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi.

(Yahya Khamis Hamad)
KATIBU
BARAZA LA WAWAKILISHI,

10 Machi, 2015.                                          ZANZIBAR.

ZIARA YA KINANA JIMBO LA LUSINDE

$
0
0
 Mbunge wa Jimbo la Mtera Ndugu Livingstone Lusinde akielezea maendeleo ya ujenzi wa Shule ya msingi Lowasa kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katika kijiji cha Muungano wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana(kushoto) akimuonyesha Mbunge wa Jimbo la Mtera Ndugu Livingstone Lusinde namna ya kufatua matofali wakati wa kushiriki ujenzi wa shule ya msingi Lowasa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupampu maji ya kisima cha mkono kilichopo katika shule ya msingi Mvumi Mission mara baada ya kukagua na kuuzindua mradi huo wa maji.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji Bi. Happiness Misile ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Shule mara baada ya kuzindua kisima cha maji katika shule ya Msingi Mvumi Mission.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi mara baada ya kuzindua kisima cha maji ambapo aliwaambia wananchi hao watunze  sana miundo mbinu ya maji.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Suli kata ya Mvumi Makulu ambapo alijionea ujenzi wa shule ya Msingi Suli unavyoendelea.

 Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mheshimiwa Farida Mgomi akimwagilia maji mti alioupanda katika shule ya Sekondari ya FUFU ikiwa sehemu ya utunzaji mazingira.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpa mkono wa pongezi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Fufu Hassan M.Kilindi kwa kuweza kujenga bweni zuri la wasichana shuleni hapo.
 Mbunge wa Jimbo la Mtera Ndugu Livingstone Lusinde akicheza ngoma wakati wa kuwasili kwenye uwanja wa mkutano wa hadhara uliofanyika Manzase.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kulia) akijadiliana jambo na Mbunge wa Jimbo la Mtera Ndugu Livingstone Lusinde (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Chamwino Ndugu Charles Ulanga kabla ya kuhutubia wakazi wa Manzase.
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutoka wilaya ya Chamwino akisalimia wananchi wa Manzase.
 Mbunge wa Jimbo la Mtera Ndugu Livingstone Lusindeakihutubia wakazi wa Manzase ambapo aliwaambia kuwa watendaji wa Serikali wajitahidi kufuata maagizo na maelekezo ya Mheshimiwa Rais kwa wakati.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Manzase na kuwaambia CCM Ipo Imara inajenga nchi na kuwataadharisha vijana wasikimbilie vyama visivyo na sera za maendeleo.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa Manzase wilaya ya Chamwino na kwenye mkutano wa hadhara wa CCM ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukagua, kusisitiza utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010.
 Wazee wakifuatilia kwa makini hotuba ya Kinana.
 Wananchi wa Manzase wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati akihutubia wakazi wa Manzase ambapo pia aliwasisitiza kujiandikisha kwa ajili ya kupiga kura.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi kadi ya uanachama wa CCM kwa Bi.Roda ambapo zaidi ya wanachama wapaya 750 walijiunga na CCM.
 Katibu Mkuu akiwashukuru wazee wa Manzase mara baada ya mkutano kuisha.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kushoto) pamoja na Mbunge wa Jimbo la Mtera Ndugu Livingstone Lusinde wakiwashukuru wananchi mara baada ya kumaliza mkutano katika kijiji cha Manzase,wilaya ya Chamwino.

USHIRIKINA CHANZO CHA MAUAJI YA WATU WENYE ALBINISM' - DK. ALLY POSSI

$
0
0
Na Andrew Chale                                                                                                          
Dk. Ally Possi ambaye ni Mhadhiri wa chuo kikuu cha Ardhi, Dar es Salaam. Akielezea na kuchambua kwa kina kuhusiana na wimbi la mateso na mauaji dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi wenye albinism.
Mo dewjiblog, iliamua kufanya mahojiano maalum ilikukuletea wewe msomaji wetu unayeperuzi mtandao wako bora kabisa kujua na kuelewa na nini kifanyike ikiwemo mimi na wewe katika kuchukua hatua.
Suala la mauaji dhidi ya watu wenye albinism:
“JAMII yenye ushirikina ndio yenye kuamini suala la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi ambao wana albinism, hivyo ilikuondoa imani hii potofu ni kutoa elimu katika maeneo yote na kuwalinda popote pale, Jambo hili ni jukumu letu sote” anabainisha Dk. Ally Possi.
Dkt. Possi anabainisha kuwa, Serikali itaendelea kulaumiwa mpaka hapo juhudi za dhati za kukomesha mauaji na vitendo vya kikatili vitakavyochukuliwa na kutokomezwa kabisa.
Fuatilia hapa Mahojiano hayo maalum.
DSC_0391
Mwanasheria na mhadhiri wa chuo kikuu cha Ardhi, Dk. Ally Possi akiwa kwenye ofisi za modewjiblog kabla ya mahojiano na mtandao huu.

MO DEWJI BLOG : Karibu, mgeni wetu katika mtandao huu wa kijamii unaokuletea habari bora kabisa zilizochambuliwa kwa kina za ndani, nje na makala maalum za kina.
DK. POSSI: Asante, nashukuru sana…
MO DEWJI BLOG: Unadhani nini chanzo na hali ya ongezeko la vitendo hivi kwa sasa hapa Tanzania?
DK.POSSI:“Kwanza mauaji ni.. yanatokana na imani potofu. Imani potofu kwa jamii kuwa ukipata kiungo cha alibino unafanikiwa.
Hii ni imani potofu kwa jamii ya watu wenye kuamini ushirikina.
“Albino ni ulemavu ambao mtu anakosa aina ya vitamin inayoitwa melaniani…
Inakosekana ikiwemo katika ngozi, nywele na macho” anaendelea kubainisha kuwa: Kuwa albinism ni hali ya kurithi kutoka kwa wazazi wote wawili ama mmoja. Ni kwamba baba na mama wanakuwa na vinasaba vinavyokuwa na albinism na vinapokutana wakati wa kutunga mtoto ndipo mtoto mwenye albinism anazaliwa.
MO DEWJI BLOG:Vipi inahusishwa na suala la Imani?
DK. POSSI:“Imani sio dini, Ni imani ya kishirikina.
“Sijui kitu gani ambacho kimetokea kikaleta hiyo imani, kwa kifupi ipo kwenye jamii iliyoendelea na uwezo wake wa kiuchumi ni mdogo na elimu pia.
Pia tunaweza kusema: “Suala hili ni la imani, Imani si ya dini, bali ni ya kishirikina. Kwa sababu kuna mtu anasema yeye muislamu ama mkristo.
Au kuna mtu ana Phd/ Profesa, ama amesoma elimu nzuri tu ama ana pesa anafanya biashara au mfanyabishara au mwanasiasa mwenye elimu yake nzuri lakini ametumbukia kwenye imani hii ya kishirikina.
DSC_0355
Mwanadishi wa habari wa modewjiblog, Andrew Chale akiwa kwenye mahojiano maalum na Dk. Ally Possi.
MO DEWJI BLOG: Kwa nini Kanda ya ziwa mauaji haya yamezidi kwa kasi?.
Dk. POSSI:“Kwanza kuna tatizo: Ofkozi..mauaji hayo Kanda ya ziwa mauaji yameripotiwa sana pia kuna Morogoro pia na sehemu nyingine.
“Serikali imekuwa kimya sana… katika mauaji yametokea husikii kiongozi mkubwa, ukiondoa Rais alivyosema (Machi 2-wakati wa hotuba ya mwisho wa mwezi wa Februari), lakini kiongozi mkubwa wa juu Waziri Mkuu, tangu mtoto Yohana yule wa Geita, Chato kukutwa ameuwawa
Sijasikia kauli nyingine zaidi ya Rais…Ambayo nayo ameitoa wiki mbili hadi moja na nusu, kupita ndio Rais anatoa tamko hilo.
“Nafikiri Serikali imekaa kimya kutoa matamko ama imekuwa ‘slow’ kuchukua maamuzi ama hatua stahiki hasa kwa watuhumiwa huko vijijini.
“Sote tumekaa vijijini ama tuna ndugu vijijini, Mtu anaweza kuibaa Baiskeli kijijini lakini masaa tu, anakamatwa. Lakini watuhumiwa wale wa vijiji wa mauaji ya watu wenye albinism kwa nini ichukue muda wasikamatwe?.
MO DEWJI BLOG:Tuambie inakuaje katika suala la kisheria?.
Dk. POSSI:“Sidhani kama kuna kitu kigumu kuwachukua watuhumiwa vijijini, wakati mtu akiiba baiskeli baada ya muda anakamatwa. Hapa nadhani suala la kisheria lipo kwa watu wote. Sheria inabidi ichukue mkondo wake kwa kuchukua maamuzi stahiki na ya haraka katika kuyafanyia kazi ikiwemo kuwakamata watuhumiwa popote walipo.

Benki ya Watu wa Zanzibar Wakala Wakuu wa EZYPESA Tanzania

$
0
0
Afisa wa Muandamizi wa Huduma kwa Wateja wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ)Ndg Anasi Rashid, akizungumza na Mawakala wa Kampuni ya Zantel wa EZY PESA, juu ya makubaliano ya kibiashara ya Ezypesa kupata fursa ya kupitisha fedha Mawakalwa wa Ezy pesa katika PBZ, kulia Mkurugenzi Masoko wa Kampuni ya Simu ya Zanztel Zanzibar Ndg Mohammed Mussa Baucha.

Maofisa wa PBZ wakifuatilia mkutano huo uliowashirikisha Mawakala wa EzyPesa jinsi ya kutumia PBZ katika kutowa huduma za Ezy Pesa ikiwa PBZ ni Mawakala Wakubwa wa Kampuni ya Simu ya Zantel katika Huduma ya EzyPesa. 
 Mawakala wa Ezy Pesa wakifuatilia maelezo kutoka kwa Maofisa wa PBZ wakitowa maelezo ya ufuguaji wa Akauti katika PBZ ili kuendesha biashara zao za EzyPesa kwa wateja wao.  



Mawakala wa Ezy Pesa wakifuatilia maelezo kutoka kwa Maofisa wa PBZ wakitowa maelezo ya ufuguaji wa Akauti katika PBZ ili kuendesha biashara zao za EzyPesa kwa wateja wao.
Afisa wa Benki ya Watu wa Zanzibar akitowa maelezo kwa Mawakala wa Ezy Pesa wakati wa mkutano huo wa kutowa Elimu ya mawakala kuweza kutumia PBZ kuweka fedha na kutowa fedha kwa ajili ya kuendesha Biashara yao ya Ezy Pesa kupitia PBZ. 
Afisa wa Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ akitowa maelezo kwa Mawakala wa EzyPesa wakati wa kufungua Akaunti ya PBZ kwa mawakala hao kupata huduma ya kibenki kwa kutumia simu zao kuweza kuwahudumia wateja wao wa EzyPesa wakati wowote bila kukwama kifedha.
Afisa wa PBZ akitowa maelekezo ya kujaza fomu ya ufunguzi wa akaunti katika PBZ mmoja wa Wakala wa EzyPesa, Mawakala wa EzyPesa wamepata fursa ya kufungua akaunti zao za kuendesha biashara hiyo kupitia PBZ ni Wakala wakubwa wa Ezy Pesa Tanzania. 
Afisa wa PBZ akitowa maelekezo ya kujaza fomu ya ufunguzi wa akaunti katika PBZ mmoja wa Wakala wa EzyPesa, Mawakala wa EzyPesa wamepata fursa ya kufungua akaunti zao za kuendesha biashara hiyo kupitia PBZ ni Wakala wakubwa wa Ezy Pesa Tanzania. 

Balozi Seif Awapongeza wananchi wa Kibweni kwa Ushirikiano wao kufanikiwa kuuzima Moto.

$
0
0
Na Othman Khamis OMPR
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewashukuru na kuwapongeza Wananchi wa Mtaa wa Kibweni  Wilaya ya Magharibi kwa moyo wao waliouonyesha katika kusaidia kuuzima moto ulioibuka majira ya saba 7.00 usiku juzi kwenye nyumba ya Sheha wa Shehia ya Kibweni Bibi Asha Ali Nassor.

Alisema licha ya kwamba vitu vyote vilivyokuwemo ndani ya chumba cha mmoja wa watoto wa Sheha huyo alitwae Asumini Moh’d Juma kuteketea kwa moto huo lakini juhudi za pamoja kati ya wakaazi wa nyumba hiyo na wananchi jirani zimesaidia kuepuka maafa zaidi katika janga hilo.

Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati alipofika Kibweni kuwafariji wakaazi wa nyumba hiyo na kuwapa mkono wa pole kutokana na maafa hayo akiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Magharibi Nd. Ayoub Moh’d Mahmoud.

Alishauri na kuomba mpango huo uendelezwe zaidi ili kutoa faraja kwa wananchi wanaopatwa na maafa katika matukio mbali mbali yakiwemo yale ya moto na hata ya tabia nchi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimtaka mpatwa na maafa hayo Bibi Asumini Moh’d  Juma kuwa na moyo wa subira katika kipindi hichi cha  mtihani na kumtakia hali ya utulivu katika maisha yake ya baadaye.


Mapema Mmmoja wa mashuhuda ya tukio hilo anayeishi ndani ya nyumba hiyo Abdulla Kombo Hamad alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwamba  moshi mkubwa uliotanda ndani ya nyumba hiyo ndio chanzo kilichowatanabahisha kuwepo kwa hali isiyo ya kawaida vyumbani humo.

Bwana.Abdullah  Kombo alisema wakazi wa nyumba hiyo kwa kusaidiana na majirani walilazimika kuvunja mlango wa Chumba kilichokuwa na moshi mwingi cha Bibi Asumini ambaye kwa wakati huo alikuwa Harusini na kufanikiwa kuuzima moto huo.

Alifahamisha kwamba baada ya kuangalia kwa kina chanzo cha moto huo walichodhania kuwa ni hitilafu za umeme, wakagundua  kuwa ni chupa ya mafuta ya Petroli iliyopenyezwa kwenye durisha la nyuma la chumba hicho.

Bwana.Abdullah  Kombo Hamad alielezea faraja yake baada ya kuona juhudi zao pamoja na majirani  zilisaidia kuudhibiti moto huo usiathiri mfumo wa waya za umeme zilizomo ndani ya nyumba hiyo.

Naye Mkaazi wa chumba hicho Bibi Asumini Moh’d Juma alisema kwamba moto huo umesababisha kuteketeza vitu vyote vilivyokuwa vimehifadhiwa  ndani ya chumba chake.

Bibi Asumini alivitaja baadhi ya vitu vilivyokuwemo ndani ya chumba chake kuwa  ni pamoja na kabati lililohifadhiwa nguo zote, Kitanda na Godoro lake,Charahani, vyakula pamoja na baadhi ya vitu vya ndani.

Alisema licha ya mtihani huo lakini anawashukuru watu wa wasamaria mbali mbali kwa moyo wao wa huruma waliomuonyesha wa kumpatia baadhi ya huduma zikiwemo nguo za kujistiri hali iliyompa faraja kubwa.

Ukiukwaji wa Sheria za Barabarani

$
0
0
Imekuwa ni jambo la kawaida kwa maderevya wa daladala kukiuka sheria ya usalama barabarani kwa kuegesha  daladala katika eneo siyo salama kwa watumiaji wa barabara hiyo na kuleta usumbufu kwa wakati wakiwa wameegesha, kama inavyoonekana daladala hizi zikiwa katika eneo la donge zikiwa zimeegeshwa kinyume na utaratibu wa sheria za barabara

Wataalamu wa Mafunzo ya Ujasiriamali Wawapatia Mafunzo Wanakijiji wa Kitogani Zanzibar.

$
0
0
 Kaimu Mkuu wa Taaluma wa Chuo cha Fedha Chwaka Zanzibar Dkt. Iddi Salum Haji akitoa mafunzo ya Ujasiriamali                                     kwa Wajasiriamali wa Kijiji cha Kitogani kilichopo Wilaya ya Kusini Unguja
Kaimu Mkuu wa Idara ya Masomo ya Jumla na Mafunzo Mafupi Zanzibar Nd. Said Mohammed Khamis akitoa                                                  ufafanuzi juu ya mafunzo hayo kwa Wajasiriamali wa Kijiji hicho.
      Baadhi ya Wajasiriamali waliohudhuria katika mafunzo ya Ujasiriamali wakisikiliza kwa makini mafunzo hayo.
 Afisa Tawala Wilaya ya Kusini Unguja Bi. Kibibi Mwinyi ambae ndiye Mgeni Rasmi wa kwanza kulia akiwasisitiza Wajasiriamali wa Kijiji cha Kitogani kuyafanyia kazi Mafunzo waliyoyapata katika Semina hiyo.

 Wakufunzi wa Mafunzo ya Ujasiriamali wakiwa katika picha ya pamoja na Wajasiriamali wa Kijiji hicho
                                         Wakufunzi wa Ujasiriamali wakiwa katika picha ya pamoja. 
                                                      (Picha na Miza Othman- Maelezo Zanzibar).

Warsha kwa Waandishi wa Habari Zanzibar Kuripoti Habari za Uchaguzi Zanzibar.

$
0
0

Mwenyekiti wa Warsha ya Waandishi wa Habari Mhe Salma Said,  kuhusiana na kuripoti Habari za Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar mwishoni wa Mwaka huu, warsha hiyo imewashirikisha Waandishi wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar, iliofanyika katika ukumbi wa jengo la Zanlink majestik Zanzibar.
Viongozi wa meza kuu wakisimama kwa dakika moja kuwakumbuka Mwakilishi waJimbo la Jimbo la  Magomeni Mhe Salmin Awadh na Mbunge wa Mbinga Magharibi, Mhe John Komba waliofariki dunia hivi karibuni.  

Waandishi wakisimama kwa dakika moja kuwakumbuka marehemu Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Zanzibar Mhe Salmin Awadhi na Mbunge wa Mbinga Magharibi Mhe John Komba, tayari walishafika mbele ya haki Mwenyezi Mungu awalaze mahali pema peponi Aman.
Waandishi wakisimama kwa dakika moja kuwakumbuka marehemu Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Zanzibar Mhe Salmin Awadhi na Mbunge wa Mbinga Magharibi Mhe John Komba, tayari walishafika mbele ya haki Mwenyezi Mungu awalaze mahali pema peponi Aman.
Mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya Jumuiya  Global Network of Religions for Children Dk Mohammed Hafidh, akifungua warsha ya Waandishi wa habari wa Vyombo mbalimbali kuhusiana na kuripoti habari za Uchaguzi Zanzibar iliofanyika katika jengo la Zanlik majestik Zanzibar.
Waandishi wakimsikiliza Mjumbe wa GNRC, Dk Mohammed Hafidh wakati wa ufunguzi wa warshi hiyo iliowashirikisha waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar jinsi ya kuripoti habari za Uchaguzi Mkuu Zanzibar. 
Waandishi wakimsikiliza Mjumbe wa GNRC, Dk Mohammed Hafidh wakati wa ufunguzi wa warshi hiyo iliowashirikisha waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar jinsi ya kuripoti habari za Uchaguzi Mkuu Zanzibar.
           Mkuu wa Taaluma Chuo cha Habari Hanzibar Ndg Rashid Omar Kombo akitowa Mada    kuhusiana na Misingi Mikuu ya Uandishi wa Habari za Uchaguzi na                     Utambuzi wa Viashiria vya Uvunjifu wa Amani, akiwasilisha mada     yake kwa Waandishi wa habari waliohudhuria Warsha hiyo ya siku moja iliowashirikisha Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali Zanzibar.

Mtoa Mada Mhe Ali Saleh akitowa Mada ya kuhusu Katiba wakati wa Warsha ya Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali Zanzibar iliofanyika katika jengo la Zanlink Majestiki Zanzibar 













Balozi Seif Atembelea Nyumba ya Sheha wa Kibweni Ilioungua kwa Moto

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiifajiri Familia ya Sheha wa Shehia wa Kibweni Bibi Asha Ali Nassor ambayo moja ya chumba cha nyumba hiyo kimeteketea na kuunguza vitu vyote vilivyokuwemo.kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Wilaya ya Magharibi Nd. Ayoub Mohammed Mahmoud.
 Balozi Seif akikagua hasara iliyotokana na moto katika chumba cha Nyumba ya Sheha wa Kibweni Bibi Asha Ali Nassor Wilaya na Magharibi Mkoa wa Mjini Magharibi.kushoto ya Balozi Seif ni Mkuu wa Wilaya ya Magharibi Nd. Ayoub Moh’d Mahmoud na kulia ya Balozi Seif ni Mmoja wa miongoni mwa wakaazi wa Nyumba hiyo Bwana Abdulla Kombo Hamad
Mtoto wa Sheha wa Shehia ya Kibweni anayeishi ndani ya chumba kilichoteketea kwa Moto Bibi Asumini Moh’d Juma akimueleza Balozi Seif mkasa ulimpata kutokana na maafa hayo ya moto.
.(Picha na Hassan Issa OMPR)

Zantel “ZALENDO CONCERT”

$
0
0
ZANTEL the cheapest network in Tanzania, last week organised an open concert in collaboration with Times FM dubbed “Tanzania Zalendo” which aimed at creating patriotism in the youth by unleashing their potential and to provide a platform to come together and work for self and societal development at Coco Beach Grounds.

Various undertakings were carried on the ground such as EzyPesa Registration, SIM Registration, and one to one interaction to discuss more with existing ZANTEL and the would be customers on Mpakabasi bundles which gives our customers better volume of minutes, SMSs and MBs for less.

The concert was well-crowded with the population of Dar es Salaam that arrived at Coco Beach to participate in the edutainment concert which gave them an opportunity to learn more about Zantel and its products and services.
                                                The rocking hip hop artist, Roma Mkatoliki on stage

                                             Roma Mkatoliki performing to the crowd (Pictures above)
                             Tunda Man on the ZANTEL Zalendo Concert entertaining the audiences



Baraka The Prince well known by his voice, amusing the crowd





Rais wa Zanzibar Dk Shein Akutana na Balozi wa China Ikulu leo.

$
0
0
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
  Zanzibar                                                                                                           10.3.2015
---
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa Zanzibar itaendeleza uhusiano na ushirikiano wa kihistoria uliopo kati yake na China na kusifu juhudi za nchi hiyo kwa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika sekta za maendeleo na uchumi.

Dk. Shein aliyasema hayo leo huko Ikulu mjini Zanzibar wakati alipokuwa na mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania Mhe. Lv Youqing aliyefuatana na ujumbe wake akiwemo Balozi mdogo anayefanyia kazi zake hapa Zanzibar Mhe. Xie Yunliang.

Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein alisisitiza kuwa Zanzibar inathamini uhusiano huo na ushirikiano na China ambao umeasisiwa na Marehemu Mzee Abeid Amani Karume na Marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere pamoja na kiongozi wa China wakati huo Marehemu Mao tse tung.

Dk. Shein alisema kuwa China inahistoria kubwa katika harakati zake za kuiunga mkono Zanzibar na ni miongoni mwa nchi za mwanzo zilizoyatambua Mapinduzi ya Januari 12, 1964 na kuanzia hapo hadi leo inaendeleakuwa bega kwa bega na Zanzibar.

“Zanzibar na China ni marafiki wa kweli... uhusiano wa Zanzibar na China ni wa kihistoria na ulianza mara tu baada ya Mapinduzi matukufu ya Januari 12, 1964 ambapo kuanzia hapo China imeweza kuiunga mkono Zanzibar katika shughuli zake mbali mbali hadi leo hii.. wananchi wa Zanzibar wanathamini uhusiano huu na watauendeleza’, alisema Dk. Shein.

Aidha, Dk. Shein alisema kuwa tokea wakati huo Zanzibar imeweza kupata misaada mbali mbali kutoa China hatua ambayo imeweza kusaidia mafanikio yake makubwa yaliopatikana hapa nchini hivi sasa.

Alisema kuwa China imeweza kuisaidia Zanzibar katika kuimarisha sekta mbali mbali za Maendeleo zikiwemo afya, elimu, kilimo, michezo na nyenginezo ambapo kwa upande wa sekta ya afya China imeendelea kutoa madaktari wake na wataalamu kuja kufanya kazi Zanzibar tokea mwaka 1964.

Kwa upande wa sekta ya michezo, Dk. Shein aliipongeza China kwa kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha miundombinu ya michezo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa uwanja wa Amaan mjini Unguja sambamba na kusaidia sekta hiyo kwa ujumla.

Kutokana na mafanikio hayo, Dk. Shein alisema kuwa azma ya China ya kuisaidia Zanzibar katika ujenzi wa uwanja wa mpira wa Mao tse tung itasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuimarisha sekta ya michezo sambamba na kusaidia shughuli nyengine za kijamii na kimaedeleo.

Dk. Shein pia, alimueleza Balozi huyo hatua zinazoendelea za ujenzi wa Hospitali ya Abdalla Mzee, Mkoani Pemba na kusisitiza kuwa ujenzi huo utsaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha sekta ya afya na kuimarisha huduma zake.

Pamoja na hayo, Dk. Shein alieleza hatua za ujenzi wa kiwanda cha Sukari Mahonda pamoja na viwanda vyengine vidogo vidogo viliojengwa wakati huo ambapo nchi hiyo imeweza kutoa ushirikiano na msaada mkubwa sambamba na kuendelea kutoa nafasi mbali mbali za mafunzo nchini humo na kuleta wataalamu wa sekta kadhaa.

Dk. Shein pia, alitumia fursa hiyo kumuelza Balozi Youqing kuwa miongoni mwa mafanikio makubwa yaliopatikana Tanzania kutokana China ni pamoja na ujenzi wa Reli ya TAZARA kati ya Tanzania na Zambia ambayo ni mfano mkubwa kwa nchi za Afrika.

Nae Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Lv Youqing alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa mafanikio makubwa yaliopatikana hapa Zanzibar na yanaoendelea kupatikana chini ya uongozi wa Dk. Shein katika sekta mbali mbali za maendeleo ikiwemo kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Pamoja na hayo, Balozi huyo alitumia fursa hiyo kumpongeza Dk. Shein kwa mara nyegine tena pamoja na Serikali anayoiongoza kwa kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Januari 12, 1964.

Balozi huyo wa China alimueleza Dk. Shein kuwa China inathamini sana uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu kati yake na Zanzibar na kuahidi kuuendeleza kwa manufaa ya pande zote mbili.

Balozi Youqing alimueleza Dk. Shein kuwa licha ya China kuendelea kuiunga mkono Zanzibar na Tanzania kwa jumla katika harakati zake za maendeleo nchi hiyo pia, inathamini sana juhudi za Tanzania katika kuiunga mkono nchi hiyo kwenye Umoja wa Mataifa.

Aidha, Balozi huyo aliipongeza Zanzibar kutokana na  mafanikio iliyoyapata kwenye sekta ya utalii huku akiendelea kusifu juhudi za kuendeleza amani na utulivu hapa nchini hatua ambayo imeendelea kuijengea sifa kubwa Zanzibar duniani kote kutokana na juhudi zake hizo.

Sambamba na hayo, Balozi huyo alitumia fursa hiyo kutoa shukurani zake na pongezi kwa Zanzibar ikiwa ni pamoja na kufikisha salam za Makamu wa Rais wa wa nchi hiyo Mhe. Li Yuanchao aliyetembelea Zanzibar hapo mwaka jana kutokana na ukarimu mkubwa na mapokezi aliyoyapata wakati wote alipokuwepo hapa Zanzibar.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

Katibu wa Baraza Azungumza kwa Kukamilika kwa Matayarisho ya Kikao cha Baraza Kesho.

$
0
0
Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Nd. Yahya Khamis Hamad akizungumza na waandishi wa habari kwa kutoa ufafanuzi kuhusu kikao cha Mkutano wa Kumi na Tisa (19) wa Baraza la Nane (8) la Wawakilishi unaotarajiwa kuanza siku ya Jumatano ya Tarehe 11 March, 2015
Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Nd. Yahya Khamis Hamad akijibu maswali yaliyoulizwa na baadhi ya waandishi wa habari wakati wa mkutano huo
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika mkutano huo wakimsikiliza kwa makini Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar. (Picha na Rahma Khamis Maelezo-Zanzibar).
Viewing all 36244 articles
Browse latest View live
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>