Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all 35978 articles
Browse latest View live

Waajiri sekrta binfasi wafikishwa mahakamni kisiwani Pemba

$
0
0
NA/ SAID ABDULRAHMAN PEMBA. 

 WAAJIRI wa sekta binafsi wapatao saba (7) wamefikishwa Mahakamani na mfuko wa hifadhi ya Jamii (Z.S.S.F) kutokana na makosa ya kutowasajili wafanyakazi wao katika mfuko huo pamoja na kutowalipia ada zao. 

 Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi huko Ofisini kwake Tibirinzi Chake Chake Pemba,Meneja wa Mfuko huo Tawi la Pemba, Rashid Mohamed Abdulla, alisema kwa mwaka 2016 – 2017 ni waajiri saba tu ndio waliyoweza kufikishwa katika vyombo vya sheria.

 Alieleza mfuko huo hauna nia ya kuwapeleka Waajiri Mahakamani ,bali kuna baadhi ya waajiri wanakwepa sheria ya kuzisajili taasisi zao pamoja na kuwasajili na kuwalipia wafanyazi wao waliowaajiri katika sekta zao.

 “Kuna baadhi ya waajiri ambao wanakwepa Sheria za kusajili taasisi zao hivyo kwa upande wetu tunatumia Sheria ya mwaka 2005, ambayo inatupa uwezo wa kuwapeleka Mahakamani ila tu kwa wale wakaidi ambao hawataki kufuata sheria lakini hatuna lengo la kufanya hivyo,”alieleza Meneja. Rashid, alifahamisha kwa sasa kesi ambazo zimeshafikia makubaliano ni kesi nne (4) ambapo tayari waajiri wa sekta hizo, wamekubali kuzisajili taasisi zao pamoja na wanyakazi wao na kuwalipia ada zao na kesi tatu (3) tu ndizo bado wanaendeleana nazo huko Mahakamani.

 “Kwa vile sisi mara nyingi huwa hatutaki kesi hivyo tunapofika kule mahakamani huwa tunajaribu kutafuta suluhu kwa upande wetu na kwa waajiri na anaekubali tu sisi tunaondosha shauri hilo Mahakamani,’alisema Meneja Rashid. 

 Meneja huyo, alisema kuwa endapo mwajiri huyo atakubali kulipia ada hizo hulazimika kulipa na faini japo kidogo kama ni adhabu yake. Hivyo alitoa wito kwa wenye taasisi binafsi kuzisajili taasisi zao pamoja na kuwalipia ada wafanyakazi wao na wasisubiri kusukumwa na kufikishana katika vyombo vya sheria kwani hilo sio zuri.

Balozi Seif akagua miradi mbali mbali ya kimaendeleo katika Wilaya ya Magharibi

$
0
0
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifanya mzaha na Wanafunzi wa Skuli ya Msingi ya Fuoni  Jimbo la Dimani baada ya kulikagua Jengo jipya la Skuli hiyo litakalosaidia kupunguza idadi kubwa ya Wanafunzi  madarasani.

 Balozi Seif na Baadhi ya Mawaziri na Watendaji Wakuu wa Serikali wakikagua shughuli za uwezekaji wa Jengo jipya la Skuli ya Msingi Fuoni linalojengwa kwa nguvu za Wananchi ambapo aliahidi kukamilisha ujenzi wake.

  Balozi Seif Kati kati akiwa na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud Kushoto yake na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed wakikagua ujenzi wa Nyumba za Makaazi katika Mradi wa Bakhresa Group Fumba.

 Balozi Seif akibadilishana mawazo na Uongozi wa Timu ya CPS Live Bwana Johan Vanden Abeele na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Bibi Katrin Dietzold wanaoendesha Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Makaazi katika  ukanda wa Maeneo huru ya Uwekezaji Fumba Wilaya ya Magharibi “B”.

 Pango la Maji safi na salama linalotoa Huduma za Maji na salama na kusambazwa katika Vijiji vilivyomo ndani ya Jimbo la Dimani.

 Mhandisi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar {ZAWA} Nd. Hussein Hassan Njuma  wa kwanza kutoka kulia akimuelezea Balozi Seif   aliyepo Kulia yake tatizo linalolikumba pango hilo la kupunguza kiwango cha idadi ya Lita zinazosambazwa kwa Wananchi kutokana na maji yake kuchanganyika na Chumvi baadhi ya wakati. 

Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Ardhi, Maji Nishati na Mazingira Mh. Salama Aboud Talib na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mheshimiwa Ayoub Mohamed Mahmoud.

 Balozi Seif na Ujumbe wake akimaliza kulikagua Jengo Jipya la Soko la Samaki  lililojengwa kwa nguvu za Wauvi  wenyewe wa Pwani ya Kichangani.

 Haiba nzuri inayoonekana ya Jengo Jipya la Skuli ya Bwefum Jimboni Dimani linalojengwa na Muwekezaji Mzalendo ambalo kukamilika kwake litatoa huduma za kitaaluma kwa Wanafunzi wa Wilaya Nzima ya Magharibi “B”.

 Meneja Mkuu wa Kiwanda cha uzalishaji wa maziwa Maeneo huru ya Uwekezaji Fumba Bwana  Adson Fagundes Kulia akimtembeza Balozi Seif na Ujumbe wake ndani ya Kiwanda hicho kujionea uzalishaji wa Bidhaa hiyo muhimu kwa afya za Wanaadamu.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na Viongozi wa Shehia zilizomo ndni ya Jimbo la Dimani katika Mkutano wake wa majumuisho ya ziara yake Jimboni humo hapo Skuli ya Kombeni.

Picha na – OMPR – ZNZ.

Bongo Magazetini leo Tz 15/7/2017.

Kocha Kwerekwe City aelezea siri ya mafanikio ya timu yake, apania kuipandisha daraja

$
0
0
 Kocha mkuu wa timu ya Kwerekwe City Suleiman Mohammed “Moo-Mani Gamera”

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Kocha mkuu wa timu ya Kwerekwe City Suleiman Mohammed “Moo-Mani Gamera” amesema siri kubwa ya timu yake ni umoja wao kati ya Wachezaji, Walimu, Viongozi pamoja na Mashabiki.

Amesema umoja ndo silaha kubwa kwao kwani wachezaji wao wana ari kubwa ya kuipandisha timu yao daraja la Pili Taifa ili msimu ujao wa mwaka 2017-2018 wacheze daraja hilo.

“Siri kubwa ya kufanya vizuri timu yetu ni umoja wetu kwa pamoja sote Walimu, Wachezaji, Mashabiki na Viongozi lakini pia ari ya Wachezaji wangu, nawapenda kwa vile wanapenda mazoezi, mpira mazoezi najivunia sana kwa hili naamini kwa asilimia kubwa tutapanda daraja”. Alisema Gamera.

Kwerekwe City juzi walianza vyema katika mchezo wa ligi ya Mabingwa Wilaya Daraja la Pili baada ya kuifunga Afrikan Boys mabao 4-0.

Mabao ya City siku hiyo yalifungwa na Saleh Massoud dakika ya 12 na 63, Abdallah Omar dakika ya 50 na Ally Mohd "Vially" dakika ya 90.

Mjini Unguja na JKU Academy watinga robo fainali mashindano ya Rolling Stone

$
0
0
Wachezaji wa kikosi cha kombaini ya Wilaya ya Mjini

Na: Said Salim “Hazard” kutoka Mbulu, Manyara.

Wawakilishi wa wawili wa Zanzibar katika Mashindano ya vijana ya Afrika Mashariki na kati ya Rolling Stone timu ya Mjini Unguja na JKU Academy watacheza hatua ya robo fainali leo mkoa wa Manyara na Arusha ambapo michezo yote minne ya hatua hiyo itapigwa saa 10:00 za jioni.

Kituo cha Mbulu Mkoani Manyara katika uwanja wa Julias Nyerere kutapigwa mchezo kati ya mabingwa watetezi Wilaya ya Mjini ya Zanzibar dhidi ya Lindi academy kutoka Lindi.

Na huko katika kituo cha Babati mkoani Manyara kutapigwa mchezo mmoja katika uwanja wa Babati kati ya Singi Academy dhidi ya Fire boys kutoka Karatu.

Na katika Mkoa wa Arusha kutapigwa robo fainal katika vituo viwili tofauti katika kiwanja cha Sheikh Amry Abeid mjini humo kutapigwa mchezo mmoja kati ya JKU academy kutoka Zanzibar dhidi ya Arusha central vijana kutoka hapo hapo Arusha.

Na huko katika kituo cha Mererani kutakua na mchezo mwengine wa robo fainali kati ya Saint Patrick dhidi ya Middle age.

Balozi Seif aipongeza Serikali ya China kwa kusaidia katika taaluma na huduma kwenye sekta ya afya

$
0
0
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Timu ya Wanahabari wa Kituo cha Matangazo ya Televisheni cha Kimataifa cha China {CCTV } iliyofika Ofisini kwake kumfanyia Mahojiano Maalum.
 Balozi Seif akimkaribisha Mtampta wa Timu ya Wanahabari wa CCTV aliyepo katika Kitengo cha Madaktari wa China  waliopo Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Bwana Zhou Ziyue { Maarufu – Juma }.
 Timu ya Wanahabari wa CCTV ikimpongeza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa kukubali ombi lao la kumfanyia Mahojiano Maalum kuhusu Historia ya Madaktari wa China wanaotoa huduma Zanzibar tokea miaka ya 60.
 Mhadhiri wa Chuo Kukuu cha Taifa cha Zanzibar {SUZA} wa Lugha ya Kichina  Profesa Li  Xany Alice kushoto  akimpongeza Balozi Seif kwa kukamilisha vyema Mahojiano yao.
 Timu ya Wanahabari wa Kituo cha Matangazo ya Televisheni cha Kimataifa cha China {CCTV }  ikiwa kazini kuchukuwa Picha ya Mahojiano baina ya Wanahabari wa Kituo hicho na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.

Balozi Seif akifurahia zawadi nzuri alizopewa kama ukumbusho kutoka kwa Timu ya Wanahabari wa Kituo cha Matangazo ya Televisheni cha Kimataifa cha China {CCTV } baada ya kumaliza Mahojiano yao.

Picha na – OMPR – ZNZ.


Na Othman Khamis, OMPR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameipongeza Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China kwa uamuzi wake wa kujitolea kwa dhati wa kuiunga mkono Tanzania na Zanzibar  katika kusaidia Taaluma na Huduma kwenye Sekta ya Afya.

Amesema mchango wa China katika sekta hiyo umewezesha Wananchi walio wengi Nchini kujihisi kwamba Wataalamu na Madaktari  hao wa Kichina wanaotoa huduma za afya Nchini kama ni miongoni mwa Ndugu zao wanaoshirikiana katika maisha ya Kawaida Mitaani.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa pongezi hizo hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar wakati akihojiwa na Wanahabari wa Kituo cha Matangazo ya Televisheni cha Kimataifa Cha China {CCTV}  ambapo wanahabari hao wapo Zanzibar kufanya kipindi Maalum kinachohusu Historia ya Madaktari wa China wanaotoa huduma za Afya kwa Takriban Mikaka 53 iliyopita.

Alisema Wananchi wa Zanzibar kwa kipindi kirefu wamekuwa na ukaribu na Madaktari wa Kichina kutokana na Wataalamu na Mabingwa hao mahiri katika utendaji kazi wao kuzingatia zaidi maadili yaliyowawezesha kujenga sifa na Heshima kubwa.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwahakikishia Wanahabari  hao wa Kituo cha Matangazo ya Televisheni ya CCTV kwamba  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na China katika kuona malengo ya ushirikiano yaliyofikiwa kati ya pande hizo mbili karibu Miaka 53 iliyopita nyuma yanafanikiwa ipasavyo.

Akizungumzia ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii  uliopo kati  ya China na Bara la Afrika Balozi Seif alisema yapo mafungamano mazuri yaliyofikiwa kupitia Mpango Maalum ulioanzishwa wa China – Africa ambao tayari umeshaanza kuleta mafanikio.

Alisema ushirikiano wa Kiuchumi na Kitaalamu ambao China imejikubalisha kusaidia zaidi Taaluma  Kwenye Mataifa ya Bara la Afrika umesaidia kuibua Wataalamu wa Kizalendo katika Mataifa hayo ambao wameanza kusaidia nguvu za uzalishaji unaozingatia Teknolojia ya Kisasa.

Balozi Seif alifahamisha kwamba miradi ya Maendeleo hasa katika sekta za Miundombinu ya Mawasiliano, Afya, Kilimo, Utamaduni, Michezo na hata shughuli za Kijamii chini ya usimamizi wa Mabingwa na Wataalamu wa China imeanza kushuhudiwa ikipiga hatua kubwa za maendeleo.

Hata hivyo Balozi Seif aliielezea Timu hiyo ya Wanahabari wa CCTV kwamba China bado ina safari ndefu ya kuendelea kulisaidia  Kitaaluma Bara la Afrika katika  azma ya Bara hilo ya kujikomboa  na umaskini hasa kwa Mataifa ya Jangwa la Sahara.

Matokeo kidato cha sita yatangazwa leo

$
0
0
Matokeo ya kidato cha sita nchini  yametolewa leo Jumamosi, Julai 15, yameonyesha kuwa wasichana wameongoza kwa ufaulu ambapo  kati ya wasichana 28,731 (38 asilimia) waliofanya mtihani, waliofaulu ni ni 27,577 (sawa na asilimia 97.21).
Jumla ya watahiniwa 75, 116, walifanya mtihani huo Mei mwaka huu.
Kwa upande wa watahiniwa wavulana,  waliofaulu walikuwa ni 42,975 (sawa na asilimia 95.34) kati ya  46,385.

Taarifa iliyotolea inaonyesha kuwa watahiniwa 58,556 (asilimia 93.72) walipata daraja la kwanza hadi la tatu. Kati ya hao, wasichana ni 22, 909 na wavulana ni 35,647.
“Mchanganuo wa ufaulu katika madaraja unaonyesha kuwa watahiniwa walipata daraja la 1-11  umepanda  kwa asilimia 0.59 kutoka asilimia 93.13 mwaka 2016 hadi 93.72 mwaka huu,” imesema taarifa hiyo na kuongeza;

“Pia, ufaulu katika madaraja kwa upande wa wasichana umepanda ikilinganishwa na wavulana. Ubora wa ufaulu kwa wasichana ni asilimia 94.07 ikilinganishwa na asilimia 93.49 ya wavulana.”

Ufaulu wa masomo
Kadhalika taarifa hiyo imeonyesha kuwa ufaulu kwa watanikiwa wa shule kwa upande wa masomo, ya Sayansi, Biashara, Lugha na Sanaa, haukuonyesha tofauti kubwa ukilinganisha na mwaka jana.

Hata hivyo, ufaulu katika somo la General Studies umeshuka kwa asilimia 7.54 kutoka asilimia 71. 24 hadi 63.70.


TOVUTI YA BARAZA LA MITIHANI TANZANIA (NECTA)

MATOKEO KIDATO CHA SITA (ACSEE) 2017

MATOKEO YA DIPLOMA YA UALIMU (DSEE) 2017

MATOKEO YA CHETI CHA UALIMU (GATCE) 2017


Shule kumi bora na zilizoshika mkia katika matokeo ya kidato cha sita

$
0
0

Shule kumi bora ni 
  1. Feza Girls
  2. Marian Boys
  3. Kisimiri (Arusha)
  4. Ahmes ( Pwani)
  5. Marian Girls
  6. Mzumbe
  7. St Marry Mazinde Juu
  8. Tabora Boys
  9. Feza Boys
  10. 10.Kibaha ( Pwani)
Shule kumi  zilizoshika mkia ni 

1 Kiembesamaki Unguja, 
2 Hagafilo (Njombe),
3 Chasasa (Pemba), 
4 Mwenyeheri Anuarite (Dar es Salaam) 
5 Ben Bella (Unguja).
6 Meta (Mbeya), 

7 Mlima Mbeya(Mbeya)
8 Shule ya Sekondari ya Mbeya (Mbeya),

9 Al-Ihsan Girls (Unguja 
10 St Vicent(Tabora).

Kombaini Wilaya ya mjini yatinga Fainali mashindano ya Rolling Stone

$
0
0

Na:Said Salim “Hazard” kutoka Mbulu, Manyara.

Mabingwa watetezi wa Mashindano ya Vijana ya Afrika Mashariki na Kati ya Rolling Stone timu ya Kombain ya Mjini Unguja imefanikiwa kutinga hatua ya fainali baada ya wapinzani wao Saint Patrick Academy ya Arusha kushindwa kusafiri kwenda Mbulu Mkoani Manyara wakitokea huko Arusha kucheza na wapinzani wao Mjini mchezo ambao wa nusu fainali ulikuwa usukumwe kesho majira ya saa 10 za jioni katika uwanja wa Julius Nyerere.

Akithibitisha taarifa hizo Mwenyekiti wa Mashindano hayo Wilium Zongwe (Dell Piero) amesema Saint Patrick Academy wameshindwa kwenda huko Mbulu kutokana na gharama za fedha hivyo Mjini Unguja wametinga wao moja kwa moja fainali.

“Saint Patrick Academy washatoa taarifa kama hawatoweza kufika Mbulu kesho katika mchezo wao wa nusu fainali dhidi ya Mjini kutokana na uhaba wa fedha, hivyo Mjini wameshafanikiwa kufika fainali moja kwa moja”.

Lakini inasemekana kuwa timu ya Saint Patrick Academy ya Arusha imewaogopa Mjini Unguja baada ya kutoa dozi nene hasa baada ya jana kuwachapa Lindi academy kwa mabao 5-1 huku magoli ya Mjini yalifungwa na Ibrahim Abdalla (Imu Mkoko ) 2, Mohamed Mussa (Modi) 2 na Mohamed Haji (X Box) 1, hivyo sababu ya kushindwa kumudu gharama ni kisingizio tu.

Kwa maamuzi hayo Mjini Unguja watasubiri kucheza fainali siku ya Jumanne ya July 18, 2017 na mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya JKU Academy kutoka Zanzibar au Fire Boys kutoka Karatu Arusha.

Mama Salma Kikwete awasisitiza wanamichezo pindipo wakihojiwa wajibu kwa kiswahili

$
0
0

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Mke wa Rais wa awamu ya nne nchini Tanzania Mama Salma Kikwete amehimiza Wachezaji wa soka nchini wanapohojiwa na waandishi wa habari ikiwa nje au ndani ya nchi wazungumze Kiswahili na kufanya hivyo ni kudumisha Utamaduni wa Tanzania na si kama mtu anaezungumza Kiswahili kitupu  hajaenda shule.

Mama Salma ambae ni Balozi wa Kiswahili katika bara la Afrika ameyasema hayo asubuhi ya leo katika hafla maalum ya uzinduzi wa Makavazi na Jumuiya ya Watetezi wa Kiswahili Tanzania (WAKITA) iliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) huko Vuga Mjini Zanzibar.

Mama Salma amesema tamko la Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Tanzania Dkt Harrison George Mwakyembe la kuwataka wachezaji wanapohojiwa wajibu kwa Kiswahili yeye amefurahi sana kwani huo ni uzalendo na njia moja ya kukuza Kiswahili.

“Nakumbuka hata juzi tu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo DK Harrison Mwakyembe alitoa tamko muhimu wakati anawapokea wachezaji wa timu ya Taifa wa mpira wa miguu, aliwataka wachezaji wote wanapohojiwa na Waandishi wa Habari wa ndani na nje ya nchi wawe wanajibu kwa lugha ya Kiswahili, tamko hili mimi nimelifurahia kwa kuwa limeweza kukuza na kuitangaza lugha yetu ya Kiwahili ndani na nje ya nchi”. Alisema Mama Salma.

Mwanzoni mwa mwezi huu wa July, 2017 kuliibuka mjadala kwa baadhi ya wapenzi wa soka nchini Tanzania baada ya Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania Elias Maguli kujibu kwa Kiswahili alipoulizwa swali kwa Kiengera na kituo kimoja cha TV huko Afrika ya Kusini baada ya kuibuka kuwa nyota wa mchezo kufuatia kufunga bao katika dakika ya 18 ya mchezo ambapo Stars waliichapa Afrika Kusini bao 1-0 katika Mashindano ya COSAFA CUP.

“Ahsante sana namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuaajilia kuweza kupata ushindi katika mchezo huu. Ulikuwa mchezo muhimu sana ila tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia kuweza kutoka na ushindi nawashukuru mashabiki waliojitokeza na kuweza kutushangilia na kutupatia nguvu”. Alisema Elius Maguli ambaye alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo.

Uzinduzi wa Tamasha la kushajiisha Elimu ya Mafunzo ya Sayansi, Teknolojia na Uhandisi wa Hesabu {STEM}

$
0
0
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akionyesha umahiri wake wa kucheza ngoma ya Ndege wakati akizindua Tamasha la kushajiisha Elimu ya Mafunzo ya Sayansi, Teknolojia na Uhandisi wa Hesabu {STEM} kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed  Shein hapo Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni.
 Balozi Seif akizindua Tamasha la kushajiisha Elimu ya Mafunzo ya Sayansi, Teknolojia na Uhandisi wa Hesabu {STEM} kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed  Shein.

 Baadhi ya wageni na walikwa kutoka Chuo Kikuu cha cha George Mason cha Nchini Marekani wakishuhudia  uzinduzi wa Tamasha la kushajiisha Elimu ya Mafunzo ya Sayansi, Teknolojia na Uhandisi wa Hesabu { STEM}.
 Balozi Seif akisalimiana na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Zanzibar Profesa Mshimba nje ya Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi wakati wa mwanzo wa mafunzo ya Sayansi, Teknolojia na Uhandisi wa Hesabu { STEM.

Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Walimu wa Hesabu Tanzania  Mwalimu Said Sima.
Mkuu wa Timu ya Wakufunzi kutoka Chuo Kikuu cha George Mason Nchini Marekani Profesa Padu kati kati akimpatia maelezo Balozi Seif  juu ya ufundishaji wa masomo ya Sayansi, Teknolojia na Hesabu kwa wanafunzi wa Fani hiyo.

Nyuma ya Profesa Padu ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uwezeshaji kwa wote Zanzibar { JUZA }iliyoandaa Mafunzo hayo ya STEM  Bibi Giftness Castico.

Picha na – OMPR – ZNZ

Na Othman Khamis. OMPR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein alisema ni dhahiri kwamba Maendeleo ya Nchi au Taifa lolote Duniani yanategemea juhudi zinazochukuliwa na Taifa hilo katika kukuza na kuendeleza  Sayansi na Teknolojia.

Alisema fani hizo mbili ndio msingi imara katika kuwapata wahandisi waliobobea kwenye nyanja mbali mbali huku ikifahamika kwamba msingi wa mambo  yote hayo kwa kiasi kikubwa unatokana na uweledi wa Taaluma ya Hesabu kama wataalamu walivyokubaliana kwamba Hesabu ni Mama wa Sayansi.

Dr. Shein alieleza hayo wakati akizindua Tamasha la kushajiisha Elimu ya Mafunzo ya Sayansi, Teknolojia na Uhandisi wa Hesabu { STEM} katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi uliopo Kikwajuni Mjini Zanzibar.

Rais wa Zanzibar alisema Taifa lazima liwe na wataalamu wake wenyewe  katika sekta mbali mbali pamoja na Teknolojia ya kisasa katika utekelezaji wa mipango ya Maendeleo iliyoandaliwa na Serikali katika sekta zote za Kiuchumi na Kijamii.

Alisema Serikali inahitaji Sayansi na Teknolojia katika kuendeleza sekya ya Kilimo, Afya miundombinu ya Bara bara  pamoja na utekelezaji wa Mipango Miji iliyokwishaanzishwa.
Dr. Shein alieleza wazi kwamba mpango huo wa STEM unahitaji kuendelezwa kwa nguvu zote ili Taifa liweze kujitegemea kwa kuwa na Wataalamu Wazalendo  katika fani tofauti na hatimae iweze kujiendesha na kusimamia mambo yake yenyewe.

Alisema kwa kutambua umuhimu wa Sayansi na Teknolojia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea na juhudi za kuimarisha ufundishaji wa masomo hayo kuanzia elimu ya Msingi, Sekondari hadi Vyuo Vikuu huku ikiimarisha vyuo vya Ufundi kwa kujenga Vituo vipya vya Mfunzo ya Amali pamoja na kuviimarisha vilivyopo hivi sasa.

Alifahamisha kwamba Serikali Kuu tayari imeanza  ujenzi wa chuo kipya cha Amali kiliopo Mtambwe  Kisiwani Pemba na Makunduchi Kisiwani Unguja ili kuwawezesha Vijana wa Maeneo hayo kupata elimu ya Ufundi wa kazi mbali mbali  na hatimae waweze kujiajiri watakapomaliza mafunzo yao.

Rais wa Zanzibar alielezea matumaini yake kwamba  Vijana wengi Nchini watahamasika, kuupokea  na kuuendeleza vizuri mpango huo wa kushajiisha Elimu ya Mafunzo ya Sayansi, Teknolojia na Uhandisi ya Hesabu  { STEM} katika ngazi zote za Elimu kama wanavyofanya Vijana wengine katika Mataifa mbali mbali Duniani.

Dr. Shein aliwashauri wasimamizi wa mpango huo  kuwatumia Wataalamu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania { COSTECH} ambao wamekubali kushirikiana nao kwa vile watendaji wa Tume hiyo ni mahiri na makikni waliobobea.

Alieleza kwamba lengo la kwenda sambamba na kasi pamoja na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia, ni lazima jamii yote ikubali kushirikiana ili kuhakikisha kwamba Vijana wanapenda kusoma na kuchagua mafunzo yanayohusiana na Taaluma hiyo ya Sayansi, Teknolojia na uhandisi wa Hesabu.

Dr. Shein amewahimiza Vijana wa Kike waendelee kuongeza bidii ili waweze kujijengea sifa waliyoidhihirisha  katika matokeo yao ya Mitihani wakati wa   kufaulu vyema mafunzo yao ya sekondari na vyuo mbali mbali yanayoendelea kushuhudiwa hapa Nchini.

“ Nawahimiza na kuwatia moyo Wanafunzi Wanawake waupokee vizuri mpango huu wa STEM kutokana na uwezo wao mkubwa wa kujifunza masomo ya Sayansi na Hesabu unaowapa fursa ya kuchukuwa zawadi za Wanafunzi bora wa masomo hayo ”. Alisema Dr. Shein.

Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alitanabahisha Vijana wote Nchini umuhimu wa kutambua kwamba wasipoongeza kasi ya kujifunza mafunzo ya Sayansi na Teknolojia wanaweza kujikuta wameachwa nyuma na Vijana wenzao Duniani.

Alisema ni vyema wakazingatia  kwamba Maendeleo ya haraka yaliyopatikana katika miaka ya hivi karibuni katika baadhi ya Mataifa machanga kama China na India ni matokeo ya juhudi zao katika kushajiisha masomo na mafunzo ya Sayansi na Teknolojiapamoja naUhandisi na Hesabu.

Dr. Shein alifafanua wazi kuwa Mataifa hayo yaliyopiga hatua kubwa ya kiuchumi kwa kiasi kikubwa  yameacha kuwategemea Wataalamu kutoka Nje ya Nchi zao na tayari yamejipanga  vizuri katika kuendeleza rasilmali zao wenyewe bila ya kuyategemea Mataifa mengine.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliipongeza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar  pamoja na Jumuiya ya Uwezeshaji kwa wote Zanzibar { JUZA } kwa juhudi walizochukuwa za kushirikiana na wadau wengine  katika kufanikisha  Tamasha hilo.

Dr. Ali Mohamed Shein kuunga mkono Mpango huo wa STEM amekubali kulipokea ombi lao la kuwawezesha kuanzisha  Kituo muhimu na Maalum  kwa Vijana katika kutoa  Elimu, kushajiisha na kuendeleza Mpango wa STEM              {  STEM  STOP  CENTER – SSC } ili ifahamike na kutumika ipasavyo.

Mapema Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uwezeshaji kwa wote Zanzibar  { JUZA } Bibi Giftness Castico alisema Jumuiya hiyo ikipata kuungwa mkono kiuwezeshaji ina uwezo na Taaluma ya kutosha ya kutoa mafunzo ya Sayansi, Teknolojia na Hesabu Maskulini Unguja na Pemba.

Bibi Giftness alisema licha ya JUZA kujipanga kufanya Tamasha kila Mwaka lakini mipango ya awali tokea kuanzishwa kwake mwaka 2017 yalielekezwa katika mapambano dhidi ya udhalilishaji wa Kijinsia.

Alisema mpango huo ulioungwa mkono na Wananchi na Taasisi mbali mbali ndani na nje ya Nchi umeleta mafanikio makubwa na Ripoti ya mpango wa Jumuiya hiyo utaufikishwa Serikalini kwa kuchukuliwa hatua zitakazostahiki.

Mwenyekiti huyo wa Jumuiya ya Uwezeshaji kwa wote Zanzibar  { JUZA } alifahamisha kwamba lengo la mafunzo hayo litapangwa na kuelekezwa kwa wanafunzi wa skuli za Msingi, Sekondari hadi Vyuo Vikuu.

Akitoa salamu za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar katika uzinduzi huo wa  Tamasha la kushajiisha Elimu ya Mafunzo ya Sayansi, Teknolojia na Uhandisi wa Hesabu  Naibu Waziri wa Wizra hiyo Mh. Mmanga Mjengo Mjawiri aliahidi kwamba Wziara ya Elimu itaendelea kujenga msingi mzuri utakaowawezesha Vijana kupendelea na kuendelea kusoma masomo ya Sayansi, Teknolojia na Hesabu.

Mh. Mjawiri aliwaomba Wafadhili na Wadau wa Sekta ya Elimu ndani na nje ya Nchi kuendelea kuiunga mkono Wizara hiyo na tayari imeshikitita kushirikiana na wadau hao katika kusimamia masomo ya Sayansi ambayo hayasomeshwi kwa kubahatisha.

Alisema Walimu na wakufunzi wa masomo na mafunzo ya Sayansi, Teknolojia na Hesabu lazima wajengewe misingi imara itakayowapa mbinu na fursa za kusomesha Kitaalamu na kwa uhakika.

Naibu Waziri huyo wa Elimu na Mfunzo ya Amali aliwahakikishia Walimu wa Hesabu kwamba Wizra ya Elimu iko tayari kuwawezesha walimu wa Somo hilo kuunda Chama chao endapo watafikia hatua ya kufanya hivyo.

Timu mpya ya madaktari kutoka nchini China yaanza kutoa huduma vijijini

$
0
0
 Wananchi wa Shehia ya Banko wakisubiri huduma za matibabu kutoka kwa timu ya madaktari bingwa kutoka China waliofika katika skuli ya sekondari Chumbuni kutoa hudua hizo.
 Daktari bingwa wa macho kutoka china Qin Qin akimfanyia uchunguzi wa macho mtoto Nassor Idrisa katika zoezi la kutoa huduma vijiji lililofanyika skuli ya sekondari Chumbuni.

 Mzee Abdalla Bakari akielezea matatizo ya afya yake kwa Dkt. He Qibin kutoka China wakati timu ya madaktari hao ilipokua ikitoa huduma za afya katika Shehiya ya Banko skuli ya sekondari Chumbuni (kulia) Dkt. Zulekha Bakari akisaidia tafsiri.

Dkt. Zhou Ziyue kutoka China akimpima sindikizo la damu (Pressure) Mzee. Ali Simai Makame wakati wa zoezi la kuchunguza afya wananchi wa Shehia ya Banko katika skuli ya sekondari Chumbuni.

Picha na Makame Mshenga.

Wanafunzi skuli za sekondari Pemba wapatiwea mafunzo ya haki za binadamu

$
0
0
 WANAFUNZI wa Skuli mbali mbali za Sekondari kutoka Wilaya nne za kisiwani Pemba, wakifuatilia kwa makini mafunzo ya Haki za Binaadamu, yaliyotolewa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Tawi la Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
 MRATIB wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Tawi la Pemba, Fatma Khamis Hemed akiwasilisha mada ya haki za Watoto, kwa wanafunzi wa skuli za Sekondari Kisiwani Pemba, huko katika Ukumbi wa Kituo hicho
Mjini Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
 AFISA elimu ya Ukimwi kutoka Tume ya Ukimwi Zanzibar Tawi la Pemba, AFISA elimu ya Ukimwi kutoka Tume ya Ukimwi Zanzibar Tawi la Pemba, Ali Mbarouk Omar akiwasilisha mada ya athari za Madawa ya Kulevya kwa
wanafunzi wa skuli za Skondori Kisiwani Pemba, wakati wa mafunzo ya haki za Binaadamu yaliyoandaliwa na ZLSC.(PICHA NA ABDI SULEIMAN

AFISA Mipango kutoka Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Tawi la Pemba, Safia Saleh Sultani akiwasilisha mada ya sheria ya Ukimwi kwa wanafunzi wa skuli za sekondari Kisiwani Pemba, wakati wa mafunzo ya
haki za binaadamu huko katika kituo cha ZLSC.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).



BAADHI ya wanafunzi wakiwa katika kazi za vikundi, wakati wa mafunzo ya haki za binaadamu yaliyoandaliwa na kituo cha huduma za Sheria Zanzibar Tawi la Pemba Mjini Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN,
PEMBA).

Ligi Kuu Zanzibar kuanza kesho mzunguko wa 6

$
0
0

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Mzunguko wa 6 wa ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya 8 bora utaanza rasmi kesho Jumatatu ya July 17, 2017 kwa kupigwa mchezo mmoja kati ya Mwenge watacheza na Zimamoto katika uwanja wa Gombani saa10:00 za jioni.

Kesho kutwa Jumanne ya July 18, 2017 mechi nyengine 3 ambapo Okapi watasukumana na Taifa ya Jang’ombe katika uwanja wa Gombani saa 10:00 za jioni, na katika uwanja wa Amaan JKU watakipiga na Kizimbani saa 10:00 za jioni, kisha saa 1:00 za usiku Jang'ombe boys dhidi ya Jamhuri.

Ikumbukwe kuwa hatua hiyo ya 8 bora ni kwaajili ya kuwatafuta Wawakilishi wa Zanzibar watakaoshiriki Mashindano ya Kimataifa ambapo Bingwa atawakilisha kwenye Kombe la Klabu Bingwa Barani Afrika na mshindi wa pili atawakilisha kwenye Kombe la Shirikisho Barani humo ambapo msimu uliopita Zimamoto na KVZ waliwakilisha Zanzibar katika Mashindano hayo.

ADC Yapokea Wanachama 25 Wapya Kutoka Chama Cha TADEA Zanzibar.


ADC Yapokea Wanachama Wapya 25 Kutoka Chama cha ADA-TADEA Zanzibar.

$
0
0
Na Abdi Shamnah
Wanachama wa chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) wametakiwa kushirikiana na serikali zilizoko madarakani, ili kufanikisha azma ya kuwaletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii wananchi.
Changamoto hiyo imetolewa na mwanachama wa Chama hicho Mussa Jangwa Bohero katika hafla ya kupokea na kukabidhi kadi mpya kwa wanachama 25 wa chama cha TADEA waliojiunga na chama hicho, iliofanyika katika makao makuu ya ADC Bububu.

Miongoni mwa waliokihama chama hicho, wapo viongozi watatu ambao walishiriki katika kugombea nafasi za uongozi ngazi za tofauti, katika uchaguzi mkuu  wa 2015.

Akizungmza katika hafla hiyo, mwanachama huyo aliefika kwa madhumuni ya kushudia tukio hilo, alisema ni wajibu wa wanachama wa chama hicho kushirikiana kikamilifu na serikali zilioko madarakani, kwa kuelewa kuwa ndizo zenye jukumu la kuwahudumia wananchi na kuimarisha uchumi wa Taifa.

Alisema katika kufanikisha jambo hilo, wanachama wa ADC wana jukumu a kudumisha amani na utulivu uliopo nchini pamoja na kujenga mshikamano na wanachama wa vyama vyengine, ili kuleta ustawi wa Taifa.

‘‘ Tunapaswa kuhirikiana na serikali zilizoko madarakani, hizi ndio zenye dhima ya kuongaza Taifa hili hadi mwaka 2020, hivyo tuna wajibu wa kuzitii na kudumisha aman  iliopo’’, alisema.

Nae Issa Ame Issa, aliekuwa Katibu wa TADEA Mkoa wa Kusini Unguja, aliahidi kushirikiana an wanachama wa chama hicho (ADC) katika kuendeleza harakati za kukiimarisha chama hicho, ili kukiweka katika mazingira bora ya uchaguzi mkuu ujao .

Alisema yeye pamoja na wanachama wengine 25, wameamuwa kwa hiari yao kujiunga na ADC baada ya kuridhika na utendaji wake na kubaini kuwa ni chama chenye malengo ya kweli na sera zinazotekelezeka.

Mapema Naibu Katibu Mkuu wa ADC Zanzibar, Khamis Mohammed  Kombo alipokea kadi 25 za wanachama hao kutoka TADEA, sambamba na kukabidhi kadi mpya za ADC.

Miongoni mwa wanachama wapya wa ADC ambapo kabla walikuwa  Viongozi wa TADEA na kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu wa 2015 jimbo la Mtopepo ni pamoja na Hamad Rashid Kombo(Ubunge), Amana (Uwakilishi) pamoja na Khadija nafasi ya Udiwani.


Katika siku za hivi karibuni Chama cha TADEA kimekumbwa na jinamizi la kuondokewa na viongozi pamoja na wanachama wake na kujiunga na ADC, ambapo Julai, 4  mwaka huu, kundi kubwa lilikihama chama hicho. 

Rais wa Tanzania Dkt.John Magufuli Akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli Washiriki Ibada ya Jumapili Katika Parokia Bikira Maria Chato Mkoani Geita na Kuendesha Harambee ya Kuchangia Ujenzi wa Kanisa Hilo.

$
0
0
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli pamoja na mke wake Mama Janeth Magufuli wakitoa sadaka wakati wa ibada ya jumapili katika kanisa la Katolikila  Bikira Maria Parokia ya Chato Mkoani Geita.Leo 16 julai 2017
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli wakisikiliza mahubiri kutoka kwa Padri  Henry Mulinganisa wakati wa ibada ya jumapili katika kanisa la Katoliki la  Bikira Maria Parokia ya Chato Mkoani Geita.Leo
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisisitiza jambo wakati wa ibada ya jumapili katika kanisa la Katoliki la  Bikira Maria Parokia ya Chato Mkoani Geita
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisisitiza jambo wakati wa ibada ya jumapili katika kanisa la Katoliki la  Bikira Maria Parokia ya Chato Mkoani Geita
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli aliyeshika kikapu cha sadaka akipokea sadaka kutoka kwa Mke wake Bi Janeth Magufuli wakati wa kuchangia ujenzi na upanuzi wa katika kanisa la Katoliki la  Bikira Maria Parokia ya Chato Mkoani Geita.Leo
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli aliyeshika kikapu cha sadaka akipokea sadaka kutoka kwa waumini mbali mbali waliohudhuria ibada katika kanisa la Katoliki la  Bikira Maria Parokia ya Chato Mkoani Geita Leo.
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa ameshika kikapu chenye michango ya fedha zilizotolewa na waumini wa kanisa Katoliki la  Bikira Maria Parokia ya Chato Mkoani Geita kwa ajili ya ujenzi na upanuzi wa kanisa hilo.Leo
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimshukuru mmoja wa waumini wa kanisa hilo ndugu Mwita Chacha mara baada ya kuchangia mifuko mitano ya saruji kwa ajili ya ujenzi na upanuzi wa kanisa Katoliki la  Bikira Maria Parokia ya Chato Mkoani Geita 


Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiondoka kwenye kanisa Katoliki la  Bikira Maria Parokia ya Chato Mkoani Geita, mara baada ya ibada.





Wanawake Wanye Ulemavu Pemba Wapata Mafunzo ya Elimu ya Haki za Binaadamu.

$
0
0
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Wenye Ulemavu Zanzibar,Bi.Salma Haji Saadati akizungumza na wanawake wenye Ulemavu Kisiwani Pemba, katika mafunzo ya siku mbili kwa wanawake hao huko katika ukumbi wa madungu maandalizi Chake Chake Pemba

Wabawake wa Jumuiya  Watu Wenye Ulemavu  Kisiwani Pemba wakifuatilia semina ya mafunzo ya haki za binadamu, huko katika skuli ya madungu maandalizi Chake Chake Pemba.
(PICHA NA HABIBA
ZARALI, PEMBA)

Serikali Kuendelea Kuboresha Mazingira ya Kuabudu Nchini

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora  Angela Kairuki akihutubia kwenye mkutano wa kitaifa wa shukrani na kumuombea Rais Dk.John Magufuli pamoja na nchi uliofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam jana.
 Kwaya ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kijitonyama ikitoa burudani ya nyimbo za kumsifu mungu katika mkutano huo.
 Burudani ya kwaya ikiendelea.
 Kikundi cha Utoaji Hamasa  kikiwa kazini uwanjani hapo.
 Mwonekano katika majukwaa.

 Maandamano yakipita mbele ya mgeni rasmi Angela Kairuki.

 Maandamano yakiendelea.
 Mjumbe wa Kamati ya maandalizi ya mkutano huo, Jane Magigita akimwelekeza jambo mgeni rasmi wa mkutano huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora  Angela Kairuki baada ya kuwasili kwenye mkutano huo.
 Baadhi ya maaskofu na wachungaji wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.
 Mratibu wa maombi hayo ambaye ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Abudant Blessing Center (ABC), Askofu Flaston Ndabila akisalimiana na mgeni rasmi.
 Mgeni rasmi Angela Kairuki akisaini baada ya kufika katika mkutano huo.
 Wananchi wakiwa jukwaani wakati wa mkutano huo.
 Mtumishi wa mungu muhubiri wa kimataifa mtanzania anayeishi Marekani, Dk. Nicku Kyungu 'Mama Afrika' (katikati), akiwa meza kuu na mgeni rasmi, Angela Kairuki (kulia). Kushoto ni Mratibu wa maombi hayo ambaye ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Abudant Blessing Center (ABC), Askofu Flaston Ndabila
 Jukwaani.
 Wanafunzi kutoka Shule maalumu ya Jeshi la Wokovu wakiimba katika mkutano huo.
 Mtumishi wa mungu muhubiri wa kimataifa mtanzania anayeishi Marekani, Dk. Nicku Kyungu 'Mama Afrika' akizungumza kwenye mkutano huo.
 Maaskofu wakimsindikiza mgeni rasmi Angela Kairuki kuelekea jukwaa lililoandaliwa kwa maombi na kuhutubia.
 Maombi yakifanyika.
 Askofu Bernard Nwaka kutoka nchini Zambia akimuombea Rais Dk.Joh Magufuli.
 Mtumishi wa mungu Askofu kutoka Marekani akiomba.
 Askofu Timoth Joseph kutoka Nigeria akiombea nchi.
 Askofu Sylvester Gamanywa akiomba.
 Maombi ya kuombea vyombo vya usalama na ulinzi yakifanyika.
 Maombi yakiendelea.
 Askofu kutoka Afrika Kusini akiombea nchi.
 Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya maombi hayo, Askofu Mkuu wa Naoith Pentekoste Church, Dk.David Mwasota akiombea nchi kuhusu uchumi.
 Mtumishi wa mungu muhubiri wa kimataifa mtanzania anayeishi Marekani, Dk. Nicku Kyungu 'Mama Afrika' akiteta jambo na Waziri Angela Kairuki.

 Mwakilishi wa Askofu Dk. Alex Malasusa wa Kanisa la Kinjili la Kilutheri Tanzania , Mchungaji Andrew King akizungumza kwenye mkutano huo.

Maaskofu Wakuu wakiwa jukwaani katika mkutano huo.
 Maombi ya kuombea nchi yakiendelea.



 Kwaya ikitoa burudani.
Mratibu wa maombi hayo ambaye ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Abudant Blessing Center (ABC), Askofu Flaston Ndabila akihitima maombi hayo kwa kutoa neno la shukrani.

Na Dotto Mwaibale

SERIKALI itaendelea kuboresha mazingira bora na wezeshi ili kila mtanzania apate uhuru wa kuabudu kupitia dini yake na hata kwa yule ambaye hana dini.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora , Angela Kairuki wakati akihutubia kwenye maaombi maalumu ya kitaifa ya kuombea nchi na Rais Dk.John Magufuli yaliyofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam jana ambapo alikuwa mgeni rasmi.

"Serikali licha ya kuwa haina dini itaendelea kuboresha mazingira ya kuabudu ili kila mwananchi apate fursa ya kuabudu bila ya bugudha yoyote" alisema Kairuki.

Alisema viongozi wa dini kuptia taasisi zao wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kuiletea nchi maendeleo na amani ambayo imedumu tangu tupate uhuru hivyo wanapaswa kupongezwa.

Kairuki alisema serikali ina thamini maombi yanayofanywa na viongozi wa dini hapa nchini kwani yanaleta amani, umoja na uzalendo na si kwa waumini wa dini pekee bali na kwa watu wote wenye mapenzi na nchi yetu.

Waziri Kairuki alisema ni vizuri tukatumia fursa hii ya amani iliyopo nchini kwa kila mtu kufanya kazi kwa bidii kama Rais Dk.John Magufuli anavyohimiza kila siku ikiwa pamoja na kumuombea.

Mtumishi wa mungu muhubiri wa kimataifa mtanzania anayeishi Marekani, Dk. Nicku Kyungu 'Mama Afrika' ambaye alipata maono ya kufanya mkutano huo wa maombi ya shukrani hapa nchini alisema Afrika pamoja na Tanzania zimebarikiwa kwa kuwa na rasilimali za kutosha tulizopewa na mungu hivyo hatuna budi kumshukuru mungu.

Alisema Tanzania imejaa kila kitu kizuri, mbuga za wanyama, madini, ardhi ikiwemo amani iliyodumu tangu utawala wa Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na sasa Dk. John Magufuli.

Alisema kutokana na neema hiyo kutoka kwa mungu aliona ni vema yakafanyika maombi ya shukrani ya kitaifa na kumuombea Rais Dk.John Magufuli na nchi kwa ujumla.

Dk.Kyungu alisema kauli alioianzisha Rais Dk. Magufuli ya Hapa Kazi tu ipo katika biblia hivyo ni wajibu wa kila mtu kufanya kazi kama mungu alivyomuagiza adamu pale bustani ya hedeni na hiyo itasaidia kupambana na adui umaskini, ujinga na maradhi hasa katika kipindi hiki ambacho Rais Dk. John Magufuli anahimiza nchi kuingia katika uchumi wa viwanda.


Katika maombi hayo maaskofu wakuu zaidi ya kumi kutoka ndani na nje ya Tanzania waliweza kuiombea nchi katika maeneo mbalimbali, kama uchumi, vyama vya siasa na viongozi wao, Rais na Serikali, Bunge, amani, masuala ya ulinzi na usalama na mambo mengine.

Maombi hayo ambayo ni ya kihistoria hapa nchini yaliandaliwa na  viongozi wa dini kutoka madhehebu ya Huduma ya Kikristo Tanzania na Taasisi ya I Go Africa For Jesus yalifanyika kuanzia saa nne asubuhi hadi jioni na kuhudhuriwa na mamia ya watanzania na viongozi wa dini huku yakipambwa na burudani za nyimbo za kumtukuza mungu kutoka kwaya mbalimbali ambapo yalifungwa na neno la shukrani na Mratibu wa maombi hayo ambaye ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Abudant Blessing Center (ABC), Askofu Flaston Ndabila.

Baadhi ya maaskofu wakuu waliohudhuria maombi hayo ni pamoja na Dk. Philemon Tibananason, Dk.Bernard Nwaka kutoka Zambia, Sylvester Gamanywa, Lawrence Kameta, Dk.Barnabas Mtokambali, Timoth Joseph kutoka Nigeria na wengine kutoka nje ya nchi.

Kesho Rasmin Dirisha la Usajili Zanzibar Linafunguliwa.

$
0
0
Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Dirisha la Usajili rasmi linafunguliwa kesho ambapo Makocha na Viongozi wengine wa Vilabu wanakuwa bize kutafuta wachezaji wanaowahitaji ili kuziboresha timu zao katika msimu mpya wa mwaka 2017-2018.
Hivi karibuni Chama cha Soka Visiwani Zanzibar “ZFA” kilitangaza rasmi tarehe ya kuanza zoezi la uhamisho na usajili kwa msimu wa mwaka 2017-2018 ambao unatarajiwa kuanza kesho July 17, 2017 na kumaliza Agost 17, 2017.
Tayari ZFA imepata timu 12 zitakazoshiriki ligi kuu soka ya kwa msimu wa mwaka 2017-2018 ambapo wameamua timu zilizomaliza nafasi ya 1-6 kwa kila kanda, yani Unguja na Pemba ndizo zitakazocheza ligi kuu wakati huo huo Bingwa atapata nafasi ya kuwakilisha Zanzibar katika Kombe la Klabu Bingwa Barani Afrika.

Timu 16 kati ya 28 zilizosalia ambazo hazijashuka daraja zitacheza ligi two ambapo Bingwa wa ligi hiyo atapata nafasi ya kuwakilisha Zanzibar kwenye kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Timu hizo 12 zilizofanikiwa kucheza ligi kuu msimu mpya wa mwaka 2017-2018 ni JKU, Jang’ombe Boys, Zimamoto, Taifa ya Jang’ombe, Polisi, KMKM kwa upande wa Unguja na Pemba ni Jamhuri, Kizimbani, Mwenge, Okapi, Chipukizi na New Stars.

Kwa upande wa timu 16 zitakazocheza ligi 2 msimu mpya wa mwaka 2017-2018 kati ya hizo 8 za Unguja na 8 za Pemba ambapo za Unguja ni Mafunzo, KVZ, Black Sailors, Chuoni, Kilimani City, Kipanga, Miembeni City na Charawe wakati za Pemba ni Dogomoro, Wawi Star, Shaba, Young Islander, FSC, Hardrock, Chuo Basra na Opek.

Timu 4 za mwisho za ligi 1 zitashuka darajan la ligi 2, na timu 4 za juu za ligi 2 zitapanda daraja la ligi 1.
Attachments area
Viewing all 35978 articles
Browse latest View live