Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all 36165 articles
Browse latest View live

Kampuni ya Simu ya Vodacom Limited Inauza hisa (share) Zake Kupitia Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ Bank)

$
0
0
                  BENKI YA WATU WA ZANZIBAR
·  Kampuni ya simu ya Vodacom Limited inauzahisa (share) zake kupitia Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ Bank) kwa shilingi 850/- kwa hisa moja. Hii fursa pekee kwa wananchi wote wa Tanzania kuweza kuwekeza katika kampuni hio.
· Hisa hizo zita uzwa kuanzia tarehe 09/03/2017 hadi tarehe 19/04/2017 (Kwa kipindi cha wiki sita).
· Kiwango cha mwanzo cha manunuzi ni hisa (share) 100 kwa thamani ya shilingi 85,000 na anaweza kuongeza hisa 10, 10 kwa thamani ya shilingi 8,500/- kwa kila nyongeza.

· Kwa ajili ya ununuzi, utatakiwa kufanya malipo kwenye account ya ZanSecurities Limited yenye nambari 06107000074 iliopo Benki ya Watu Wa Zanzibar (PBZ Bank). 
· Baada ya kufanya malipo utajaza fomu maalumu ya kununulia hisa kulingana na kiwango cha fedha zako ulizolipa.
· Kwa maelezo Zaidi tafadhali fika kwenye tawi la Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ Bank) liliopo karibu yako.

PBZ BANK: BENKI YA WATU, CHAGUO LA WATU

Wafanyakazi wa Kampuni ya Pennyroyal Washiriki kufanya Usafi wa Mradi wa Best of Zanzibar Katika Ufukwe wa Pwani ya Matemwe Zanzibar.

$
0
0
Wafanyakazi wa Kampuni ya Pennyroyal Zanzibar wakishiriki katika usafi wa mazingira katika ufukwe wa pwani ya matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja,Mradi wa Best of Zanzibar unafanyia shughuli zake katika maeneo ya Kijamii ya Matemwe kwa kushirikiana na Wananchi wa katika kutoa Elimu ya Afya na Mazingira. Wakiwa na vipolo vya mabaki ya chupa za plastiki na taka nyengine ili kuuweka ufukwe huo katika hali nzuri ya mazingira. 












Yaliojiri Wakati wa Ziara ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC ) Ulipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Abiria Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.

$
0
0
Muonekano wa Jengo jipya la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume katika picha ndivyo utakavyokuwa baada ya kukamilika kwa ujenzi huo unaofanywa na kampuni ya kichina ya BCEG  ukiendelea na ujenzi wake katika hatua za umaliziaji wa mradi huo
Mjumbe wa Kamati Kuu ya  Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Guo Jinlong akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud wakati alipofanya ziara kukagua ujenzi wa Jengo la Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar alipokuwa katika ziara yake Zanzibar.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya  Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Guo Jinlong akisalimiana na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid wakati alipofanya ziara kukagua ujenzi wa Jengo la Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar alipokuwa katika ziara yake Zanzibar.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya  Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Guo Jinlong akisalimiana na Wafanyakazi wa Kampuni ya Ujenzi wa jengo hilo kutoka China. 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya  Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Guo Jinlong akimsikiliza Balozi wa China Nchini Tanzania Balozi Lu Youqing (mwenye koti jeusi) alipotembelea ujenzi wa jengo la Abiria katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar 
Sehemu ya jengo hilo la abiria likiwa katika muonekano wake 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Guo Jinlong, akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Kampuni ya BCEG inayojenga Jengo jipya la Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, akitowa maelezo miradi waliojenga nchini Tanzania. Alipotembelea jengo hilo
Mjumbe wa Kamati Kuu ya  Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Guo Jinlong , akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Kampuni ya BCEG inayojenga Jengo jipya la Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, akitowa maelezo miradi waliojenga nchini Tanzania. Alipotembelea jengo hilo
Wataalamu wa Kampuni ya BCEG inayojenga Jengo la Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume wakimshangia kiongozi wao alipotembelea mradi huo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya  Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Guo Jinlong akizungumza na Wataalamu wa Ujenzi wa jengo la Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume Zanzibar alipofika kutembelea Mradi huo.
Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mhe Balozi Ali Karume akizungumza na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Guo Jinlong, alipotembelea jengo hilo kujionea maendeleo ya mradi huo unaojengwa na Kampuni ya BCEG kutoka China
Mjumbe wa Kamati Kuu ya  Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Guo Jinlong 



Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanawema Shein, Ameutaka Uongozi wa Taasisi ya Zanzibalicious Women Group Kuongeza Kasi.

$
0
0
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar                                                                                                          26.03.2017
---
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein ameutaka uongozi wa Taasisi ya “Zanzibarlicious Women Group” kuongeza kasi ya kuendeleza shughuli zao kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Taasisi nyengine katika kupambana na vitendo vya udhalilishaji wanawake na watoto.

Mama Shein aliyasema hayo katika hotuba yake aliyoitoa katika hafla ya muendelezo wa Siku ya Wanawake duniani, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Hilton Double Tree, Shangani mjini Zanzibar.

Katika hotuba yake hiyo, Mama Shein alisema kuwa ni dhahiri kwamba jitihada za kuwasaidia wanawake wapate uwezo zaidi wa kufanya shughuli zaidi za kujiongezea kipato haziwezi kufanikiwa iwapo wataishi na hofu ya kufanyiwa vitendo udhalilishaji wao aau watoto wao.

Hivyo Mama Shein alisema kuwa taasisi hiyo ni vyema ikawa na mikakati madhubuti na kuungana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katikakupambana na vita hivyo.

Kwa kujua changamoto zinazowakabili watoto katika maisha yao Mama Shein alaisema kuwa jitihada za makusudi zinahitajika ili wasipoteze matarajio waliyonayo na kuwataka wazazi waendelee kuwaongoza, kuwafunza maadili mema kwa mujibu wa mafunzo ya dini silka na utamaduni wa Kizanzibari huku akiwataka watoto kuongeza bidii katika masomo yao.

Aliongeza kuwa jambo la kutia moyo ni kuwa Taasisi hii pia, inashughulikia ustawi wa watoto na hasa watoto wa kike na kueleza furaha yake kwa Taasisi hiyo imelitambua jukumunhilo wakiwa wanawake kwa kuwashughulikia waoto wao katika masuala mbali mbali yanayohusu ustawi wao.

Mama Shein alitoa wito kwa Taasisi hiyo kutokata tama kutokana na kukabiliwa na changamoto mbali mbali katika majukumu yao na kuwataka kuzitumia changamoto hizo kuwa ni fursa za kuwaletea maendeleo.

Alisekama kuwa jitihada za taasisi hiyo zinakwenda sambamba na mipango ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein katika kuwawezesha wanawake waliojiajiri wenyewe kwa lengo la kujiongeze kipato.

Sambamba na hayo, Mama Shein alitoa pongezi kwa Taasisi hiyo kwa kazi nzuri ambayo imekuwa ikiifanya tangu ilipoanzishwa na kuwataka kutambua kwamba Serikali inathamini sana kazi nzuri inayofanywa na Taasisi hiyo katika jamii.

Risala ya Taasisi hiyo ya wanawake iliyoanzishwa mwaka 2011 na kusajiliwa rasmi mwaka 2013 ilisomwa na Mtunza nidhamu wa Taasisi hiyo Shangwe Ramadhan Yussuf,ambayo ilieleza nia yake ikiwa ni kumuendeleza na kumuwezesha mwanamke kiuchumi, kijamii na ,imwenendo.

Aidha, risala hiyo ilieleza, changamoto, mafanikio na malengo ya Taasisi hiyo ambapo miongoni mwa malengo yake ni pamoja na kutoa eleimu ya ujasiriamali kwa vikundi mbalimbali vya wanawake na kuwawezesha kubuni biashara ndoho ndogo na jinsi ya kuweza kutafuta mitaji kutoka taasisi mbali mbali za kitaifa.

Mapema Waziri wa Kazi, Uwezeshajai Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto, Moudline Castico alitia pongezi kwa Taasisi hiyo na kueleza kuwa Wizara yake iko tayari kuendelea kutoa ushirikiano na Taasisi hiyo na nyenginezo zenye malengo kama hayo.

Pamoja na hayo, Waziri huiyo alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa Dk. Shein kwa kutimiza mwaka mmoja tokea kuingia madarakani katika awamu ya pili ndani ya Serikali ya Awamu ya Saba kutokana na ushisndi wa kishindo alioupata katika uchaguzi uliopita.

Nae Mlezi wa Taasisi hiyo ambaye pia, ni Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kiombo alieleza historuia fupi ya Taasisi hiyo na kupongeza juhudi inazozifanya katika kufikia malengo yake na kusisitiza haja ya kuungwa mkono ili izidi kupata mafanikio zaidi.

Katika hafla hiyo michango ya harambee ilifanyika ambapo Mama Shein akiwa mgeni rasmi alichangia Tsh. Milioni moja pamoja na kugawa vyeti  maalum kwa watu maalum kwa juhudi zao za kuiunga mkono taasisi hiyo.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

Mama Mwanamwema Shein Mgeni Rasmin Katika Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Duniani Yalioandaliwa na Taasisi ya Zanzibalicious Women Group Zanzibar Hoteli ya Double Tree Shangani.

$
0
0
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akipokelea na kukabidhiwa mauwa na Viongozi wa Taasisi ya Zanzibalicious Women Group ilioandaa Chakula Maalumu kwa kuadhimisha Siku ya Mwanake Duniani iliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Double Tree Shangani Zanzibar.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Viongozi wa Taasisi ya Zanzibalicious Women Group alipowasili katika viwanja vya hoteli ya Double Tree shangani Zanzibar kuhudhuria hafla ya kuadhimisha Siku ya Mwanamke Duniani ilioandaliwa na Taasisi hiyo.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Meneja wa Hoteli ya Double Tree Bi. Mary Njoroge alipowasili katika viwanja vya hoteli hiyo.
Mwanachama wa Taasisi ya Zanzibalicious Women Group Bi Mwanajuma Hussein akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani katika ukumbi wa hoteli ya DoubleTree Shangani Zanzibar.
Mzee kutoka Kijiji cha Chani Mohamad Khamis Haji akisoma dua kabla ya kuaza kwa hafla hiyo ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani. 
Mwakilishi wa Taasisi ya Zanzibalicious Women Group Bi Shangwe Ramadhan Yussuf akisoma risala na kuelezea madhumuni ya Taasisi yao kwa Jamii wakati wa hafla hiyo. 
Mwakilishi wa Taasisi ya Zanzibalicious Women Group Bi Shangwe Ramadhan Yussuf akisoma risala na kuelezea madhumuni ya Taasisi yao kwa Jamii wakati wa hafla hiyo. 
Mwanachhama wa Taasisi ya Zanzibalicious Women Group Bi Mwanajuma Hussein akimkabidhi zawadi Mlezi wa Taasisi hiyo Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, wakati wa hafla ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Double Tree Shangani Zanzibar.
Wageni waalikwa katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani wakishangilia. 
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akipokea Cheti cha heshima kwa Ushiriki wake katika Jamii akikabidhiwa na Mwanachama wa Taasisi ya Zanzibalicious Women Group Zanzibar Bi Mwanajuma Hussein, wakati wa hafla hiyo ya kuadhimisha Siku ya Wawanawake Duniani.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akionesha Cheti chake alichokabidhiwa na Taasisi hiyo kwa kuthamini mchango wake kwa Jamii.kushoto Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Mahmoud Thabit Komba na kulia Waziri wa Ajira Vijana Uwezeshaji wa Wazee Wanawake na Watoto Maudline Castico.  
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Mahmoud Thabit Kombo akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ilioandaliwa na Taasisi ya Zanzibalicious Women Group Zanzibar katika ukumbi wa hoteli ya Double Tree Shangani Zanzibar.
Waziri wa Ajira Vijana Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Mhe. Maudline Castico kazungumza kabla ya kumkaribisha Mke wa Rais wa Zanzibar kuzungumza na Wanachama wa Taasisi hiyo na Wananchi walioalikwa hafla hiyo kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ilioandaliwa na Zanzibalicious Women Group Zanzibar. 

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akizungumza wakati wa hafla hiyo akitowa nasaha zake kwa Uongozi wa Taasisi ya Zanzibalicious Women Group wakati wa kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani. ilioadhimishwa katika ukumbi wa hoteli ya Double Tree Shangani Zanzibar.


Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akizungumza wakati wa hafla hiyo akitowa nasaha zake kwa Uongozi wa Taasisi ya Zanzibalicious Women Group wakati wa kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani. ilioadhimishwa katika ukumbi wa hoteli ya Double Tree Shangani Zanzibar.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akikabidhi mchango wake kwa Taasisi ya Zanzibalicious Women Group shilingi milioni moja kwa Kiongozi wa Taasisi hiyo Shangwe Ramadhani Yussuf wakati wa hafla hiyo. iliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Double Tree Shangani Zanzibar.













 




Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Polepole Azungumza na Waandishi wa Habari.

$
0
0
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole, akzungumza na Waandshi wa habari katika Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam,leo. (Picha na Bashir Nkoromo)
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole, akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali katika Afisi Ndogo ya CCM lumumba jijini Da es Salaam.katika Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba. (Picha na Bashir Nkoromo)

Makamanda wa Polisi Kukutana Dodoma Kupanga Mikakati ya Kupambana na Uhalifu.

$
0
0


Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi.
Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi  wanatarajia kukutana mkoani Dodoma kuanzia Jumatatu tarehe 27-29/03/2017 katika kikao kazi cha siku tatu kujadili na kupanga mikakati mbalimbali ya kukabiliana na uhalifu na wahalifu hapa nchini.
Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake, Msemaji wa Jeshi la Polisi,  Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Advera Bulimba (pichani) alisema kikao hicho kitawakutanisha maofisa wakuu wa makao mkauu ya Polisi, makamanda wa Polisi wa mikoa na Makamanda wa vikosi bara na Zanzibar ili kujadili mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika utendaji katika kipindi cha mwaka uliopita na kuweka mikakati mipya ya kupambana na uhalifu kwa mwaka 2017.

Aidha, Bulimba alisema mbali na utaratibu wa mawasiliano ya kila siku katika kuimarisha usalama wa raia na mali zao, Jeshi la Polisi pia lina utaratibu wa kukutana kila mwaka kwa pamoja ili kubadilishana uzoefu kukabiliana na wahalifu kwa lengo la kuhakikisha kuwa usalama wa raia na mali zao unaendelea kuimarika hapa nchini.
“Katika kikao hicho Inspekta Jenerali wa Polisi IGP Ernest Mangu atatoa maelekezo ya kiutendaji ambayo lengo lake ni kuhakikisha kuwa kila ofisa,  mkaguzi na askari anawajibika kwa nafasi yake katika kuhakikisha uhalifu unapungua hapa nchini” Alisema Bulimba.

Bulimba alisema kikao kazi hicho kinatarajiwa kufunguliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba ambapo kauli mbiu katika kikao hicho ni “Zingatia maadili tunapopambana na uhalifu ili kuimarisha usalama kwa maendeleo ya Taifa”.


Mkuu wa Wilaya Ya Chake Pemba Afungua Mkutano Mkuu wa Saccos ya Walimu.

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Pemba, Mhe.Salama Mbarouk Khatib, akifunguwa mkutano mkuu wa Saccos ya Walimu Kisiwani Pemba , uliofanyika katika ukumbi wa Skuli ya Madungu Pemba.
Baadhi ya Walimu wa Skuli mbali Kisiwani Pemba, wakiwa katika mkutano wa uchaguzi wa Saccos yao uliofanyika humo katika ukumbi wa Skuli ya Madungu Chake Chake Pemba.
Baadhi ya Walimu wa Skuli mbali Kisiwani Pemba, wakiwa katika mkutano wa uchaguzi wa Saccos yao uliofanyika humo katika ukumbi wa Skuli ya Madungu Chake Chake Pemba.(Picha na HANIFA SALIM -PEMBA)

DKT ABBASI: Maafisa Habari Muungeni Mkono Rais Magufuli Kwa Kutangaza Mafanikio Ya Serikali

$
0
0
Na Ismail Ngayonga
MAELEZO
Morogoro
SERIKALI imewataka Maafisa Habari na Mawasiliano katika Wizara, Taasisi, Idara na Mamlaka za Mikoa na Wilaya nchini wametakiwa kutangaza mafanikio ya miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongoozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Hayo yamesemwa jana Mkoani Morogoro na Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi wakati alipokuwa akizungumza na Maafisa Habari na Maafisa TEHAMA katika mafunzo ya uwekaji wa taarifa katika tovuti za Mikoa na Halmashauri yanayofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID) na kusimamiwa na Ofisi ya Rais- TAMISEMI na Wakala ya Serikali Mtandao (EGA).

Kwa mujibu wa Dkt. Abbas alisema Serikali ya Awamu ya Tano inatekeleza miradi mikubwa ya maendeleo katika Mikoa na Halmashauri zake, hivyo ni wajibu wa Maafisa Habari kuhakikisha kuwa taarifa zinazowekwa katika tovuti hizo  zinaonyesha mafanikio ya Serikali katika utekelezaji wa miradi hiyo.

“Ipo miradi mikubwa inayotekelezwa na Serikali ikiwemo miradi ya umeme vijiji, ambapo Serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi hiyo, hivyo ni wajibu wa Maafisa Habari kuhakikisha kuwa taarifa za utekelezaji wa miradi inawafikia wananchi” alisema Dkt. Abbas.

Aliongeza kuwa  lengo la Serikali ya Awamu ya Tano inayooongozwa na Rais Dkt. John  Pombe Magaufuli ni kuleta matokeo ya haraka kwa wananchi wake, hivyo ni wajibu wa Maafisa Habari kuhakikisha taarifa mbalimbali za mafaniko katika maeneo yao ya kazi zinatangazwa kwa kuzingatia  muda na wakati.

Dkt. Abbas alisema kuwa Serikali ipo mbioni kuanza utaratibu wa kupima utendaji kazi wa Maafisa Habari na Mawasiliano katika Wizara, Taasisi, Idara na Mamlaka za Mikoa na Wilaya ili kuangalia ni kiasi gani wameweza kutangaza mafanikio ya Serikali katika maeneo yao ya kazi.

Kwa mujibu wa Dkt. Abbas alisema utaratibu huo wa upimaji utaweza kuainisha Wizara, Idara, Taasisi na Mamlaka za Mikoa na Wilaya  zinatoa na zisizotoa taarifa zake kwa umma, ambapo taarifa hiyo itaweza kuwasilishwa katika Mamlaka za juu Serikalini kwa ajili ya utekelezaji.

Aidha alisema kwa sasa suala la utoaji wa taarifa kwa umma si suala la utashi badala yake ni matakwa ya kisheria, hivyo Serikali inaandaa barua zitazoelezwa kwa Watendaji wakuu katika mamlaka za Serikali Kuu na Serikali za Mitaa kuhusu umuhimu wa utoaji wa taarifa kwa umma.

“Kwa sasa tuna sheria ya huduma za habari na sheria ya haki ya kupata taarifa, ambazo zote zinasisitiza na kutoa maelekezo kwa taasisi zote za umma kutoa taarifa kwa wananchi” alisema Dkt Abbasi

Alisema kuwa ili kutekeleza vyema majukumu yao msingi ni wajibu wa Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kuhakikisha kuwa wanatumia vyema mitandao ya kijamii katika utoaji wa taarifa za Serikali, kwani kwa sasa ulimwengu upo katika mabadiliko makubwa ya teknolojia ya habari na mawasiliano.

“Wananchi kwa sasa hawasubiri tena kusoma gazeti linalotoka siku ya pili asubuhi au taarifa ya habari katika redio na televisheni, badala yake wengi wao wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kupata taarifa za matukio ya moja kwa moja yanatokea katika maeneo mbalimbali nchini, hivyo ni wajibu wetu kutumia mitandao hiyo” alisem Dkt. Abbasi.

Mafunzo hayo ya uwekaji wa taarifa katika tovuti yamehusisha Mikoa 5 na halmashauri 33 zilizopo katika mikoa ya  Morogoro, Tanga, Simiyu, Kilimanjaro na Arusha.

Kamati ya Bunge Yawataka Watumishi wa Umma Kuchungamkia Nyumba Zinazojengwa na Serikali.

$
0
0
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),Mhandisi Elius Mwakalinga (wa tatu kulia), akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Fedha za Serikali (PAC), kabla ya kutembelea mradi wa ujenzi wa nyumba za Bunju B jijini Dar es Salaam jana zinazojengwa na wakala huo. Wa pili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Josephat Asunga.
 Baadhi ya maofisa wa TBA wakiwa kwenye mkutano na 
wajumbe wa kamati hiyo.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),Mhandisi Elius Mwakalinga (wa pili kushoto), akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Fedha za Serikali (PAC), walipotembelea mradi wa ujenzi wa nyumba Bunju B jijini Dar es Salaam jana. Wa nne kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Josephat Asunga.
 Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Josephat Asunga, akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa majumuisho ya ziara hiyo.
 Baadhi ya nyumba zinazojengwa katika mradi  wa Bunju B
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),Mhandisi Elius Mwakalinga, akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo.
 Baadhi ya nyumba zinazojengwa kwenye mradi wa Bunju B
Mwonekano wa nyumba hizo.

Na Dotto Mwaibale

WATUMISHI wa Umma wametakiwa kuchangamkia nyumba zinazojengwa na Serikali kupitia Wakala wa Nyumba Tanzania (TBA), ili kupata makazi bora baada ya kustaafu.

Wito huo umetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Josephat Asunga wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kutembelea miradi ya ujenzi wa nyumba inayofanywa na TBA jijini Dar es Salaam jana.

"Nawaomba watumishi wa umma kuzichangamkia nyumba hizi ambazo kwa  wao wanafursa ya kukopeshwa na kulipa deni polepole" alisema Asunga.

Alisema nyumba hizo zimejengwa na kuwekewa miundombinu mizuri hivyo kuwa ni sehemu bora ya kuishi.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Nyumba Tanzania (TBA), Mhandisi Elius Mwakalinga alisema nyumba zinazojengwa na TBA bei yake ni ndogo ukilinganisha na zile zinazojengwa na watu wengine.

"Hapa kwetu bei ya nyumba inaanzia sh.milioni 35 hadi milioni 200 wakati  maeneo mengine ni kuanzia sh.milioni 600" alisema Mwakalinga.

Alisema ujenzi wa nyumba hizo unakwenda sanjari na miundombinu yake na mahitaji mengine kama soko, bustani na  maegesho ya magari.

Alisema katika awamu ya tatu ya mradi TBA walipata mkopo wa sh.Bilioni 25 ambapo hadi Februari 2017 walipata mkopo wa sh.Bilioni 19.5 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za kuwauzia watumishi wa umma.

Alisema katika awamu ya pili ya mradi huo jumla ya nyumba 160 za aina tofauti zinaendelea kujengwa za zipo katika hatua mbalimbali, ambapo nyumba 64 zipo kwenye hatua za mwisho tayari kwa kuuzwa na nyumba 96 bado zipo kwenye hatua ya msingi na zilitarajiwa kujengwa kwa kutumia mfumo wa "Lunnel Forwork System"

Akizungumzia changamoto katika mradi huo alisema watu kujenga nyumba katika baadhi ya viwanja ndani ya eneo la mradi hivyo kupunguza idadi ya nyumba zilizokusudiwa kujengwa katika hatua za awali za awamu ya tatu ya mradi.

Alitaja changamoto nyingine kuwa ni kupatikana kwa malighafi mbalimbali za ujenzi hasa mawe, nondo hivyo kupunguza kasi ya ujenzi, upungufu wa fedha za utekelezaji wa mradi, kupanda kwa gharama za ujenzi kutokana na kupanda kwa bei za vifaa vya ujenzi.

Alisema ili kupunguza gharama za kununua vifaa vya ujenzi  wakala amekuwa akienda kuvinunua moja kwa moja kiwandani.

Diamond with Oman Air

AGPAHI Yaadhimisha Kilele Cha Siku ya Kifua Kikuu – Mererani Mkoa wa Manyara.

$
0
0

 
Picha ya pamoja katika maadhimisho ya kifua kikuu -  Mererani.

Shirika lisilo la kiserikali la Ariel Glaser Pediatric AIDSHealthcare Initiative (AGPAHI) linalojishughulisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI limeungana na wadau wote duniani katika maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani, 24 March 2017.

Maadhimisho hayo yalifanyika katika mji mdogo wa Mererani, wilaya ya Simanjiro katika Mkoa wa Manyara, eneo ambalo Shirika la AGPAHI linatekeleza mradi wa kutoa huduma shirikishi za kifua kikuu na UKIMWI sehemu za migodini kwa hisani ya shirika la ADPP la Msumbiji.

Katika maadhimisho hayo, shirika la AGPAHI kwa kushirikiana na timu ya afya ya wilaya walifanya zoezi la kutoa huduma mbalimbali kwa jamiii inayozonguka mji mdogo wa Marerani kuanzia tarehe 23 – 25 Machi, 2017.

Huduma zilizotolewa ni uchunguzi wa kifua kikuu, kupima Virusi vya Ukimwi na kutoa elimu kwa umma kuhusu kifua kikuu na VVU/UKIMWI.

Zoezi hilo lilisimamiwa na afisa mradi wa kifua kikuu na UKIMWI, kutoka AGPAHI, mratibu wa kifua kikuu na ukoma wa wilaya ya Simanjiro, wataalamu wa maabara, watoa huduma wa Afya kutoka kituo cha Afya Mererani na wahudumu wa afya ngazi ya jamii.

Kauli mbiu ya mwaka huu katika maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani ni; “TUUNGANE PAMOJA KUTOKOMEZA KIFUA KIKUU”.

Shirika la AGPAHI linafanya kazi katika mikoa sita ambayo ni Mwanza, Geita, Mara, Tanga Shinyanga na Simiyu. Huduma zitolewazo na shirika la AGPAHI ni kusaidia serikali kupitia vituo vya kutolea huduma za afya katika:

   1.Kutoa huduma za tiba na matunzo kwa watu
      wanaoishi na virusi vya UKIMWI;

   2.Kutoa huduma za kuzuia maambukizi ya virusi vya
      UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto;

   3.Kutoa huduma ya uchunguzi wa dalili za awali na
      huduma za awali za saratani ya mlango wa kizazi
      na

    4.Kutoa huduma shirikishi za kifua kikuu na UKIMWI
     sehemu za migodini.

Vilevile, shirika linafanya kazi katika mji mdogo wa mererani katika kutekeleza mradi wa kifua kikuu sehemu za migodini.

Matukio katika picha.

Afisa mradi wa Kifua kikuu na UKIMWI kutoka AGPAHI, Bi Alio Hussein akiwaelimisha na kugawa vipeperushi kwa wakazi wa Mererani kuhusu Kifua kikuu na VVU/UKIMWI.


Mhudumu wa afya ngazi ya jamii akiwaelezea wakazi wa Mererani dalili za Kifua Kikuu na namna ya kuweza kujikinga na maambukizi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.


Wahudumu wa Afya ngazi ya jamii wakichukua maelezo ya baadhi wakazi wa Mererani waliokua tayari kuchunguzwa kama wana maambukizi ya vijidudu vya Kifua Kikuu.


Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Kajolii Maasai akitoa burudani na kuendelea kuwahimiza wakazi wa Mererani kuja kupata Elimu kuhusu Kifua Kikuu.


Elimu kwa wachimbaji wa madini ya Tanzanite kuhusu Kifua kikuu na VVU/UKIMWI ikiendelea.


Wachimbaji wa madini ya Tanzanite katika Kitalu D, wakiwa wamekusanyika kwa wingi wakielimishwa kuhusu Kifua kikuu na VVU/UKIMWI.


Bi. Alio Hussein akiwaonesha kwenye picha namna ambavyo vijidudu vya Kifua Kikuu vinaweza kusambaa kama mgonjwa atakohoa bila kuziba mdomo.


Wachimbaji wakielimishwa kuhusu aina za Kifua
Kikuu kwa njia ya bango.




Maswali mbalimbali yakiulizwa kwa wachimbaji juu ya kifua kikuu na UKIMWI.


Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Kajolii Maasai akitoa burudani kwa wachimbaji wa Kitalu D waliokusanyika kwa wingi kuja kupata Elimu kuhusu Kifua Kikuu.


Mchimbaji wa madini ya Tanzanite akijibu swali lililoulizwa ikiwa ni mwendelezo wa kutoa elimu na uhamasishaji kuhusu Kifua kikuu na Ukimwi.


Wa kwanza kushoto ni Kajolii Maasai msanii wa muziki wa kizazi kipya, wa pili kushoto ni mchimbaji wa madini ya Tanzanite ambaye alijishindia Tishirt baada ya kujibu vizuri swali kuhusu Kifua kikuu na watatu kutoka kushoto ni Afisa mradi wa Kifua kikuu na UKIMWI, Bi Alio Hussein, na mwisho ni Mratibu wa Kifua kikuu na Ukoma Wilaya ya Simanjairo, Bi Selestina Rosai.


Na Joshua Fanuel wa Kilimanjaro Official blog,

PPF Yakabidhi Vifaa Tiba Katika Kituo cha Afya Longido.

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mhe. Jenista Mhagama,(watatu kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo,(wanne kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. William Erio, (watano kushoto), Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI (anayeshughulikia Afya), Dkt. Zainabu Chaula,(kulia), Mkuu wa Wilaya ya Longido, Mhe. Daniel Chongolo, (wapili kushoto), na viongozi wengine, wakiangalia kitanda cha kujifungulia wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba vilivyotolewa na PPF.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mhe. Jenista Mhagama,(watatu kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio, (wapili kushoto), Viongozi wa Mkoa wa Arusha na Wilaya ya Longido, wakitembelea wodi ya wagonjwa ya Kituo cha Afya Longido, ambapo ni moja kati ya vituo vilivyonufaika na msaada huo wa vifaa tiba kama sehemu ya mchango  wa PPF kwenye Jamii.

ZIRPP MONTHLY LECTURE

$
0
0
Dear Members and Friends,

I have the pleasure to kindly inform you that there will be another ZIRPP Monthly Lecture.

Chairperson: Mr. Muhammad Yussuf

Speaker: Mr. Suleiman Mahmoud Jabir
Subject: "Zanzibar's Membership to CAF and Its prospects for FIFA Membership"
Date & Time: Saturday 1st April 2017; at 4:00 pm.
Venue: ZIRPP Office,Third Floor, behind Majestic Cinema (above ZANLINK

ABSTRACT: The good news that came to being two weeks ago is the revelation that Zanzibar's long elusive membership to CAF has finally been realized. And as we are all aware, the process towards achieving CAF membership was extremely long, mountaineous and increasingly cumbersome, especially so taking into consideration that Zanzibar's long, tireless and steadfast efforts to FIFA membership ended up in total failure. 

In his presentation on the above-mentioned subject, Mr. Suleiman Mahmoud Jabir, a reknown sports expert and a long time member of the Zanzibar Council of Sports, will give his thoughts and revelations about the long process that characterized Zanzibar's increasing resilience and sense of purpose that effectively contributed to the achievement of being a member of one of the most important and prestigious global football organizations. He will also talk about the rights and obligations that ZFA will be subjected to in terms of the management of football tournaments in Zanzibar in line with CAF rules, regulations and requirements; as well as the prospects for future FIFA membership.    

Tea, Coffee and Snacks will be served freely.
 Please forward this message to anybody who may be interested. Those who would like to attend should send their email addresses and telephone numbers to: zirpp@googlegroups.com.
 
Please confirm your participation. You may bring one or two friends with you.

All are welcome.

Muhammad Yussuf
Executive Director
Zanzibar Institute for Research and Public Policy
P.O. Box 4523, Zanzibar, Tanzania;
Tel: +255 242 223-8474;
Fax: +255 242 223-8475;
Cellular: 0777 707820;
Website: www.zirpp.info

Katibu Mkuu Ikulu Mpya Ndg.Alphayo Kidata Aripoti na Kuaza Kazi Rasmin leo.

$
0
0

Katibu Mkuu Ikulu mpya Mhe Alphayo Kidata akilakiwa na Katibu Mkuu Ikulu Mstaafu Mhe Peter Ilomo alipofika kukabidhiwa ofisi katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 27, 2017
Katibu Mkuu Ikulu mpya Mhe Alphayo Kidata akisaini katika kitabu cha wageni baada ya kuwasili ofisini kwake kuanza kazi rasmi leo. Pamoja naye ni Katibu Mkuu Ikulu Mstaafu Mhe Peter Ilomo ambaye alimkabidhi rasmi ofisi  katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo.(Picha na Ikulu)


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.Mwigulu Awaasa Askari Kutowabambikizia Watu Kesi.

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe Mwigulu Lameck Nchemba akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha kazi cha Mwaka 2017 cha Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi
Mzee John Samwel Malecela akizungumza wakati wa kikao cha kazi cha Mwaka 2017 cha Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi
 Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe Mwigulu Lameck Nchemba akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha kazi cha Mwaka 2017 cha Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi
SACP Ramadhani Mungi Msimamizi wa bandari Tanzania na Kamanda wa polisi mkoa wa Lindi Renata Mzinga wakifatilia kwa makini kikao cha kazi cha Mwaka 2017 cha Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe Mwigulu Lameck Nchemba akisalimiana na Makamu wa kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Samwel Malecela mara baada ya kuwasili katika ufunguzi wa kikao cha kazi cha Mwaka 2017 cha Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe Mwigulu Lameck Nchemba akisalimiana na baadhi ya Maafisa wa jeshi la Polisi mara baada ya kuwasili katika ufunguzi wa kikao cha kazi cha Mwaka 2017 cha Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi
Kamanda wa Jeshi la Polisi nchini Ernest Mangu Akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kazi cha Mwaka 2017 cha Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Jordan Lugimbana akitoa salamu za Mkoa wa Dodoma wakati wa kikao cha kazi cha Mwaka 2017 cha Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi.

Na Mathias Canal, Dodoma
Askari na Maafisa wa jeshi la Polisi nchini wameaswa kutotumia madaraka yao vibaya kwa kuwabambikizia wananchi kesi kwani kufanya hivyo ni kushindwa kusimamia dhamira njema ya Mhe Rais ya kuwapatia wananchi wanyonge haki zao stahiki.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mhe Mwigulu Nchemba wakati akifungua kikao cha kazi cha Siku tatu cha mwaka 2017 kwa maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa LAPF Mjini Dodoma.

Mhe Mwigulu amesema kuwa kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya kuwabambikizia kesi, Kuwabadilishia watu kesi zao za msingi kwa sababu ya kushindwa kutoa rushwa hivyo kikao hicho kinapaswa kuwa na maamuzi na maadhimio yenye dira na taswira njema kwa jamii na Taifa kwa ujumla.

Amesisitiza pia Askari na Maafisa wa Polisi kutotumia taarifa za watu wanaohasiana kuwa ndio chanzo pekee cha msingi wa shtaka badala yake kufanya uchunguzi kwa kina na kujiridhisha vyema ili kufikia hukumu yenye tija Na haki kwa mtuhumiwa kwani kufanya hivyo kutaimarisha amani na jeshi la Polisi kupata taarifa nyingi za uhalifu kutoka kwa wananchi endapo watajikita katika haki.

Akizungumzia Vita dhidi ya Dawa za Kulevya Mhe Nchemba alisema kuwa serikali imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kukamata na kuziteketeza Dawa za kulevya zilizopo mashambani ambapo ametilia msisitizo zaidi kwa Askari na Maafisa wa Jeshi la Polisi kuendelea kupambana ili kuzikamata Dawa za kulevya zilizopo katika viwanda.

Amesisitiza pia Jeshi la Polisi kuendelea kupambana na kubaini uhalifu sambamba na kushirikiana na vyombo vingine ili kuhakikisha lengo mahususi la serikali ambalo ni kuzuia uhalifu linafanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Mhe Mwigulu amesema kuwa kauli mbiu ya Mwaka 2017 inayosema "ZINGATIA MAADILI TUNAPOPAMBANA NA UADILIFU ILI KUIMARISHA USALAMA KWA MAENDELEO YA TAIFA" endapo kama itatekelezwa kwa vitendo itaijenga nchi na kuzidi kudumisha zaidi amani iliyopo kwa wananchi.

Naye Kamanda wa Jeshi la Polisi nchini Ernest Mangu alisema kuwa kikao hicho cha kazi kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi kina dhamira kubwa ya kufanya Tathmini ya utendaji wa mwaka 2016 na kuandaa mikakati mizuri ya mwaka 2017 na kupata fursa ya kubadilika kiutendaji kwa kuzingatia dhamira ya serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Hata hivyo amesisitiza zaidi askari wote nchini kutofanya kazi kwa mazoea, Kuacha Urasimu na kujenga uaminifu na weledi katika kazi.

Mangu amesema matendo ya Askari Polisi nchini yanapaswa kuwa mfano bora wa kuigwa katika jamii hivyo askari Polisi hapaswi kuwa chanzo cha vurugu au kujihusisha na matendo ovu yasiyostahili katika jamii.

Ameongeza kuwa miongoni mwa mambo yatakayopewa kipaombele kwa kujadiliwa katika Kikao hicho itakuwa ni pamoja na Vita dhidi ya Dawa za Kulevya, Vita dhidi ya Magendo, Vita dhidi ya ujangili na Uvuvi sambamba na Vita dhidi ya Ubambikizaji wa kesi kwa wananchi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Jordan Lugimbana akitoa salamu za Mkoa wa Dodoma kabla ya kumkaribisha Waziri Mwigulu Nchemba kuzungumza na askari hao amelipongeza jeshi la Polisi kwa kazi kubwa linayofanya ambapo pia ameeleza mpango wa Mkoa katika kupambana na migogoro ya ardhi kwa kuanzisha kamati maalumu ya wataalamu wa sheria kutoka chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) Kupitia na kushauri ili kuweza kumaliza haraka migogoro hiyo.

Naye Makamu wa kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Samwel Malecela alisema kuwa jambo la msingi ambalo askari Polisi wanapaswa kulifanya ni pamoja na kuhakikisha kila mwananchi anapata Uhuru wake na kama jambo hilo likitekelezwa ipasavyo Fikra za Hayati Mwalimu J.K Nyerere zitakuwa zimeenziwa kwa weledi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Shein, Ahudhuria Taarab Rasmin ya Kumpongeza.

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,(katikati) wakifuatana na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud (mbele) walipokuwa wakiingia katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa Zamani jana katika Tamasha la Taarab rasmi ya kusherehekea Ushindi wa CCM na Kumpongeza Dk.Shein kwa kutimiza mwaka mmoja tokea kuchaguliwa kuwa Rais,[Picha na Ikul.]26/03/2017
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Juma Abdalla Juma (Mabodi),Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Mhe,Borafya Silima na Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto Mhe,Moudline Cyrus Castico (kulia) wakiwa katika Tamasha la Taarab rasmi ya kusherehekea Ushindi wa CCM na Kumpongeza Dk.Shein kwa kutimiza mwaka mmoja tokea kuchaguliwa kuwa Rais,katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa Zamani
Wakuu wa Wilaya mbali mbali za Unguja wakiwa katika Tamasha la Taarab rasmi ya kusherehekea Ushindi wa CCM na Kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa Zamani Mjini Zanzibar
Msanii wa Kikundi cha Taraab Calture Misical Club Iddi Suwedi alipokuwa akiimba wakati wa Tamasha la Taarab rasmi ya kusherehekea Ushindi wa CCM na Kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa Zamani Mjini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Juma Abdalla Juma Mabodi (katikati) wakiwa na Viongozi wengine katika Tamasha la Taarab rasmi ya kusherehekea Ushindi wa CCM na Kumpongeza Dk.Shein kwa kutimiza mwaka mmoja tokea kuchaguliwa kuwa Rais,katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa Zamani Mjini Zanzibar
Baadhi ya Viongozi mbali mbali wakiwemo Mawaziri wakiwa Tamasha la Taarab rasmi ya kusherehekea Ushindi wa CCM na Kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein    kwa kutimiza mwaka mmoja tokea kuchaguliwa kuwa Rais,katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa Zamani Mjini Zanzibar
Wasanii wa Kikundi cha Big Star cha Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mjini kikitoa burudani wakati wa Tamasha la Taarab rasmi ya kusherehekea Ushindi wa CCM na Kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein    kwa kutimiza mwaka mmoja tokea kuchaguliwa kuwa Rais,katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa Zamani Mjini Zanzibar
Msanii wa Kikundi cha Big Star cha Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mjini Munira Mngwame Ame alipotoa burudani ya wimbo na Kikundi chake jana wakati wa amasha la Taarab rasmi ya kusherehekea Ushindi wa CCM na Kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein    kwa kutimiza mwaka mmoja tokea kuchaguliwa kuwa Rais,katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa Zamani Mjini Zanzibar.
[Picha na Ikul.]26/03/2017. 

ZAECA Yafungua Ofisi Yake Kisiwani Pemba. (Mobile Office)

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Wete Pemba , Rashid Hadid Rashid, akizungumza na Wananchi waliohudhuria katika sherehe za uzinduzi wa Ofisi inayotembea ya Zaeca ( Mobile Office) huko katika Viwanja vya Jamhuri Garden Wete.
Ofisa wa Mamlaka ya kuzuwia rushwa na uhujumu uchumi Zanzibar (ZAECA) Mkoa wa Kaskazini Pemba, Abuubakar Moh'd Lunda, akizungumza na Wananchi waliohudhuria katika mkutano wa uzinduzi wa Ofisi inayotembea Zanzibar (Mobile Office)kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Wete , Rashid Hadid Rashid , ili kuzungumza na Wananchi na kufanya uzinduzi wa Ofisi hiyo huko katika Viwanja vya Jamhuri Garden Wete.
Baadhi ya Wananchi waliohudhuria uzinduzi wa Ofisi ya ZAECA,inayotembea iliofanyika katika Viwanja vya Jamhuri Garden Wete -Pemba
.(Picha na Hanifa Salim-Pemba.)

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli Apokea Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ikulu Jijini Dar es Salaam.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Nakala ya Vitabu vya  Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 Juni, 2016, kutoka kwa CAG  Profesa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa anapiga makofi pamoja na Katibu Mkuu Ikulu, Alphayo Kidata mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kupokea Ripoti hizo kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akifurahi pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad mara baada ya kupokea ripoti hizo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad akizungumza kabla ya kuwasilisha Ripoti hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kupokea Ripoti hizo ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kupokea Ripoti hizo ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa na Katibu Mkuu wa Ikulu Alphayo Kidata pamoja na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wakati akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Ripoti hizo kutoka kwa CAG Ikulu jijini Dar es Salaam.
Maafisa kutoka katika Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wakifatilia kwa makini wakati wa uwasilishwaji wa Ripoti hizo Ikulu jijini Dar es Salaam.  
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad mara baada ya kupokea ripoti hizo za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wakiwa katika picha ya pamoja.
(Picha na Ikulu.

Waziri Mkuu wa Tanzania Apokea Taarifa ya Tume ya Faru John.

$
0
0
Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa akipokea Taarifa ya Faru John kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele  taarifa ya Tume aliyoiunda ya kuchunguza suala la Faru John, ofisini kwake jijjini Dar es salaam Machi 27, 2017
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kukabidhiwa taarifa ya tume ya kuchunguza suala la Faru John na Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele, Ofisini kwake jijini Dar es salam
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkemia Mkuu wa Serikali , Profesa Samwel Manyele wakati  alipowasilisha taarifa ya tume ya uchunguzi wa suala Faru John baada ya kukabidhi taarifa hiyo , Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam.
(Picha na Ofisa ya Waziri Mkuu))
Viewing all 36165 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>