Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all 36204 articles
Browse latest View live

Msanii wa Muziki Nchini Tanzania Babu Seya Atowa Shukrani Kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli Ikulu Kwa Kuwapa Msamaha.

$
0
0
Mwanamuziki Nguza Viking "Babu Seya" na wanae Johnson Nguza "Papii Kocha', Francis Nguza na Nguza Mbangu walipowasili Ikulu jijini Dar es salaam leo January 2, 2018 kumshukuru Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwapa msamaha wa kifungo cha maisha Babu Seya na mwanae Papii Kocha walichokuwa wanatumikia toka wahukumiwe miaka 13 iliyopita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe  akiongea na   Viking "Babu Seya" na  Johnson Nguza "Papii Kocha', Francis Nguza na Nguza Mbangu walipokwenda Ikulu jijini Dar es salaam leo January 2, 2018 kumshukuru kwa kuwapa msamaha wa kifungo cha maisha Babu Seya na mwanae Papii Kocha walichokuwa wanatumikia toka wahukumiwe miaka 13 iliyopita.



Mchezo wa Kombe la Mapinduzi Kati ya Simba na Mwenge Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu Hizo Zimetoka Sare ya Bao 1 -1.

$
0
0
 Mchezaji wa Timu ya Simba akijaribu kumpita beki wa Timu ya Mwenge wakati wa mchezo wao wa Kombe la Mapinduzi uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1. usiku huu michuano hiyo inaendelea kwa kuzikutanisha Timu ya Yanga na Mlandege











Waziri Castico azindua mradi wa maji safi na salama katika maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi Kifundi, Micheweni Pemba

$
0
0
 Waziri wa kazi , Uwezeshaji , Wazee, Vijana , Wanawake na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Maudline Cyrus Castico, akifunguwa mradi wa maji safi na salama , ikiwa ni miongoni mwa madhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar., huko Kifundi Wilaya ya Micheweni Pemba.
 Waziri wa Kazi, Uwezeshaji , Wazee , Vijana , Wanawake na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar , Maudline Cyrus Castico, akiwasha Switch ya Umeme kuashiria mradi uko tayari kwa kuanza matumizi ya maji safi na Salama katika mradi wa maji safi na Salama huko Kifundi Wilaya ya Micheweni 
 Waziri wa Kazi, Uwezeshaji , Wazee , Vijana , Wanawake na watoto wa Serikali ya Mapindduzi Zanzibar , Maudline Cyrus Castico, akizungumza na Wananchi na Viongozi mbali mbali waliohudhuria katika sherehe hiyo ya ufunguwaji wa mradi wa maji safi na salama ikiwa ni miongoni mwa madhimisho ya sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi Zanzibar.

Baadhi ya Wananchi wa Kifundi, Wilaya ya Micherweni wakimsikiliza  Waziri wa Kazi, Uwezeshaji , Wazee , Vijana , Wanawake na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar , Maudline Cyrus Castico, alipokuwa akizungumza nao

PICHA NA MASANJA MABULA-PEMBA.

Waziri Amina aweka jiwe la msingi skuli ya Michenzani Wilaya ya Mkoani ikiwa ni shamrashamra za miaka 54 ya Mapinduzi

$
0
0
WAZIRI wa Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar, Balozi Amina Salum Ali akisalimiana na Ofisa Mdhamini Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Pemba, Ali Salum Ali Mata mara baada ya kuwasili katika skuli ya Michenzani Wilaya ya Mkoani, kwa lengo la kuweka jiwe la msingi katika skuli hiyo.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).

 WAZIRI wa Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar, Balozi Amina Salum Ali, akikunjuwa kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi, banda la vyumba vinne vya skuli ya Msingi michenzani Wilaya ya Mkoani, kushoto ni Naibu katibu mkuu Wizara ya Elimu na na Mafunzo ya Amali Zanzibar Abdalla Mzee Abdalla, ikiwa ni shamrashamra za miaka 54 ya Mapinduzi.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
 WANAFUNZI wa Skuli ya Sekondari na Msingi Michenzani Wilaya ya Mkoani, wakimsikiliza kwa makini hutuba ya waziri wa biashara Viwanda na masoko Zanzibar Balozi Amina Salum Ali, wakati alipokuwa akizungumza nao baada ya uwekaji wa jiwe la msingi katika skuli hiyo.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
VIONGOZI mbali mbali wa Serikali wakiangalia ngoma ya Nkota Ngoma ya mkoani, wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la skuli ya msingi Michenzani Wilaya ya Micheweni, ikiwa ni shamra shamra za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
 KATIBU Tawala Wilaya ya Mkoani Miza Hassan Faki, akisoma utaratibu wa shuhuli ya uwekaji wa jiwe la Msingi katika skuli ya Micheweni, ikiwa ni shamrashamra za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
 WANAFUNZI wa Skuli ya Sekondari Michezani Wilaya ya Mkoani, wakiimba wimbo wa mashujaa :SISI SOTE TUMEGOMBA” mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la skuli ya msingi michenzani, ikiwa ni shamrashamra za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
NAIBU katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Abdalla Mzee Abdalla, akisoma taarifa ya kitaalamu ya ujenzi wa banda moja lenye vyumba vine vya kusomea wananfunzi wa msingi Michenzani Wilaya ya Mkoani, ikiwa ni shamrashamra za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
WAZIRI wa Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar Mhe:Balozi Amina Salum Ali, akizungumza na wazazi, walezi, walimu na wanafunzi wa skuli ya Msingi na Sekondari Michenzani Wilaya ya Mkoani, ikiwa ni shamrashamra za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).

Mapokezi ya Mwenyekiti wa UVCCM Ndg. Kheri Mkoani Mwanza.

$
0
0
Mjumbe wa Kamati kuu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kheri D James kulia akisalimiana na Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Ndg:Anthony Dialo mara baada ya kuwasili katika ofisi za Ccm Mkoa wa Mwanza.
Mjumbe wa Kamati kuu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kheri D James akiteta jambo na Mwenyekiti wa Ccm mkoa wa mwanza Dr. Anthony dialo.
Kaimu katibu mkuu wa Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi Shaka Hamdu Shaka akizungumza na Wanachama wa CCM Mkoa mwanza katika Ofisi za CCM Mkoa wa Mwanza.
Mjumbe wa Kamati kuu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kheri D James akizungumza na wanachama wa chama cha mapinduzi mkoa wa mwanza akielekea Uwasha wa CCM KIRUMBA.
 Mjumbe wa Kamati kuu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kheri D James akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Ilemela na Naibu waziri wizara ya Ardhi Dkt Angelina Mabula alipowasili katika mapokezi  Uwanja wa CCM Kirumba
 Mjumbe wa Kamati kuu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kheri D James akisalimia na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ilemela
Mjumbe wa Kamati kuu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kheri D James akiwasalimia na wanachama wa chama cha mapinduzi na jumuiya zake Uwanja wa Ccm kirumba.
wanachama wa Ccm Wakipugia mikono
 Mjumbe wa Kamati kuu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kheri D James akivikwa skafu mara baada ya kuwasili Uwanja wa CCM Kirumba
 zoezi likiendelea
 Mjumbe wa Kamati kuu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kheri D James akiwasalimia Wanachama wa CCM na Jumuiya zake waliohudhulia katika  uwanja wa CCM Kirumba
 
 vijana wa CCM wakionyesha ukomavu wao
Sehemu ya Viongozi

 kikundi cha ngoma toka bujoro kikitumbuiza
 Mwanachama wa CCM Akiwa amebebelea kipeperushi kwa uso wa furaha
 Sehemu ya madiwani na viongozi wilaya ya ilemela
 Viongozi meza kuu wakifuatilia mkutano
Katibu wa CCM Mkoa wa mwanza Ndg:raymond akizungumza katika mkutano
 Mama mzazi wa Mjumbe wa Kamati kuu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kheri D James akitoa shukrani kwa wana CCM .
 Mbunge wa jimbo la Ilemela na naibu waziri wa Ardhi Dkt Angelina Mabula akizungumza katika mkutano wa kumpongeza kwa ushindi na kumkaribisha Mjumbe wa Kamati kuu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kheri D James
 Mjumbe wa Kamati kuu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kheri D James akipokea taarifa za pongezi kwa wazee wa kata ya kirumbo
 Mkuu wa mkoa wa mwanza John mongela akizungumza
 wazee wa mkoa wa mwanza wakimsimika Utemi Mjumbe wa Kamati kuu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kheri D James
 Mjumbe wa Kamati kuu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kheri D James akinyanyua silaa juu mara baada ya kusimikwa.(PICHA NA FAHADI SIRAJI)


Makamu mwenyekiti wa UVCCM akizungumza.
 Kaimu katibu mkuu wa Umoja wa vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka akizungumza na viongozi pamoja na Wanachama wa CCM na Jumuiya zake mkoa wa Mwanza wakati akimkaribisha Mjumbe wa Kamati kuu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kheri D James kuzungumza.(PICHA NA FAHADI SIRAJI)
 Mjumbe wa Kamati kuu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kheri D James akizungumza na Viongozi pamoja na wanachama wa CCM na jumuiya zake mkoa wa mwanza (PICHA NA FAHADI SIRAJI)
wanachama wakifurahia hotuba ya Mjumbe wa Kamati kuu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kheri D James(PICHA NA FAHADI SIRAJI)





Zawadi ya vijana kata ya Kirumba (Picha na Fahadi Siraji)

Mhe.Mwanjelwa : Maendeleo Hayana Mipaka ya Vyama.

$
0
0
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akishiriki ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari Iyera wakati akiwa ziarani Mkoani Mbeya, Jana 2 Januari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikabidhi mifuko 20 ya saruji kwa ajili ya kuongeza nguvu katika ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya Sekondari Iyera wakati akiwa ziarani Mkoani Mbeya, Jana 2 Januari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akichanganya udongo wakati akishiriki ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari Iyera wakati akiwa ziarani Mkoani Mbeya, Jana 2 Januari 2018. Wengine (Kulia) aliyeshika jembe ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe Paul Ntinika na Kushoto ni Diwani wa Kata ya Iyera (CHADEMA) Mhe Charles Mkera
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akipanga mawe kwenye msingi wa darasa ishara ya mafundi kuanza haraka ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari Iyera wakati akiwa ziarani Mkoani Mbeya, Jana 2 Januari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akimpongeza Diwani wa Kata ya Iyera (CHADEMA) Mhe Charles Mkera kwa kushirikiana na serikali na kuhamasisha wananchi katika ushiriki wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari Iyera wakati akiwa ziarani Mkoani Mbeya, Jana 2 Januari 2018.

Na Mathias Canal, Mbeya
Maendeleo ni mchakato wa kujenga jamii endelevu, yenye kujiamini,  kujituma na uwezo wa kushiriki, kwa misingi ya usawa na kuheshimiana, katika kubuni, kuandaa na kutekeleza mipango ya kujiletea “maendeleo” na kutumia matokeo ya kazi zao.

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa amekuwa mwalimu mzuri wa somo la Uraia Mkoani Mbeya akifundisha kuhusu umoja na mshikamano huku akisisitiza kuwa Maendeleo ni dhana pana kwa wananchi na hayapaswi kufanywa kwa mipaka ya vyama vya siasa.

Mhe Mwanjelwa ameyasema hayo Jana 2 Januari 2018 wakati akizungumza na wananchi na mafundi wanaojenga majengo ya Shule ya Sekondari Iyera ili kutatua changamoto ya kuwa na vyumba vingi vya madarasa kwa ajili ya kuhimili wingi wa wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu.

Amewasisitiza mafundi hao kujenga madarasa hayo kwa haraka na viwango vya hali ya juu kwani shule zinatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni huku shule hiyo ikiwa na upungufu wa vyumba vinne vya madarasa.

Mhe Mwanjelwa alisema kuwa tangu serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kutangaza utoaji elimu bure kuanzia ngazi ya shule ya msingi hadi sekondari kumekuwa na ongezeko kubwa la wananfunzi wanaojiunga na masomo ikiwa ni pamoja na kurejea shuleni kwa wananafunzi waliokata tamaa ya kuendelea na masomo.

Alisifu juhudi za Uongozi wa Wilaya ya Mbeya kwa kushirikiana kwa pamoja na wananchi katika shughuli za maendeleo huku akiipongeza Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa kufanya vyema na hatimaye kuongoza kwa ufaulu wa wanafunzi dhidi ya Halmashauri zingine za Mkoa wa Mbeya.

Sambamba na hayo pia Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa ameongeza nguvu kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule hiyo ya Sekondari Iyera kwa kuchangia mifuko 20 ya saruji.

Yanga African Yaibuka na Ushindi Kombe la Mapinduzi Yaifunga Timu ya Mlandege 2-1 Mchezo Uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar.

$
0
0
Kikosi cha Timu ya Yanga African kilichotoka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Timu ya Mlandege katika mchezo wake wa kwanza wa Michuani ya Kombe la Mapinduzi uliofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar. Bao la kwanza la Yanga limefungwa katika dakika ya 7na 36 ya mchezo huo kipindi cha kwanza kupitia mshambuliaji wake Juma Mahadhi. Bao la kufutia machozi la Timu ya Mlandege limefungwa na mshambuliaji wake Omar Makamekatika kipindi cha pili cha mchezo huo katika dakika ya 48. Hadi mwisho wa mchezo huo timu ya Yanga African imetoka kifua mbele kwa ushindi wa bao 2-1.   
Kikosi cha Timu ya Mlandege wakisoma dua kabla ya kuazi kwa mchezo wao wa Kombe la Mapinduzi na Timu ya Yanga African mchezo uliofanyika jana usiku,2/1/2018. katika Uwanja wa Amaan Zanzibar. 



Mshambuliaji wa Timu Yanga Juma Mahadhi akishangilia bao lake la Pili alililofunga katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo wa Michuano ya Kombe la Mapinduzi mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar.






Wachezaji wa Timu ya Mlandege wakishangilia bao lao la kwanza lililofunguwa na mshambuliaji Omar Makame katika dakika ya 48 ya mchezo huo kipindi cha pili. 
Wachezaji wa Timu ya Mlandege wakishangilia bao lao la kwanza lililofunguwa na mshambuliaji Omar Makame katika dakika ya 48 ya mchezo huo kipindi cha pili. 


Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Latoa Onyo Kali Kuhusu Ununuzi wa Vifaa Vya Zimamoto.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,Azindua Sherehe za Miaka 54 ya Mapinduzi Kwa Shughuli za Usafi Nyumba za Wazee Sebleni Zanzibar

Uzinguzi wa Mashine ya Maji Kijiji cha Ngomeni Pemba Shamrashamra za Sherehe za Mapinduzi Kutimia Miaka 54.

$
0
0
 
WAZIRI wa Afya Zanzibar Mhe: Mohamoud Thabiti Kombo, akiondoa kitambaa, kuashiria kuufungua mradi wa maji safi na salama, kwa wajili ya wananchi wa kijiji cha Ngomeni shehia ya Mgelema wilaya ya Chakechake, ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 54 ya Mapinduzi Zanzibar
WAZIRI wa Afya Zanzibar Mhe: Mohamoud Thabiti Kombo, akifungua mashine ya kusambaazia maji safi na salama, kwa ajili ya wananchi wa kijiji cha Ngomeni shehia ya Mgelema wilaya ya Chakechake Pemba, ikiwa ni shamra shamra za miaka 54 ya Mapinduzi Zanzibar
WANANCHI wa kijiji cha Ngomeni shehia ya Mgelema wilaya ya Chakechake, wakifuatilia hutuba ya Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba, alioitoa wakati akimkaribisha Waziri wa Afya Zanzibar Mhe: Mahamoud Thabiti Kombo, baada ya kuufungua mradi wa maji safi na salama wa wananchi hao, ikiwa ni shamra shamra za miaka 54 ya Mapinduzi Zanzibar, 
WANANCHI wa kijiji cha Ngomeni shehia ya Mgelema wilaya ya Chakechake, wakifuatilia hutuba ya Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba, alioitoa wakati akimkaribisha Waziri wa Afya Zanzibar Mhe: Mahamoud Thabiti Kombo, baada ya kuufungua mradi wa maji safi na salama wa wananchi hao, ikiwa ni shamra shamra za miaka 54 ya Mapinduzi Zanzibar.
WANANCHI wa kijiji cha Ngomeni shehia ya Mgelema wilaya ya Chakechake, wakifuatilia hutuba ya Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba, alioitoa wakati akimkaribisha Waziri wa Afya Zanzibar Mhe: Mahamoud Thabiti Kombo, baada ya kuufungua mradi wa maji safi na salama wa wananchi hao, ikiwa ni shamra shamra za miaka 54 ya Mapinduzi Zanzibar, 
WANAFUNZIkutoka madrassa ya kijiji cha Ngomeni shehia ya Mgelema, wakicheza dufu, baada ya Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe: Mahamoud Thabit Kombo, kuufungua mradi wao wa maji safi na salama, ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi Zanzibar
AFISA habari wa ZAWA Pemba, Suleiman Anas, akijitikisa kwa kuchez dufu, muda mfupi baada ya Waziri wa Afya Zanzibar Mhe: Mahamod Thabit Kombo, kuufungua mradi wa maji safi na salama kwa ajili ya wananchi wa kijiji cha Ngomeni shehia ya Mgelema wilaya ya Chakechake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba). 

HESLB kuanza kuwasaka wadaiwa sugu 119,497 jumatatu ijayo * Wanadaiwa Tshs 285 bilioni * Ukaguzi kwa waajiri pia kufanyika

$
0
0
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Abdul-Razaq Badru akiongea na wanahabari leo (Jumatano, Jan. 3, 2018) jijini Dar es Salaam ambapo alielezea utekelezaji wa majukumu ya taasisi yake katika nusu ya mwaka 2017/2018 na kuanza kwa kampeni ya kuwasaka wanufaika sugu wa mikopo 119,497 ambao hawajaanza kurejesha. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Upangaji Mikopo Dkt. Veronika Nyahende na kushoto ni PHIDELIS Joseph, Mkurugenzi Msaidizi wa Urejeshaji Mikopo (Picha na Happiness Kihwele- HESLB). 

Na Mwandishi Wetu
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) wiki ijayo (Jumatatu, Januari 8, 2018) inatarajia kuanza kuwasaka jumla ya wanufaika 119,497 nchini kote ambao wamekiuka sheria iliyoanzisha Bodi hiyo kwa kutoanza kurejesha mikopo yenye thamani ya TZS 285 bilioni waliyokopeshwa tangu mwaka 1994/1995 na mikopo yao imeiva lakini hawajaanza kurejesha.

Aidha, Bodi ya Mikopo inatarajia kuanza kufanya ukaguzi kwa waajiri mbalimbali nchini kote ili kubaini kama katika orodha za waajiriwa wao (payrolls) kuna wanufaika wa mikopo ambao hawajaanza kurejesha.

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru (pichani) amesema leo (Jumatano, Januari 3, 2018) jijini Dar es Salaam kuwa msako huo utafanywa kwa miezi mitatu kuanzia wiki ijayo (Jumatatu, Januari 8, 2018).

Bw. Badru ametoa kauli hiyo wakati akitoa tathmini ya utekelezaji wa majukumu ya Bodi ya Mikopo kwa nusu ya mwaka wa fedha wa 2017/2018 uliomalizika Desemba 31, 2017. Katika tathmini hiyo, Bw. Badru alizungumzia mafanikio, changamoto na mipango ya kuboresha ufanisi katika utoaji wa mikopo ya elimu ya juu na ukusanyaji wa mikopo iliyoiva.

Maafisa wa Bodi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Serikali wamejipanga katika kutekeleza hili ili kuongeza makusanyo ya mwezi kutoka wastani wa TZS 13 bilioni hivi sasa hadi kufikia TZS 17 bilioni mwezi Juni, 2018.

Orodha kamili ya waajiri na wanufaika wa mikopo ambao wanakiuka Sheria ya Bodi ya Mikopo (SURA 178) kwa kutowasilisha makato au kurejesha mikopo ya elimu ya juu inapatikana katika tovuti ya Bodi ya Mikopo (www.heslb.go.tz) kuanzia leo (Jumatano, Januari 3, 2018).

Kampeni ya Kuwasaka Waajiri na Wanufaika wasiorejesha mikopo
Akifafanua zaidi, Bw. Badru amesema ingawa kila mwajiri ana wajibu wa kisheria wa kuwasilisha makato ya wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu kwa Bodi ndani ya siku 15 baada ya mwisho wa mwezi, baadhi ya waajiri wamekuwa hawafanyi hivyo na kuilazimisha Bodi ya Mikopo kuanza kuwasaka kwa nguvu.

“Katika msako huu hatutamuacha mtu au mwajiri yeyote anayekiuka sheria iliyoanzisha Bodi,” amesema Bw. Badru katika mkutano na wanahabari na kufafanua kuwa sheria iliyoanzisha Bodi ya Mikopo inawapa mamlaka ya kufanya ukaguzi na ni kosa kisheria kwa mtu yeyote kuzuia ukaguzi huo.

“Tayari tumeziongezea nguvu ofisi zetu za Kanda zilizopo Mwanza, Arusha, Dodoma na Zanzibar ili kuendesha ukaguzi na msako katika mikoa yao na ile iliyo karibu nayo ili kuhakikisha kazi hii inafanyika kwa ufanisi,” amesema Bw. Badru na kuongeza kuwa ukaguzi huo pia utafanyika jijini Dar es Salaam.   

Hali ya Ukusanyaji wa Mikopo iliyoiva hadi 2017/2018
Akizungumza kuhusu hali ya ukusanyaji wa mikopo iliyoiva hadi kufikia Desemba 31, 2018, Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema kiasi cha TZS 85 bilioni kilikuwa kimekusanywa huku lengo la makusanyo kwa mwaka mzima wa fedha utakaomalizika Juni 30, 2018 ni TZS 130 bilioni.

“Katika kazi hii ya ukusanyaji, kwa miezi hii sita tumewabaini wanufaika wapya zaidi ya 26,000 na wameanza kulipa na kufanya jumla ya wanufaika wanaolipa hadi sasa kuwa zaidi ya 121,000,”amesema Bw. Badru na kuwashukuru waajiri wote wanaotimiza wajibu wao.

Kuhusu changamoto inayokutana nazo katika kazi ya ukusanyaji wa mikopo, Bw. Badru amesema baadhi ya waajiri kutowasilisha kwa Bodi ya Mikopo orodha za waajiriwa ambao ni wahitimu wa taasisi za elimu ya juu kama sheria inavyotaka. Aidha, changamoto nyingine ni kutowasilisha makato ya wanufaika kwa Bodi kwa wakati.

Hali ya Utoaji Mikopo kwa Mwaka 2017/2018
Kuhusu utoaji mikopo kwa wanafunzi wahitaji, Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema katika mwaka huu wa masomo, jumla ya wanafunzi 122,623 wamepata mikopo yenye thamani ya TZS 422.45 bilioni. Kati yao, wanafunzi 33,244 ni wa mwaka wa kwanza waliopata mikopo yenye thamani ya TZS 110.37 bilioni na wengine 89,379 ni wanaoendelea na masomo ambao wamepata mikopo yenye thamani ya TZS 312.16 bilioni.

Katika mwaka wa masomo uliopita (2016/2017), jumla ya wanafunzi 112,409 walipangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 409.61 bilioni. Kati ya hao, wanafunzi 28,383 walikuwa wa mwaka wa kwanza na wengine 86,688 walikuwa wanaendelea na masomo.

Bodi ya Mikopo ilianzishwa kwa sheria mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi Julai 2005. Majukumu makuu ya Bodi ya Mikopo ni kutoa mikopo kwa watanzania wahitaji wenye sifa na kukusanya mikopo iliyoiva ili iweze kukopeshwa kwa wahitaji.


Makamu wa Rais Mama Samia Ahudhuria Msiba wa Mke wa Kangi Lugola.

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha maombolezo ya msiba wa mke wa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Kangi Lugola, Kamishna Msaidizi wa Polisi marehemu Mary Lugola aliyefariki siku ya tarehe 01, Januari, 2018 katika hospitali ya Rabininsia jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Kangi Lugola alipofika kutoa pole ya msiba wa mke wa Kangi Lugola, Kamishna Msaidizi wa Polisi Mary Lugola aliyefariki siku ya tarehe 01, Januari, 2018 katika hospitali ya Rabininsia jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiifariji familia ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Kangi Lugola wakati alipoenda kuwapa pole ya msiba wa Kamishna Msaidizi wa Polisi marehemu Mary Lugola nyumbani kwao klabu ya reli, Gerezani, jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Kangi Lugola wakati alipoenda kutoa pole ya msiba wa mke wake Kamishna Msaidizi wa Polisi marehemu Mary Lugola aliyefariki siku ya tarehe 01, Januari, 2018 katika hospitali ya Rabininsia jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapa pole watoto wa  marehemu Mary Lugola , mke wa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Lugola aliyefariki siku ya tarehe 01, Januari, 2018 katika hospitali ya Rabininsia jijini Dar es Salaam.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

UFUNGUZI WA BANDARI YA MKOKOTONI ZANZIBAR

$
0
0
Na Khadija Khamis –Maelezo 03/01/2017
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mhe. Mohamed Aboud Mohamed amewataka wafanyakazi wa shirika Bandari  Zanzibar kufanya kazi kwa bidii na kujenga uadilifu ili kuipatia pato serikali pamoja na kuleta maendeleo katika nchi.

Kauli hiyo ameieleza leo huko katika ufunguzi wa jengo la Ofisi ya Shirika la Bandari Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini  Unguja ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra ya sherehe ya miaka 54 ya Mapinduzi  Matukufu ya Zanzibar.

Alisema wafanyakazi  waweze kupambana katika kuhakikisha wanazuia rushwa na uingizaji wa biashara haramu jambo ambalo linaharibu nguvu kazi ya taifa na kuipunguzia pato serikali

“Lazima wafanyakazi wadhibiti kuvuja mapato kama hakuna mapato katika serikali na maendeleo hayapo na kipato hakiwi ikiwa kinatumiwa kwa ubadhirifu ” alisema Waziri .

Aidha alisema juhudi za serikali ni kutekeleza ilani ya chama ambayo inalengo la kuwaletea maendeleo mbali mbali wananchi wake bila ya upendeleo na kusimamia utekelezaji wa ahadi   jambo ambalo ndio malengo makuu ya Mapinduzi .

Alifahamisha serikali inatoa huduma kwa wananchi wote bila ya kuwa na ubaguzi wa rangi wala jinsia yoyote katika sekta mbali mbali za serikali pamoja na njanja tofauti za kisiasa kiuchumi na kijamii .

Alisema bandari ndogo ndogo zina mtindo wa kupitisha  biashara ya haramu ikiwemo madawa ya kulevya na kutumia mbinu mbali mbali za kuichafua nchi hivyo alizitaka taasisi husika kuchukua juhudi za kukabiliana nazo.

Alieleza kuwa Zaidi ya Shilling Million 378 zilizotumika katika Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Shirika la Bandari la Mkokotoni na kuhakikisha  kuwa si muda mrefu utaanza ujenzi wa gati ambalo linatarajiwa liwe la kisasa lenye hadhi inayolingana na mkoa huo.

Nae katibu Mkuu wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mustafa Aboud Jumbe amesema ujenzi huu ni utekelezaji wa ilani  ya chama ambayo aliahidi Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein ni moja ya ahadi zake za  kuhakikisha anaimarisha maendeleo  ya miundo mbinu ya Mkoa Kaskazini kwa  kutekeleza ahadi mbali mbali ikiwemo  ujenzi  wa Ofisi ya Bandari pamoja na Gati mpya  ya mkokotoni ambayo inatarajia kuchukua mizigo ya uzito wa tani mia moja.

Aidha alisema  ujenzi wa  bandari hiyo inakusudiwa kutumia Zaidi ya Tsh,Bilioni moja na  Million 800 na gati hiyo inatarajiwa kuwa na  urefu  wa  mita  170 na upana wa mita sita  bandari hiyo inasafirisha abiria kwa kwenda na kurudi pamoja na mizigo mkaa mbao pamoja na dhamani .

Shirika la Bandari lilianzishwa mwaka 1997 ikiwa ni muunganiko wa Idara mbili ikiwemo  Idara ya Bandari pamoja na Zanzibar Ofeji kwa lengo la kuleta ufanisi na kuimarisha uchumi wa Zanzibar.

BREAKING NEWS : NEC YATANGAZA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA KINONDONI NA SIHA PAMOJA NA KATA 4

Waziri wa Habari aweka jiwe la msingi nyumba ya wagonjwa na kufungua Jengo la huduma za Mkono kwa Mkono Makunduchi

$
0
0
 Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe, Rashid Ali Juma akikunjuwa Kitambaa kuashiria uwekaji wa Jiwe la msingi Nyumba ya Wananchi itakayotumika kwa kusubiri kuwaona Wagonjwa katika Hospitali ya Makunduchi alipokwenda kufungua Jengo la huduma za Mkono kwa Mkono Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za Maadhimisho ya kutimia miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe,Rashid Ali Juma wapili kulia akipata maelezo kutoka kwa Diwani wa Wadi ya Makunduchi Zawadi Hamdu Vuai kuhusiana na ujenzi wa Nyumba ya wananchi itakayotumika kuwaona Wagonjwa katika Hospitali ya Makunduchi Wilaya ya kusini Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za Maadhimisho ya kutimia miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe, Rashid Ali Juma akikata Utepe kuashiria Ufunguzi wa Jengo la huduma za Mkono kwa Mkono Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za Maadhimisho ya kutimia miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe, Rashid Ali Juma akikunjuwa Kitambaa kuashiria Ufunguzi wa Jengo la huduma za Mkono kwa Mkono Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za Maadhimisho ya kutimia miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe, Rashid Ali Juma katikati akipata maelezo kwa Daktari dhamana wa Hospitali ya Makunduchi Dk,Ali Omar Hamdu kuhusiana na ofisi za Jengo la huduma za Mkono kwa Mkono baada ya kulifungua Makunduchi Wilaya ya  Kusini Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za Maadhimisho ya kutimia miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 Wananchi mbalimbali waliohudhuria katika Ufunguzi wa Jengo la huduma za Mkono kwa Mkono lililofunguliwa na Waziri wa  Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe, Rashid Ali Juma Makunduchi Wilaya ya  Kusini Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za Maadhimisho ya kutimia miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Mkurugenzi wa Huduma za Hospitali Zanzibar Dk,Mohammed Dahoma  akizungumza na wananchi mbalimbali baada ya kufunguliwa Jengo la huduma za Mkono kwa Mkono na Waziri wa  Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe, Rashid Ali Juma Makunduchi Wilaya ya  Kusini Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za Maadhimisho ya kutimia miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe, Rashid Ali Juma akitoa hotuba baada ya kufungua Jengo la huduma za Mkono kwa Mkono na kuweka jiwe la msingi Nyumba ya wananchi ya kusubiri kuwaona wagonjwa Makunduchi Wilaya ya  Kusini Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za Maadhimisho ya kutimia miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

Waziri Haji Omar Kheir azindua Wodi ya wazazi ya kinamama ikiwa ni mwendelezo wa shamra shamra za miaka 54 ya mapinduzi

$
0
0
Na Ali Issa Maelezo   3/1/2018 

Waziri wa nchi afisi ya Rais Tawala za mikoa na idara maalum za Serikali Haji Omar Kheir amewataka kinamama kujifungulia Hospitalini na kuacha mazoea ya kujifungulia nyumbani ili kuepuka matatizo yanayoweza kujitokeza. 

Hayo ameyasema leo katika kituo cha Afya cha Sebleni wakati wa uzinduzi wa Wodi ya wazazi ya kinamama wa zaidi ya shehia saba ikiwa ni mwendelezo wa shamra shamra za miaka 54 ya mapinduzi ya Zanzibar.

Amesema kinamama kujifungulia hospitali kuna wapa asilimia kubwa kuzaa salama kwani inapotokea tatizo inakuwa ni rahisi kulitatua,kuliko kujifungulia nyumbani.

Amesema frusa hiyo waitumie na waache kwenda jifungulia nyumbani kwani vituo vya Afya vipo kwa ajiliyao navinatoa huduma bure kwa kuzaa.

“Nakuombeni acheni kujifungulia nyumbani kwa sababu nyumbani hakuna utalamu wa kutosha na likitokea tatizo ni vigumu kulikabili”alisema Waziri huyo.

Waziri huyo akijibu changamoto ya kutoajiriwa wafanyakazi wanao jitotea waliopo hapo waliokuwa hawajaajiriwa kwa kipindikirefu ameitaka Ofisi ya mkoa, wilaya na manispaa kulitatua tatizo hilo kwa kulifikisha idara ya uajiri ili ufumbuzi wa ajira upatikane.

Nae mkuu wa mkoa wa mjini magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud amesema kuwa kufunguliwa kwa wodi hiyo ni fursa ya kipekee kwa mkoa huo una idadi kubwa ya wazazi wanao kwenda hospital ya mnazi mmoja hospitali kujifungua.

Amesema malengo na dhamira ya mapinduzi ya Zanzibar ni kuwaondolea wananchi matatizo yanayo husiana na huduma za kijamii ikiwemo Afya,maji,elimu hivyo ni jukumu la wananchi kuzidisha mashirkiano kwa serikali yao.  

Nae Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Jamala Adam Taib alisema ujenzi wa wodi hiyo ni msaada wa Shirika la DANIDA na UNFPA kujenga ukuta na kutoa vifaa tiba.

Wodi hiyo ya Wazazi kwa sasa itakuwa inazihudumia shehia saba ikiwemo Sebleni, Amani,kilimahewa,magogoni, na Kwa mtipura.

Taarifa maalum kuhusu hali ya mafuta Zanzibar

$
0
0
TAARIFA MAALUM KUHUSU HALI YA MAFUTA ZANZIBAR

Kufuatia hali ya kupungua Mafuta ya Petroli iliyojitokeza hasa katika Vituo vya Mafuta vya Kampuni ya GAPCO, na kusababisha Foleni katika Vituo vya Mafuta vya Kampuni za ZP na UP, ZURA imechukua hatua zifuatazo kukabiliana na changamoto hiyo:-

Meli ya MT Ukombozi Jana imefanikiwa kupakia Mafuta ya Petroli Tani Elfu Moja na Mia Nne (1400 Metric Tones) sawa na Lita Milioni moja Laki Nane na Arobaini na Nane Elfu (1,848,000). Mafuta hayo yanatarajiwa kufika Leo na kusambazwa Vituoni Kesho.

Pia ZURA inaendelea kusimamia zoezi la usambazaji na uuzwaji wa mafuta vituoni kwa yale yaliyopo hadi Mafuta yaliyoagizwa yatakapofika nchini na kuhakikisha yanauzwa kwa mujibu wa maelekezo ya Mamlaka.

Katika kutekeleza hili, ZURA inahakikisha Mafuta yaliyopo yanasambazwa Vituoni ili kukabiliana na hali iliyotokea.

Hali ya Mafuta iliyopo Nchini kwa sasa ni kama ifuatavyo:-

Kampuni ya GAPCO

·        Petrol: Lita 20,000

·        Diesel: Lita 314,106

·        Kerosene: Lita 78,576

Kampuni ya ZANZIBAR PETROLEUM (ZP)

·        Petrol: Lita 40,000

·        Diesel: Lita 89,884

·        Kerosene: 144,443

Kampuni ya UNITED PETROLEUM (UP)

·        Petrol: Lita 60,000

·        Diesel: Lita 1,006,000

·        Kerosene: Lita 312,663

Aidha, upungufu umejitokeza kwa Mafuta ya Petroli tu, hali ya upatikanaji wa bidhaa nyengine za Mafuta kama vile Dizeli na Mafuta ya Taa ipo kama kawaida.

Kwa Kampuni za ZP na UP zinatarajiwa kuingiza Mafuta kwa kutumia Meli zao kuanzia Kesho Tarehe 4/01/2018, ili kuongeza kiwango cha Mafuta kuwa ya kutosheleza nchini.

Wananchi wanaombwa kuwa wastahamilivu, wakati Mamlaka inafanya juhudi za kutosha kuhakikisha hali ya upatikanaji wa Mafuta inarejea katika hali ya kawaida na kukidhi mahitaji ya Soko.

Matarajio ya ZURA ni kwamba hadi Siku ya Ijumaa Tarehe 5/01/2018 upatikanaji wa bidhaa za Mafuta utakua umeshapatiwa ufumbuzi na kurudi katika hali ya kawaida, na kuanzia Jumamosi Tarehe 6/01/2018 Mafuta yatakua yanapatikana kwa uhakika. Tunaomba ushirikiano kutoka kwa Wadau wote wa Mafuta na Wananchi, aidha tunawaomba Wananchi wawe watulivu na wastahamilivu katika kipindi hiki.

IMETOLEWA NA MAMLAKA YA UDHIBITI WA HUDUMA ZA MAJI NA NISHATI ZANZIBAR (ZURA)

Mchezo wa Kombe la Mapinduzi Kati ya Azam na Jamuhuri Uwanja wa Amaan Zanzibar. Azam Imeshinda Bao 4-0.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Azindua Jengo Jipya la Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Mazizini Zanzibar Ikiwa ni Shamrashamra za Sherehe za Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiondoa kipazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Jengo Jipya la Mtakwimu Mkuu wa Serekali lililopo mazizini Zanzibar, ikiwa ni shamrashamra za sherehe za Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria kulifungua jengo jipya la Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar katika maeneo ya mazizini Zanzibar kulia Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dk. Khalid Salum Mohammed (MBM),Mkurugenzi Mkaazi Banki ya Dunia,Ms. Bella Bird na kushoto Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Tanzania Dk. Ashatu Kijaji wakishiriki katika kukata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo hilo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria kulifungua jengo jipya la Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar katika maeneo ya mazizini Zanzibar kulia Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dk. Khalid Salum Mohammed (MBM),Mkurugenzi Mkaazi Banki ya Dunia,Ms. Bella Bird na kushoto Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Tanzania Dk. Ashatu Kijaji wakishiriki katika kukata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo hilo
MTAKWIMU Mkuu wa Serikali Bi, Mayasa Mahfoudh Mwinyi , akitowa maelezo kwa Rai wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akitembelea jengo hilo baada ya kulifungua rasmin leo, ikiwa ni shamrashamra za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akipanda mti wa mnazi katika eneo la jengo la Mtakwimu Mkuu wa Serikali baada ya uzinduzi wa jengo hilo huko mzizini Zanzibar
MKURUGENZI Mkaazi wa Banki ya Dunia Ms.Bella Bird akizungumza na kutowa salamu za Banki ya Dunia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jengo la Mtakwimu Mkuu wa Serikali uliofanyika katika eneo la mazizini Zanzibar
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango Tanzania Dk. Ashatu Kijaji akizungumza wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Jengo jipya la Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali mazizini Zanzibar
WAZIRI wa Fedha na Mipango Zanzibar Dk. Khalid Salum Mohammed, akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo la Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali katika eneo la mazizini Zanzibar 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akionesha Tunzo ya Takwimu aliyokabidhiwa na Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dk. Khalid Salum Mohammed, wakati wa hafla hiyo.iliofanyika katika viwanja vya jengo hilo mazizini Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jengo la Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar lilioko katika eneo la mazizini, ikiwa ni shamrashamra za Miaka 54 ya Mapinduzi Zanzibar
BAADHI ya wageni waalikwa katika hafla ya Uzinduzi wa engo Jipya la Mtakwimu Mkuu wa Serikali wakifuatilia hafla hiyo wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ai Mohamed Shein, akihutubia. baada ya uzinduzi huo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Awazawadia Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Soka la Ufukweni Zanzibar Sand Heroes Kwa Kutowa Ubingwa wa Mchezo Huo Katika Michuano ya Kimataifa Ilioandaliwa na TFF Dar es Salaam Kwa Kuifunga Timu ya Malawi Bao 3 - 2.

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akijumuika na Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Sand Heroes katika chakula cha mchana alichowaandalia katika viwanja vya Ikulu Zanzibar kwa kuchukua Ubingwa wa Mchezi wa Beach Soka michuano ilioandaliwa na TFF Jijini Da es Salaam baada ya kuingia faina na kuifunga Timu ya Malawi kwa mabao 3 -2
WACHEZAJI wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Sand Heroes wakijumuika katika chakula cha mchana walichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kuwapongeza na kuwazawadia kila Mchezaji shilingi milioni moja taslim, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ikulu Zanzibar leo
WACHEZAJI wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Sand Heroes wakijumuika katika chakula cha mchana walichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kuwapongeza na kuwazawadia kila Mchezaji shilingi milioni moja taslim, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ikulu Zanzibar leo
KOCHA Mkuu wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Sand Heroes Ali Shariff Adof , akizungumza wakati wa hafla hiyo ya chakula cha mchana kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, walipofika Ikulu Zanzibar kutambulishwa baada ya kuchukua Ubingwa wa Mchezo wa Bech Sko kwa kuifunga Timu ya Malawi kwa bao 3-2. michuani iliofanyika Jijini Dar es Salaam wiki iliopita 
RAIS wa Zanzibar na Mwnyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akifurahia jambo wakati wa kutambulishwa kwa Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Sand Heroes na Kocha Mkuu Ali Shariff Adof, wakati hafla ya chakula cha mchana alichoandaa kwa ajili yao
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa ufukweni Zanzibar Sand Heroes iliotowa Ubingwa wa mchezo huo baada ya kuifunga Timu ya Malawi 3 -2, wakati wa mashindano ya Kimataifa yalioandaliwa na TFF Jijini Dar es Salaam wiki iliopita, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ikulu Zanzibar leo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi mmoja wa Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Sand Heroes shilingi milioni moja kwa ajili ya kuwapongeza kwa ushindi waliopata wa kulitowa Kombe la Ubingwa wa Mchezo wa Soka la Ufukweli lililoandaliwa na TFF Jijini Dar es Salaam
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pamoja na Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Sand Heroes,wakiwa katika picha ya pamoja bada ya hafla hiyo ya kuwapongeza na kuwazawadia kila mchezaji na Viongozi wao shilingi milioni moja kila mmoja
MAWAZIRI na Makatibu Wakuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Sand Heroes, baada ya hafla ya chakula cha mchana kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, katika viwanja ya Ikulu Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwnyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwa na Kombe la Ubingwa wa Mchezo wa Soka la Ufukweni baada ya kukabidhiwa wakati wa hafla ya chakula cha mchana alichowaandaliwa wachezaji hao, akiwa na Waziri wa HabariUtalii Utamaduni na Michezo Zanzibar. Mhe. Rashid Ali Juma.leo Ikulu Zanzibar
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Wachezaji wa zamani wa Zanzibar na Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Znzibar Sand Heroes baada ya hafla ya chakula cha mchana Ikulu Zanzibar leo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Mchezo wa Sola la Ufukweni Zanzibar Sand Heroes baada ya hafla ya chakula cha mchana na kuwazawadia kila mmoja shilingi milioni moja
Viewing all 36204 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>