Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all 35828 articles
Browse latest View live

WAZIRI KIGWANGALLA ATUA NCHINI HISPANIA, AUNGURUMA

$
0
0

Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) akiwa ni miongoni mwa Wazungumzaji  kwenye kongamano la 10 la Uwekezaji na Biashara katika sekta ya Utalii Afrika (Investour) lililofanyika jana katika jiji la Madrid nchini Hispania ambapo katika Kongamano hilo Waziri Kigwangalla alitumia fursa hiyo  kuwaita Wawekezaji kuja nchini kwa ajili ya kuwekeza katika sekta ya Utalii na viwanda.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla (wa tatu kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Washiriki wa kongamano la 10 la Uwekezaji na Biashara katika sekta ya Utalii Afrika (Investour) lililofanyika Jana katika jiji la Madrid nchini Hispania ambapo katika Kongamano hilo Waziri Kigwangalla alitumia fursa hiyo kuwaita Wawekezaji kuja nchini kwa ajili ya kuwekeza katika sekta ya Utalii na viwanda.

Na Mwandishi wetu-Hispania
Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla amewaita Wawekezaji kuja nchini Tanzania kwa ajili ya kuwekeza katika sekta ya Utalii wakati aliposhiriki kongamano la 10 la Uwekezaji na Biashara katika sekta ya Utalii Afrika.

Kongamano hilo limefanyika jana katika jiji la Madrid nchini Hispania likiwa limeandaliwa na Shirika la Utalii  la Umoja wa Mataifa (UNWTO)kwa kushirikiana na Taasisi za Casa Afrika pamoja na Taasisi yamaonesho ya Biashara ya Madrid (IFEMA) na kushirikisha nchi mbali mbali duniani.

Katika Kongamano hilo, Waziri Kigwangalla alipata fursa ya kuwa mmoja wa wazungumzaji ambapo amewahakikishia Wawekezaji wenye nia ya kuja kuwekeza nchini Tanzania kwamba ni sehemu salama ukizingatia hali ya amani na utulivu iliyopo nchini lakini pia kuna vivutio vingi vya utalii na fursa za kuwekeza.

"Nawakaribisheni nyote, Njooni Tanzania muwekeze kufuatia uwepo wa mazingira na miundombinu bora kwa ajili uwekezaji katika sekta ya utalii pamoja na viwanda" Alisema

Waziri Kigwangalla pia  alitumia nafasi hiyo kwa kuutangaza ukanda mpya wa kusini mwa Tanzania ambao umejaliwa kuwa na vivutio vya Utalii vya kipekee vinavyopatikana katika  Hifadhi ya Taifa ya  Ruaha, Mikumi pamoja  Pori la Akiba Selous.

Katika hatua nyingine , Waziri Kigwangalla wakati akizungumza  katika kongamano hilo aliwaeleza washiriki hao  kuhusu  juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli kwa kutaja mifano michache kama vile kufufua kampuni ya ndege (ATCL) kwa kununua ndege mpya sita pamoja kujenga chanzo kikubwa cha kuzalisha  umeme katika mto Rufiji.

Alisema serikali ya Tanzania pia inaendelea na mradi wa kisasa wa ujenzi wa njia mpya ya kisasa ya reli (Standard Gauge) pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara ili kurahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo.

Alibainisha kuwa kutokana na juhudi hizo zilizochukuliwa  na Serikali hiyo, sekta ya utalii itaweza kusonga mbele ikiwa pamoja na kurahisisha usafiri kwa watalii pamoja na  wawekezaji kwa ujumla.



Serikali Itaendelea Kushirikiana na Sekta Binafsi-Dkt Abbasi.

$
0
0

Mwandishi wetu-MAELEZO.25-1-2019.
SERIKALI itaendelea kushirikiana na sekta binafsi katika kutoa fursa kwa watu wengi kwa kuwezesha utekelezaji wa miradi mingi kwa mapana, katika Taasisi za serikali na Taasisi binafsi.

Akizungumza katika mjadala wa Clouds Media katika kipindi cha The Big Breakfast chenye kauli mbiu ya The power of Man yaani Nguvu ya Pamoja kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Serena, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassan Abbasi alisema kuwa serikali inaendelea na jukumu la ujenzi wa nchi kwa kushirikiana na sekta binafsi.

“Tunatambua na kuheshimu nguvu ya wengi kama kauli mbiu hii inavyoeleza, katika dhana ya maendeleo kuna mengi Serikali inafanya ili kutekeleza azma yake kwa wananchi, mfano Ujenzi wa madaraja mbalimbali nchini, Miradi ya Maji, Miradi ya Umeme, Ujenzi wa vituo vya afya na Hospitali na kulete ndege, kwetu sisi haya ni maendeleo makubwa sana”, Dkt. Abbasi.

Katika dhana ya Nguvu ya pamoja, Dkt. Abbasi alisema kuwa kauli mbiu hii inaonesha namna gani sasa haya mambo ambayo Serikali inafanya yanawafikia wananchi na kuwanufaisha  popote walipo.

Dkt.Abbasi alieleza kuwa katika mjadala  wa nguvu ya pamoja dhana ya  maendeleo  ina nadharia mbili ambazo wasomi wanazijadili duniani kote ikiwa ni moja ya miongozo ya maenedeleo duniani, huku wakiamini katika nadharia ya  maendeleo ni watu na wengine wakiamini katika nadharia ya maendelo ni vitu.

“nilichokisema ni kwamba duniani kuna mjadala mkubwa sana katika suala la  maendeleo, wapo wanaoamini kwamba maendeleo ni watu kwa mambo yanafanyika moja kwa moja  na yanagusa watu, wapo wanaoamini kwamba maendeleo ni vitu kwamba huwezi kuwaendeleza watu bila kuwajengea miundombinu kama vile barabara, reli, umeme na maji”, Dkt Abbasi.

Katika kuunga mkono kauli mbiu ya nguvu ya pamoja, Dkt Abbasi alieleza kuwa katika nadharia mbili za maendeleo Serikali inaamini katika nadharia zote  yaani maendeleo ni vitu kwani inatekeleza miradi mbalimbali kama barabara, Umeme, Maji, Afya na elimu, huku ikiwawezesha wananchi kupata elimu bure, dawa katika vituo vya afya na umeme, ambao kwa sasa unafika mpaka vijijini kwa maana ya maendeleo ni watu.

Aidha Dkt Abbasi alieleza kuwa kauli mbiu ya Nguvu ya pamoja kutoka Clouds Media ni moja ya njia kubwa katika kutimiza malengo la wananchi kwa kutekeleza na kusimamia miradi mbalimbali ambayo  ndiyo inawawezesha wananchi kufanya shughuli zao za maendeleo.

Kwa upande wa sekta ya habari Dkt.Abbasi alieleza kuwa Serikali inafanya kazi kubwa kwa kushirikiana na sekta binafsi katika sekta hiyo muhimu pamoja na sekta zingine ambazo zinawezesha wananchi kujikwamua kimaendeleo.

“Serikali ndiyo mwezeshaji mkuu wa sekta mbalimbali, Sekta haiwezi kufanya kazi nchini bila Serikali kuiwezesha kwa hiyo katika dhana hiyo hiyo ya Nguvu ya pamoja Serikali inashiriki kwa nguvu zote”, Dkt Abbasi.

Dkt. Abbasi aliongeza kuwa Serikali itaendelea kuheshimu uwepo wa sekta binafsi katika sekta ya habari kwani mpaka sasa imewezesha upatikanaji wa leseni kwenye majarida na mageti 202, Vituo vya Televisheni 35 na Redio 160.

Alieleza pia kuwa nguvu ya pamoja ni pamoja na watendaji wa Serikali kushirikiana na sekta binafsi ili kuwawezesha kupata huduma  mara moja pale inapohitajika kwa sababu watakuwa wanatenda jambo la kuwafanya wengi kupata ajira katika sekta hizo.

“Ukiangalia uanzishwaji wa viwanda ni lazima kuna mtendaji alijituma kutoa leseni, maendeleo ya biashara mbalimbali, kilimo na sekta zingine ni lazima upate leseni ni hata  kwenye sekta ya habari hii inamaana kuwa mtendaji wa Serikali unapoharakisha kwa kufuata sheria na taratibu kuhakikisha mtu anapata leseni ya kuanzisha kiwanda, Biashara kubwa au gazeti utakuwa umeajiri watu wengi bila kujua na hii ndiyo the power of man (Nguvu ya pamoja)”, Alisisitiza Dkt. Abbasi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu na Mumiliki wa Clouds media Group Joseph Kusaga aliahidi kushirikiana na Serikali katika kutangaza maendeleo ya nchi hasa kwenye sekta ya usafiri wa anga (shirika la ndege la Tanzania AirTanzania) pamoja na sekta ya utalii  katika kampeni mbalimbali zitakazokuwa zinatangazwa Clouds Media.

Shehena ya Kwanza ya Madawati ya Wanafunzi wa Skuli za Sekondari na Msingi za Zanzibar Yawasili.

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Uhamasishaji wa Uchangiaji wa Vikalio vya Wanafunzi ambae pia ni Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumisha wa Umma na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Riziki Pembe Juma wakitoa taarifa mbele ya waandishi wa habari kuhusu kuwasili vikalio vya Skuli za Serikali za Zanzibar.

Baadhi ya wajumbe wa Kamati Maalum ya Uhamasishaji wa Uchangiaji wa Vikalio vya Wanafunzi pamoja na Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati hiyo Haroun Ali Suleiman alipokuwa akitoa taarifa ya kuwasili awamu ya kwanza ya vikalio kwa ajili ya Skuli za Serikali katika Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mazizini.
Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Uhmasishaji wa Uchangiaji wa Vikalio vya Wanafunzi Haroun Ali Suleiman na Makamu Mwenyekiti Riziki Pembe Juma pamoja na Wajumbe wawili wa kamati hiyo Ali Khalil Mirza (kulia) na Naila Majid Jidawi wakiwa wamekalia madawati huko Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Mazizini. 
                           Picha Na Miza Othman -Maelezo Zanzibar.

Na.  Khadija Khamis Maelezo Zanzibar.
Jumla ya seti 22,000 za vikalio ikiwa ni awamu ya kwanza ya viti na meza 44,620 zilizonunuliwa na Serikali ya Zanzbar na kugharimu shilingi bilini 2.96 vimewasili nchini kutoka China kwa ajili ya wanafunzi wa skuli za sekondari.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Mazizini, Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Uhamasishaji wa Uchangiaji wa Vikalio vya Wanafuzi ambae pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman alisema kazi za usambaji wa samani hizo itaanza mwezi ujao.
Alifahamisha kuwa awamu ya pili wa vikalio 22,620 unatarajiwa kufika Zanzibar Mwezi Februari 2019 na kukamilisha idadi ya viti na meza 44,620 ambavyo vitawawezesha wanafunzi wa Skuli za Sekondari 88,520 kuwa na vikalio katika madarasa yao kwa utaratibu wa mikondo miwili.
Hata hivyo Mwenyekiti Haroun alieleza kuwa pamoja na kupatikana kwa vikalio hivyo bado kutakuwa na upungufu wa vikalio 17,950 kwa Skuli za Sekondari kwa utaratibu wa mikondo miwili ya masomo.
Aliongeza kuwa Kamati Maalum ya kuhamasisha uchagiaji wa vikalio inakusudia kununua madawati ya wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la tatu hivi karibuni kwa lengo la kuondosha tatizo la vikalio.
Alisema katika mwaka huu wa fedha, Serikali imetenga shilingi bilioni 2.5 kwa ajili ya vikalio na shilingi milioni 465.8 zilizobakia katika michango iliyotolewa hapo awali na wachangiaji mbali mbali na kufikia shilingi bilioni 3.36 kwa ununuzi wa vikalio.
Mwenyekiti Haroun alisema mwaka 2017, Serikali iliunda Kamati maalum ya uhamasishaji wa uchangiaji vikalio vya wanafunzi yenye wajumbe 11 wakiwemo Mawaziri wanne, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Wafanyabiashara maaarufu ili kukabiliana na upungufu wa vikalio maskulini.
Alisema jukumu kubwa la Kamati hiyo ni kuwahamasisha Wafanyabiashara viongozi mbali mbali, Wafanyakazi, wananchi na wahisani mbali mbali kuchangia fedha kwa ajili ya ununuzi wa vikalio kwa ajili ya wanafunzi wa skuli za Serikali.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Riziki Pembe Juma amezitaka Kamati za Skuli kushirikiana na Walimu na wazazi kuhakikisha madawati hayo yanalindwa na kutunzwa vizuri ili yaweze kudumu muda mrefu.
Alieleza matarajio yake kuwa kwa vile madawati hayo yanapelekwa katika skuli za sekondari zenye wanafunzi wanaojielewa watafanya juhudi maalum na iwapo atatokea mwanafunzi kufanya uharibifu wa makusudi atalazimika kulipa.
Mfuko wa Madawati umekusanya shilingi bilioni 1.37 na kupitia fedha za mfuko wa Bandari uliingiza shilingi bilioni 2.5 na kufanya jumla ya shilingi bilioni 3.84 ambazo zimetumika kununua vikalio vya viti na meza 44, 620 kutoka Kampuni ya Guangzhou Everprety Furniture ya China.

Mhandisi wa Wilaya na Mkandarasi Waliomdanganya Naibu Waziri wa Maji,Mhe.Juma Aweso,Watupwa Mahabisu.

$
0
0
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliji,Juma Aweso akitizama namna mafundi wakiunganisha Bomba za Maji  katika mradi unaopeleka maji katika Kata ya Sopeko kikiwemo kijiji cha Lendikinya wilayani Monduli katika mkoa wa Arusha.
Mafundi wakiendelea na uunganishaji wa Bomba za kupeleka Maji katika kijiji cha Lendikinya wilayani Monduli mkoa wa Arusha.
Mhadisi wa Maji wa wilaya ya Monduli Charles Seidea akimueleza Naibu Waziri wa Maji ,Juma Aweso kuhusu namna mradi huo ulivyotekelezwa katika kijiji cha Lendenyika wilayani Monduli.
Baadhi ya Wananchi katika kijiji cha Lendenyika wilayani Monduli wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Juma Aweso (hayupo pichani) alipotembelea mradi huo kujionea maendeleo yake.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Juma Aweso akiwa ameongozana na Mbunge wa jimbo la Monduli ,Julius Kalanga pamoja na wananchi wakienda kujionea namna mkandarasi alivyopitisha Bomba za Plastiki kwenye Korongo badala ya Bomba za Chuma.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Juma Aweso akitizama Bomba za Plastiki zilizopitishwa katika Makorongo badala ya Bomba za Chuma katika mradi wa maji wa kusaidia vijiji 10 vya kata ya Sopeko wilayani Monduli.
Baadhi ya Bomba za Plastiki zikiwa zimepita kwenye Korongo badala ya Bmba za Chuma .
Askari Polisi akiwa amewashikilia ,Mhandisi wa Maji wa wilaya ya Monduli,Charles Saidea (kulia) na Mkandarasi ,Ayo Jeremia wa kampuni ya Meru Constructions mara baada ya Naibu Waziri kuamuru wakamatwe kutokana na kubainika kufanya udanganyifu katika mradi huo.
Mhadisi wa Maji wa wilaya ya Monduli,Charles Saidea akiingia kwenye gari la Polisi mara baada ya kushikiliwa kwa amri ya Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Juma Aweso baada ya kubaini kuwepo kwa udanganyifu katika mradi wa Maji unaendelea katika kijiji cha Lendenyika wilayani Monduli.
Mkandarasi ,Ayo Jeremia wa kampuni ya Meru Constructions akiingia kwenye gari la Polisi mara baada ya kushikiliwa kwa amri ya Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Juma Aweso baada ya kubaini kuwepo kwa udanganyifu katika mradi wa Maji unaendelea katika kijiji cha Lendenyika wilayani Monduli.
Mkandarasi ,Ayo Jeremia wa kampuni ya Meru Constructions pamoja na Mhandis wa Maji wa wilaya ya Monduli ,Charles Saidea wakiwa kwenye gari la Polisi mara baada ya kushikiliwa kwa amri ya Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Juma Aweso baada ya kubaini kuwepo kwa udanganyifu katika mradi wa Maji unaendelea katika kijiji cha Lendenyika wilayani Monduli.
Baadhi ya wananchi katika kijiji cha Lendenyika wakishuhudia wakati watalaamu hao wakichukuliwa katika gari la Polisi.


Na.Dixon Busagaga,Monduli.
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Juma Aweso ameamuru kukamatwa na kuwekwa mahabusu kwa Mhandisi wa Maji wa wilaya ya Monduli ,Charles Saidea na Mkandarasi kutoka kampuni ya Meru Constructions ,Ayo Jeremia kwa tuhuma za kufanya udanganyifu katika miradi wa maji inayoendelea katika vijiji 10 vya Halmashauri ya wilaya ya Monduli .

Waziri Aweso ametoa agizo hilo katika kijiji cha Lendinyika wakati wa ziara yake ya siku moja katika wilaya ya Monduli kukagua utekelezaji wa Miradi ya Maji katika vijiji 10 vya Halmashauri hiyo,ziara  ambayo hata hivyo alilazimika kuikatisha mara baada ya kubaini  kuwepo kwa taarifa zinazo kinzana na taarifa ya utekelezaji wa mradi wa maji wenye thamani ya Sh Bil 1 na Mil 79 .

Mbali na uwepo wa dosari nyingi za kiufundi ,mradi huo unaotajwa kukamilika kwa asilimia 85 bado haujaanza kutoa maji huku Mkandarasi akieleza kuidai Serikali sehemu ya fedha za mradi hu jambo ambalo Mhandisi alionekana kupinga uwepo wa madai hayo.

Hoja ya kuwepo kwa Mabomba ya plastiki yaliyopita katika Makorongo iliibuliwa na mmoja wa wakazi wa kijiji cha Lendikinya Lemta Naisikie baada ya kutaka kujua kama ni sahihi kwa mkandarasi kupitisha Bomba hizo katika sehemu za wazi badala ya bomba za chuma.

“Swali langu ni moja ,Bomba zilizotandazwa kuleta maji katika kisima kuu  ,kuna sehem za Makorongo zote zimewekwa hii bomba la mpira ,hii naona ni changamoto afadhali ingewekwa bomba la chuma na maeneo mengine kuna mawe tungeomba mkandarasi atandaze bomba la chuma ili zisilete athari baadae”alisema Naisikie.

Baada ya kutolewa kwa hoja hiyo Naibu Waziri ,Aweso aliamua kutembelea baadhi ya Makorongo na kujionea Bomba la Plastiki likiwa limepita juu badala ya Bomba la Chuma ndipo akaamua kutoa maelekezo .

“Viongozi wenu wote wanazungumzia swala la maji ,Lendikinya ni moja ya vijiji vyenye changamoto kubwa sana ya maji ,Mbunge wenu amepiga sana kelele kuhusu maji kwa wananchi wa Monduli,sasa sisi leo tumekuja hapa tumeona kuna mradi wa zaidi ya sh Bil 1 na Mil 79 lakini mradi uko zaidi ya asilimia 80 lakini maji kwa wananchi hakuna .”alisema Aweso 

“Unawauliza wataalamu wetu wakupe taarifa zile sahihi ,hawakupi ,leo mwananchi huyu wa kawaida kabisa anakupa taarifa sahihi mahala ambapo yalitakiwa kuwekwa mabomba ya chuma yameweka mabomba ya plastiki na hakuna usimamizi wa iana yoyote .”aliongeza Aweso.

Magazetini leo Jumapili 27,Janyary 2019.

SBL Yazindua Kampeni ya ‘Usitumie Kilevi na Kuendesha Chombo cha Moto’ Jijini Mwanza

$
0
0

Mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti John Wanyancha, akizungumza na wadau wa usafiri jijini Mwanza, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Usinywe na Kuendesha.

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Mwanza Mkadam Mkadam, akizungumza na wadau wa usafiri jijini Mwanza, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Usinywe na Kuendesha.

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Mwanza Mkadam Mkadam, akizungumza na wadau wa usafiri jijini Mwanza, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Usinywe na Kuendesha,kushoto ni Mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti John Wanyancha na kulia ni Mrakibu wa Polisi Mwandamizi Audax Majaliwa. 
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti John Wanyancha(kushoto) akimshukuru Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Mwanza Mkadam Mkadam alipozindua mafunzo kwa  wadau wa usafiri jijini Mwanza, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Usinywe na Kuendesha.


Mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti John Wanyancha, akiwasilisha mada ya kuepuka kunywa na kuendesha kwa wadau wa usafiri jijini Mwanza, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Usinywe na Kuendesha.

Wadau wa usafiri jijini Mwanza wakifuatilia mada wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Usinywe na Kuendesha inayofanywa na kampuni ya Bia ya Serengeti.


Na.Mwandishi Maalum ,Mwanza.
Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imezindua kampeni inayolenga kutoa elimu kwa umma juu ya unywaji wa kistaarabu, ikiwa ni moja ya hatua muhimu inayochukuliwa na kampuni hiyo kuzuia ajali nyingi zinazosababishwa na madereva wanaoendesha wakiwa wametumia vilevi
Kampeni hiyo inayobeba ujumbe wa, “Usitumie Kilevi na Kuendesha Chombo cha Moto’ imezinduliwa jijini  Mwanza leo na ilianza na kongamano lililojadili unywaji wa kistaarabu ambalo liliwaleta pamoja wadau kama vile Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani, Mamlakka ya Usafirishaji wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA), madereva, abiria, na wadau wengine katika sekta ya usafirishaji
Akiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika katika hoteli ya Gold Crest, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani (RTO) mkoani Mwanza Mkaddam Hamis Mkaddam, alisema kwa kulishirikisha jeshi la Polisi kampuni ya SBL imeiunga mkono serikali katika kuelimisha umma juu ya unywaji wa kistaarabu na kusisitiza umuhimu wa kutatua tatizo hilo.
Mkaddam alisema baadhi ya watu na haswa madereva hunywa kiasi kikubwa cha pombe pasipo kujali madhara yanayoweza kusababishwa na kitendo hicho na kuonya kuwa vitendo vya aina hiyo vinaweza kusababisha ajali mbaya.
“Sote tunafahamu kuwa matumizi ya vileo yana uhusiano mkubwa na uendeshaji mmbovu ambao unaweza husababisha ajali mbaya za barabarani zenye athari kubwa kwa jamii zetu. Athari zake siyo tu zinawagusa watumiaji wa vilevi bali hata maisha ya wengine na kusababisha upotevu wa maisha na ulemavu kwa watu ambao wangeweza kuchangia uchumi wa nchi,” alisema Mkaddam.
Alisema pamoja na kusababisha vifo visivyotarajiwa na majeraha, unywaji usiokuwa wa kistaarabu una maadhara makubwa kwenye sekta ya afya kwa kuwa kiasi kikubwa cha fedha kinatumika kwa ajili ya huduma, madawa na vifaa tiba kwa waathirika wa ajali za barabarani na hivyo kuwa ni mzigo kwa Serikali.
“Ajali hizi pia ni mzigo kwa vyombo vyetu vya utekelezaji wa sheria kwa kuwa maofisa wanalazimika kuzishughulikia wakati zinaweza kuzuilika ambazo zinasabishwa na madereva wanaondesha wakiwa wametumia vilevi,” Mkaddam aliongeza.
Akizungumzia namna kampeni hiyo itaisadia jamii, mkuu huyo wa usalama barabarani alisema, “sote kwa pamoja ikiwamo sisi polisi, madereva, jamii na wadau wengine tuna jumuku la kutafuta suluhisho la kumaliza tatizo la kutumia vilevi na kuendesha vyombo vya moto. Ninayo furaha kuona SBL pamoja na kwamba biashara yao ni kuuza vilevi, wameona wanawajibu wa kuhimiza unywaji wa kistarabu”.
Kampeni hii inalenga kuwafikia vijana na watu wengine na kuwaeliisha juu ya madhara ya unywaji usiokuwa wa kistaarabu huku ikiwataka kubadili tabia kwa manufaa yao na jamii kwa ujumla
Akiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL John Wanyancha alisema kampeni ya unywaji wea kistaarabu inalenga kuielimisha jamii kuwa wanywaji wanapaswa kunywa kwa kiasi na kuhakikisha unywaji wao hauna madhara kwao na kwa watu wanaowazunguka.
“SBL imedhamiria kuungana na serikali na wadau wengine kuhakikisha kuwa jamii na haswa madereva ambao wanakunywa na kuendesha vyombo vya moto wanaelimishwa juu ya madhara ya vitendo hivyo na kutakiwa kubadilisha tabia,” alisema Wanyancha.

Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wzee Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe. Maudline Castico Azindua Mradi wa Ufugaji wa Kuku Zanzibar.

$
0
0
Na Mwashungi Tahir. Maelezo - Zanzibar.
Makamo wa Pili wa Raisi wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  amewataka Vijana kutumia fursa zinazotolewa na Serikali ili waweze kufaidika kwa kupata ajira na kujiongzea kipato cha kuweza kuendesha maisha yao ya kil;a siku.
Alisema Ilani ya Chama cha Mapinduzi inataka kuwezeshwa wananchi kiuchumi ikiwemo vijana ili waweze kujiletea maendeleo.
Akizungumza kwa niaba yake Waziri wa Kazi,Uwezeshaji wanawake na Watoto Maudline Cyrus Castico huko kwenye uwanja wa Mapinduzi Square Kisonge katika uzinduzi wa mradi wa Uwezeshaji Ajira na kujiongezea kipato kwa vijana kupitia ufugaji wa kuku.
Aidha alisema mradi huo umeanzishwa na Mkuu  wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud  kwa lengo la kupunguza umasikini kwa vijana na kupata kujishughulisha na miradi ili kujiepusha na kuepukana na mambo maovu ambayo yatawaharibia mustakbali wa dira  ya maisha yao.
Amewataka vijana hao kuitumia fursa hiyo ili waweze kufaidika kwa kupata ajira  itakayoweza kuwaongezea kipato katika maisha  yao ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi katika kuitumikia wananchi wake na kuwaletea maendeleo.
“Nataka vijana muichangamkie fursa zinazotoka serikalini kupitia katika Wizara ya Kazi Uwezeshaji Wanawake na Watoto kwa lengo la kuwaletea maendeleo mazuri katika maisha yenu”, alisema Waziri Castico.
Pia alisema anampongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein kwa jinsi anavyowatilia mkazo vijana kwa kuwapatia fursa mbali mbali ili waweze kujikwamua kimaisha wao pamoja na familia zao.
Hivyo aliwaomba vijana hao kuzidisha mashirikiano katika mradi huo kutumia fursa hiyo kwa wale waliopata elimu waweze kuwa walimu kwa  wenzao na kuwapatia elimu hiyo ya ufugaji kuku ili na wao waweze kutumia fursa hizo watazoelekezwa .
Vile vile aliipongeza asasi ya mimi na wewe kwa hatua wanazochukuwa kwa kuimarisha wananchi wake wakiwemo vijana kwa kuwawezesha kiuchumi na kimaendeleo katika Mkoa huo .
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud ambae pia ni Mlezi wa Mradi huo alisema dhamira kubwa ya kuwakusanya vijana kuwa pahala pamoja na kuwawezesha ni kutaka kujikwamua kimaisha kwa kuwaanzishia miradi mbali mbali ikiwemo ya ufugaji wa kuku.
Pia alisema kufanya hivyo tunakusudia kupunguza umasikini kwa vijana ambao wao ndio tegemeo la kesho katika utendaji wa kazi zao za kujiongeze kipato.
Akisoma risala katika uzinduzi huo Msimamizi wa Mradi wa Ufugaji kuku Rashid Muhammed Othmani alisema amempongeza Mkuu huyo wa Mkoa kwa kuazisha Mradi huo ambao utawezesha kuwakwamua na tatizo la umasikini lililodumu kwa muda mrefu kwa vijana na kuwaomba viongozi wengine kuiga mfano kama huo.
Hata hivyo amesema juhudi anazozichukua katika kuwakwamua vijana kumewawezesha vijana kujikwamua kiuchumi jambo ambalo litawaweka katika mazingira rafiki na kuwa wazalendo , wapenda amani  na kuilinda nchi yao.
Aidha alisema juhudi hizo zinazochukuliwa  zinawanufaisha vijana walio  wengi na kusababisha kuachana na vitendo vilivyo viovu na kuweza kufuata miongozo na maadili  ya  mambo yaliyo mema na kupelekea Taifa kusonga mbele kwa kuwa na vijana waliyo madhubuti.
Mradi huo wa ufugaji wa kuku aina ya Saso unasimamiwa na kampuni ya Silverland kutoka Iringa na umewapa mafunzo vijana kumi na mbili  na kuifikisha walimu kwa vijana wenzao wafikao 300 na tayari  wanavifaranga vya kuku mia tisa na hamsini 9,500 katika kituo cha malezi ya vifaranga vya kuku huko Mwachealale shehia ya Mbaleni Wilaya ya Kaskazini B.

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Afungua Mkutano wa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara.

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Waziri wa Madini, Dotto Biteko, wakati akiwasili kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma Januari 26, 2019, kufungua mkutano wa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Binilith Mahenge, wakati akiwasili kwenye mkutano wa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara, katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, katikati ni Waziri wa Madini, Dotto Biteko
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara, wakati akifungua mkutano kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma
Wakuu wa Mikoa wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati akiwahutubia kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, 
Wakuu wa Mikoa wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati akiwahutubia kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiteta jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jafo, kabla ya kufungua mkutano wa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara, uliofanyika katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka, mara baada ya kufungua mkutano wa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara, katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma. Katikati ni Waziri wa Madini, Doto Biteko
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Constantine Kanyasu (kulia), akimsikiliza  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, baada ya kufungua mkutano wa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara jijini Dodoma Januari 26, 2019. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, baada ya kufungua mkutano wa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara, nje ya  ukumbi wa Hazina jijini Dodoma Januari 26, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)




Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Constantine Kanyasu (kulia), akimsikiliza  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, baada ya kufungua mkutano wa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara jijini Dodoma Januari 26, 2019. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waumini wa Dini ya Kiislam Watakiwa Kuelewa Msikiti ni Nyumba ya Mwenyenzi Mungu.Inayowakutanisha Kuteleleza Dini.

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana Sheikh Abdullah Talib alipofika Maungani Wilaya ya Magharibi “B” kuufungua Msikiti Salama { Masjid Salama } wa Kijiji hicho.Kulia ya Sheikh Talib ni Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikha Fadhil Suleiman Soraga.

Mjumbe wa Kamati ya Msikiti Salama wa Maungani Dr. Ali Uki akisoma Risala kwenye hafla ya Ufunguzi rasmi wa Masjil Salama Maungani Wilaya ya Magharibi “B”.
Waumini wa Dini ya Kiislamu wakimsikiliza  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hayupo pichani wakati akiufungua rasmi Msikiti Salama wa Maungani.

Waumini wa Dini ya Kiislamu wakimsikiliza  Sheikh Khalid Ali Mfaume kutoka Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar hayupo pichani wakati akitoa risala ya umuhimu wa msikiti katika Uislamu. Picha na – OMPR – ZNZ.
Na.Othman Khamis.OMPR. 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewakumbusha Waumini wa Dini ya Kiisalamu kuelewa kwamba Msikiti ni nyumba ya Mwenyezi Mungu inayowakutanisha kutekeleza Nguzo ya Pili ya Dini hiyo inayojumuisha pamoja na mambo mengine Ibada ya sala, Elimu, Maarifa  pamoja na Malezi kwa Watoto.
Alisema katika kutekeleza hayo Waumini hao wanapaswa kuwa madhubuti katika kuilinda Misikiti  kutokana na madarasa ya uchochezi yaliyoibuka katika baadhi ya sshemu Nchini ambayo huwa na muelekeo wa kuwagawa Waumini Kibadhehebu au Kisiasa.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa kumbusho hilo wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Msikiti Salama { Masjid Salama } uliojengwa kwa nguvu za Waumini wenyewe wa Dini ya Kiislamu pamoja na misaada ya Wahinsani katika Mtaa wa Maungani Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa Mjini Magharibi.
Alisema Jamii imekuwa ikishuhudia ongezeko kubwa la dhulma na mmong’onyoko wa Maadili unaochangiwa na vitendo vya Ubakaji, Ulawiti, udhalilishaji wa Watoto Wadogo, Utumiaji wa Dawa za Kulevya kwa kiwango cha kutisha mambo yanayosababishwa na upungufu wa Maadili yanayopaswa kutiliwa mkazo hasa kwenye madarasa Misikitini.
Balozi Seif aliwaomba Waumini na Wananchi wote Nchini kuendelea kushirikiana kwa pamoja katika kuondosha maasi hayo yaliyokithiri na kutishia Imani za waja ambayo tayari yameshakemewa na Kiongozi wa Dini ya Kiislamu Mtume Muhammad {SAW}.
“ Masheikh wetu wajitahidi kuielimisha Jamii juu ya athari ambazo Mja anaweza kuzipata kwa kuendeleza vitendo viovu”. Alisema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Alieleza kwamba Msikiti ni Nyumba isiyo na mbadala kutokana na utukufu wake. Hivyo aliwanasihi  Wana Maungani kutumia Mali na nguvu zao zote katika kuutunza ili ubakie Mpya, wakupendeza ili uendelee kuhudumia kazi ya mola ya kuabudiwa na Viumbe vyake.
Balozi Seif alisema zipo Hadithi zinazohimiza juu ya wajibu wa kuishughulikia Misikiti na kuitumikia ili wale waliokuwa mstari wa mbele  kwa jambo hilo wazidi kuongeza harakati na wale waliowazito kutoa mali zao washajiike kutoa msukumo huo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema Mwenyezi Mungu ameamrisha Waja wake kutoa sehemu ya Mali zao ili ziwanufaishe wengine katika Jamii na kuahidi kuwalipa Waja hao watakaotoa kwa ajili ya fisabili – llahi.
Alisema kwa bahati mbaya wapo Waumini wachache miongoni mwao wanaoelewa umuhimu wa kutoa mali zao kwa ajili ya kumtakasa Mwenyezi Muungu katika maamrisho aliyowaelekeza waja wake kumtakasa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza Waumini wa Maungani pamoja na maeneo jirani waliotoa wazo na kuanza kufikiria ujenzi wa Jengo hilo la Ibada wazo lililopokewa na Muumini aliyejitolea kutumia mali zake kumaliza ujenzi wa Msikiti huo.
“ Ye yote anayekufanyieni mambo mema, basi mlipeni na mtakapokosa cha kumlipa basi muombeeni dua kwa Mwenyezi Mungu”. Balozi Seif alisisitiza hilo wakati akikariri Maneno ya Nabii Muhammad {SAW}.
Akisoma Risala kwa niaba ya Wamini wa Dini ya Kiislamu wa Masjid Salama Dr. Ali Uki alisema baadhi ya  Waumini wa Kijiji cha Maungani walilazimika kufanya Ibada zao ndani ya Majumba yao hasa kwa ile Sala ya Alfajiri kutokana na umbani wa Msikiti uliopo kwenye eneo hilo kwa kuhofia kiza kilichotanda katika eneo hilo.
Dr. Uki alisema usumbufu huo uliwapa fikra iliyozaa maarifa ya kuanza ujenzi wa Jengo lao la Ibada ili kuondokana na kadhia hiyo iliyopelekea jitihada zao kuzaa matunda ya kuanza ujenzi ndani ya kipindi cha Miaka Mitano iliyoanzia Mwezi Mei Mwaka 2014.
Alisema Ujenzi huo ulioanzishwa kwa nguvu za Waumini wenyewe ulipata baraka za kuunga mkono na Taasisi moja ya Kiserikali iliyojitolea kusaidia Mabati 100 pamoja na Waumini wawili wa Dini ya Kiislamu Mume na Mkewe mwenye asili ya Zanzibar wanaoishishi Nchini Oman.
Dr. Uki aliiambia hadhara hiyo iliyohudhuria ufunguzi wa Masjid Salama kwamba harakati za ibada ya sala zilianza Rasmi mnamo Tarehe 29, Januari Mwaka 2018 wakati jengo hilo tayari limeshapata usajili Mwezi Juni Mwaka 2016 kutoka Taasisi husika na masuala ya Kiislamu Nchini.
Alifahamisha kwamba wakati Msikiti huo ukifanikiwa kuwa na uwezo wa kusaliwa na Waumi ni wapatao 250 kwa wakati Mmoja umejengwa kwa Gharama inayokadiriwa kufikia zaidi ya Shilingi za Kitanzania Milioni 200,000,000/- .
Dr. Uki alisema Jengo hilo la Ibada  lina Sehemu za kusaliwa kwa Wanaume, Wanawake, Madrasa sambamba na Sehemu Maalum ya kuoshea Maiti pale inapotokezea Fardhi ndani ya Mtaa huo uliopo Magharibi mwa Mji wa Zanzibar.
Mjumbe huyo wa Kamati ya Msikiti Salama aliwaomba radhi kwa niaba ya wenzake baadhi ya Mafundi kwa hitilafu zilizojitokeza wakati wa Ujenzi wa Msikiti huo ambapo Kamati ya usimamizi ililazimika kuwa kali ili ujenzi huo ufikie kiwango kinachokubalika.
Akitoa Mawaidha kuhusu umuhimu wa Msikiti Sheikh Khalid Ali Mfaume kutoka Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar alisema kuimarisha Msikiti maana yake Waumini wasali sala Tano na kwa wakati wake mahsusi.
Sheikh Khalid alisema kazi hiyo inakwenda sambamba na kazi ya Mwenyezi Muungu Mola wa Viumbe vyote aliyeumba Mbingu na Ardhi anayeshusha utulivu kwa  Waumini wanaoamini kubakia Msikitini baada ya Sala wakisoma Quran na kufundishana maamrisho yake.

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Yazindua Mafunzo ya Kuwajengea Uwezo Walimu wa Sayansi na Kiingereza Madarasa ya Tano na Sita Zanzibar.

$
0
0
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mmanga Mjengo Mjawiri akizungumza na walimu, Maafisa Elimu na Wakurugenzi wa Halmashauri katika uzinduzi wa Mradi wa Mafunzo ya kutoa msaada kwa wanafunzi wa Skuli za Msingi (TESS) katika Kempasi ya SUZA Nkrumah
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Maalim Abdulla Mzee akiwaeleza walimu wa Skuli za Sekondari walioshiriki uzinduzi wa Mradi wa Mafunzo ya kutoa msaada kwa wanafunzi wa Skuli za Msingi (TESS) katika Kempasi ya SUZA Nkrumah.
Baadhi ya Walimu, Maafisa Elimu na Wakurugenzi wa Halmashauri walioshiriki Mafunzo ya kutoa msaada kwa wanafunzi wa Skuli za Msingi (TESS) wakifuatilia uzinduzi wa Mradi huo katika Kempasi ya SUZA Nkrumah.
Picha ya pamoja ya Naibu Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Amali Mmanga Mjengo Mjawiri na baadhi ya washiriki wa mafunzo ya kutoa msaada kwa wanafunzi wa Skuli za Msingi (TESS) katika Kempasi ya SUZA Nkrumah.

Na Ramadhani Ali   -Maelezo -Zanzibar.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mmanga Mjengo Mjawiri amesema ili kupata matokeo mazuri ya wanafunzi katika mitihani ya elimu ya juu na vyuo, juhudi kubwa inahitajika katika kuimarisha elimu ya maandalizi na msingi.

Amesema Maafisa Elimu na Walimu wakuu wa skuli za msingi wanapaswa kuwa wasimamizi na wafuatiliaji wa karibu wa kazi za kila siku za walimu wao ili malengo yaliyowekwa ya elimu yaweze kufikiwa. 

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali alieleza hayo alipokuwa akizindua Mradi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Walimu wa masomo ya Sayansi, Kiingereza na Hesabu wa darasa la tano na sita wa skuli za Unguja ili waweze kutoa msaada kwa wanafunzi na kuongeza ufaulu wao.

Alisema imebainika kuwa pamoja na juhudi zinazochukuliwa za kuwapatia walimu mafunzo ya mara kwa mara suala la ufuatiliaji na ufuatiliaji limekuwa ni tatizo kubwa kwa skuli nyingi za Zanzibar.

Aliweka wazi kuwa msimamo wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kuwa kuanzia sasa inataka kuona mafunzo yanayotolewa kwa walimu wa skuli yanaleta mabadiliko na kuongeza ufanisi  katika skuli zao 

Aliwataka walimu wakuu kuwa wabunifu katika kuongoza na kushirikiana na Maafisa Elimu na viongozi wa Halmashauri, hasa wakati huu wa wa ugatuzi, kubuni mbinu mpya za kuendeleza mbele skuli zao
.
 Aidha aliwataka walimu wakuu kujitambua na kuthamini nafasi waliyopata huku wakijenga upendo kwa walimu, wanafunzi na kujiepusha kufanya makosa ambayo yanaweza kuwavunjia heshma mbele ya jamii.

Akizungumza katika uzinduzi wa Mradi huo katika Kempasi ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar Kempasi ya Nkrumah, Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo ya Walimu Maimuna Fadhil Abass alisema kwa vile  elimu ya msingi imeingizwa katika ugatuzi, viongozi wa Wilaya wanatakiwa kuipokea na kuifanyia kazi huku Wizara ya elimu ikiendelea na wajibu wa kusimamia sera.

Akimkaribisha Naibu Waziri kuzindua Mradi huo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Maalim Abdulla Mzee alisema zipo baadhi ya skuli zinawalimu wazuri lakini zimeshindwa kutoa mwanafunzi hata mmoja kwenda michepuo jambo linaloashiria uwajibika mdogo kwa skuli hizo.

Alisema lengo la Wizara ya Elimu ni kuona kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa michepuo kinaongeza kila mwaka na wameandaa zawadi maalum  kwa skuli itakayo ongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wao kwa kila mwaka.

Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mhe. Constantine Kanyasu Awahamasisha Wabunge Kutembelea Vivutio Vya Utalii.

$
0
0
Mwenyektiti w Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, ,Maliasili na Utalii, Nape Nnauye akiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati  hiyo  akiwaonesha kundi la tembo mara baada ya kamati hiyo kufanya utalii nyakati za jioni mwishoni mwa wiki  wakati Kamati hiyo ilipomaliza kufanya  kikao cha kujadili mradi  wa kukuza na kuendeleza utalii Kusini katika Hifadhi ya taifa ya Ruaha  koani Iringa.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Maliasili na Utalii, Neema Mgaya akiwa ameongoza na Mwenyekiti wa Kamati nhiyo, Nape Nnajuye pamoja na wajumbe wengine wakitelemka katika eneo la kuonea wanyama aina ya viboko  nyakati za jioni wanapokunywa maji mto wa Ruaha Mkuu katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha mkoani Iringa mwisho ni wa wiki wakati kamati hiyo ilipofanya utalii wakati Kamati hiyo ilipomaliza kikao cha kujadili mradi  wa kukuza na kuendeleza utalii Kusini. 
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Maliasili na Utalii, Mwita Getere akiwa ameongozana  na wajumbe wengine wakipanda ngazi juu ya sehemu ya  kuonea wanyama aina ya viboko  nyakati za jioni wanapokunywa maji mto wa Ruaha Mkuu katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha mkoani Iringa mwisho ni wa wiki wakati kamati hiyo ilipofanya utalii wakati Kamati hiyo ilipomaliza kikao cha kujadili mradi  wa kukuza na kuendeleza utalii Kusini.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Constantine Kanyasu (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja  kwenye jabali ambalo watalii hupanda katika jiwe hilo kwa ajili ya kuona makundi ya wanyama aina ya kiboko wakiwa wanakunywa maji katika mto wa Ruaha Mkuu katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha mkoani Iringa mwisho ni wa wiki wakati kamati hiyo ilipofanya utalii wakati Kamati hiyo ilipomaliza kikao cha kujadili mradi  wa kukuza na kuendeleza utalii Kusini.(Picha na Lusungu Helela-MNRT)


Na.Lusungu Helela - Arusha.- IRINGA
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu amewataka Wabunge wa  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa chachu ya kuhamasisha utalii wa ndani kwa wananchi wanawaongoza  kwa kutenga muda wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Imeelezwa kuwa hamasa ya wananchi ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini imekuwa na mwitikio mdogo ukilinganisha na idadi ya watalii wa kutoka nje.

Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu akiwa na  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara ya siku mbili ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa mradi wa kukuza na kuendeleza utalii Kusini katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha mkoani Iringa.

Amesema endapo kila Mbunge kwa nafasi yake ataweza kuhamasisha wananchi kutembelea vivutio vya utalii mapato yataweza kuongeza maradufu kupitia Utalii wa ndani tofauti na ilivyo sasa.

"Tengeni muda wa kupumzika baada ya pilikapilika ya kuwahudumia wapiga kura wenu, unakuja huku Ruaha unapumzisha akili huku ukijipanga  mwaka 2020 kwa ajili ya uchaguzi Mkuu" alisema.

" Tusisubiri tuje kikazi kama tulivyokuja hivi, Panga njoo na familia yako ufurahie maisha mara moja moja sio mbaya" Alisisitiza Kanyasu.

Pia, Kanyasu aliwaomba Wabunge hao  kila wanapopata nafasi ya kukutana na wananchi majimboni mwao wawahamasishe kutembelea vivutio vya utalii ili kumuunga mkono Rais John Magufuli kwa jitihada anazofanya za kutaka kuongeza mapato yatokanayo na sekta ya utalii.

Amesema ufufuaji wa kampuni la usafiri wa ndege nchini (ATCL) kwa kununua ndege saba achilia mbali mradi wa reli ya Standard Garge ni juhudi wazi za  Rais John Magufuli kuona sekta ya utalii inagusa maisha ya kila wananchi kimapato.

Katika hatua nyingine, Kanyasu aliwaomba Wabunge hao wawahamasishe wananchi kuchangamkia fursa za utalii kwa kujenga Hoteli au kwa kuanzishavituo vya  utalii wa kiutamaduni ambao umekuwa ukipendwa sana na watalii wengi wa kutoka nje.

Aidha, Mhe.Kanyasu aliwaeleza Wabunge hao kuwa baada ya kufungua utalii Kusini, Serikali inakusudia kufungua utalii katika kanda nyingine ikiwemo ya kanda ya  ziwa na kanda ya Kaskazini Magharibi, Hivyo wawaandae wananchi wao kuchangamkia fursa za utalii badala ya kubaki walalamikaji.

Kwa upande wake, Mbunge wa Mtama ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Nape Nnauye alisema kufunguliwa mapema kwa utalii Kusini kutatoa picha halisi kwa wananchi katika kunufaika kiuchumi kupitia sekta hiyo katika kanda nyingine

Pia, Mhe, Nape aliishauri Serikali kulifanyia kazi suala la  tozo ya kuingia ndani ya hifadhi (single entry) kutokana na  malalamiko ya muda mrefu wanayoyatoa wananchi kwanaoishi Katibu na Hifadhi kuwa imekuwa ikiwabana watalii kutoka nje ya Hifadhi kuwatembelea wananchi hao.

Madrasatul Tarbiyyatul Islamiyya Limbani Wete Kisiwani Pemba. Yaadhimisha Sherehe za Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad SAW .

$
0
0
MLEZI wa Almadrasat Tarbiyyatul Islamiyya ya Limbani Wete bi Mauwa Abeid Daftari akiwa na wanawake wa kiislamu katika maulidi ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (SAW) huko Limbani Wete.
MKURUGENZI wa green light foundation Salim Mussa Omar (wa pili kulia) akiwaongoza waislamu katika mauled ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (SAW) katika chuo cha almadrasat Tarbiyya Islamiyya ya Limbani Wete
WANAFUNZI wa Almadrasat Tarbiyyatul Islamiyya ya Limbani Wete wakitumbuiza katika mauled ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (SAW)  katika chuo hicho huko limbani Wete  

MKURUGENZI wa Green Light Foundation Zanzibar Ndg.Salim Mussa Omar, akizungumza na kutowa nasaha zake kwa Wanafunzi wa Madrasatul Tarbiyya Islamiyya ya Limbani Wete Pemba wakati wa hafla ya Maulidi ya kuzaliwa Mtume Muhammad SAW, yaliofanyika katika Madrasa hiyo Wete Pemba.
(Picha na Said Abdulrahman - Pemba).

India Yaadhimisha Miaka 70 ya Siku ya Jamuhuri ya India Katika Ubalozi Mdogo wa India Migombani Zanzibar.

$
0
0
Balozi Mdogo wa India anayefanyia Kazi zake Zanzibar. Mhe. T.C.Barupal, akipandisha Bendera katiika Viwanja vya Ofisi Ndogo ya Ubalozi wa India Migombani Zanzibar,kuadhimisha Miaka 70 ya Siku ya Jamuhuri ya India, hafla hiyo imefanyika katika Ubalozi huo na kuhudhuriwa na Wananchi Wenye Asili ya India na Raia wa India waliopo Zanzibar. 
Balozi Mdogo wa India anayefanyia Kazi zake Zanzibar Mhe. T.C.Barupal, akihutubia na kutoa salamu za Wananchi wa India wakati wa hafla hiyo ya kuadhimisha Miaka 70 ya Jamuhuri ya India, zilifanyika katika viwanja vya Ubalozi Migombani Zanzibar. na kuhudhuriwa na Wananchi wenye Asili ya India. 
Wananchi wenye Asili ya India wakifuatilia hafla hiyo ya kuadhimisha sherehe za Miaka 70 ya Jamuhuri ya Watu wa India, zilizofanyika katika viwanja vya Ubalozi Mdogo wa India Migombani Zanzibar.
Wananchi wenye Asili ya India wakifuatilia hafla hiyo ya kuadhimisha sherehe za Miaka 70 ya Jamuhuri ya Watu wa India, zilizofanyika katika viwanja vya Ubalozi Mdogo wa India Migombani Zanzibar.
 BALOZI Mdogo  wa India aliepo Zanzibar, T.C. Barupal akisalimiana na Raia wa nchi hiyo pamoja na Wazanzibari wenye asili ya India wakati wa hafla ya sherehe za miaka 70 ya siku ya Jamhuri ya India zilizofanyika katika Ubalozi huo uliopo Migombani mjini Unguja jana.(

BALOZI Mdogo wa India aliepo Zanzibar, T.C. Barupal akisalimiana na Raia wa nchi hiyo pamoja na Wazanzibari wenye asili ya India wakati wa hafla ya sherehe za miaka 70 ya siku ya Jamhuri ya  India zilizofanyika katika Ubalozi huo uliopo Migombani mjini Unguja jana.(PICHA NA HAROUB HUSSEIN).

Mradi wa Usambazaji wa Mabomba ya Maji Safi na Salama Zanzibar Ukiendelea Kwa Kasisi.

$
0
0
Wafanyakazi wa Kampuni ya Kichina ya STECOL Inayosambaza  mabomba ya Maji Safi na Salama katika Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, wakiendelea na uwekaji wa mabomba hayo mapya katika maeneo mbali mbali katika Mji wa Unguja. Kama walivyokutwa na Kamera yetu wakiwa katika mitaa ya maruhubi wakiweka mabomba hayo kuelekea bububu. kama wanavyoonekana pichani.



Maadhimisho ya Siku ya Sheria Duniani Kuadhimishwa Kisiwani Pemba

$
0
0
Mrajis wa Mahakama Kuu Zanzibar Mhe.Mohammed Ali Mohammed, akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Kisiwani Pemba kuhusiana na kukamulika kwa maandalizi Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Sheria Duniani, inayotarajiwa kuadhimishwa Kisiwani Pemba, Kitaifa mwaka huu..
Baadhi ya Watendaji wa Mahakama Chake Chake, wakiwa katika mkutano maalumu wa Mrajis wa Mahakama kuu Zanzibar , Mohammed Ali Mohammed, na Waandishi wa habari Kisiwani Pemba , juu ya maandalizi ya sherehe ya siku ya sheria Duniani inayotarajiwa kufanyika Kisiwani Pemba kwa Zanzibar.
Baadhi ya Waandishi wa habari wa Vyombo mbali mbali Kisiwani Pemba, wakimsikiliza kwa makini Mrajis wa Mahakama kuu Zanzibar.Mhe.Mohammed Ali Mohammed , juu ya maandalizi ya siku ya Sheria Duniani inayotarajiwa kufanyika Kisiwani Pemba sambamba na maonesho ya Shughuli za Mahakama.
Picha na Hanifa Salim -Pemba.

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Azungumza na Viongozi wa CWT Taifa.

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Taifa, ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Januari 25, 2019. Kutoka kushoto ni Makamu wa Rais , Deus Seif, Mweka Hazina , Abubakar Allawi, Katibu Mkuu, Christopher Banda na Wapili kulia ni  Rais wa CWT , Leah Ulaya.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, Azindua Mradi wa Maji Safi na Salama Skuli ya Msingi Mangapwani Unguja.

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizindua Rasmi Mradi wa Huduma ya Maji safi na salama uliopo Skuli ya Msingi Mangapwani utaosambaza pia katika Vijiji Jirani vinavyoizunguuka Skuli hiyo.
Balozi Seif akitoa onyo kwa Mtendaji ye yote wa Halmashauri ya Wilaya atakayebainika kuzorotesha uendelezaji wa Miradi ya Wananchi ndani ya Majimbo.
Balozi Seif  akikemea ucheleweshwaji wa Mradi wa Maji safi katika Kijiji cha Mangapwani uliofanywa na Mhandisi wa Mradi huo unaotekelezwa kupitia Fedha za Mfuko wa Mbunge wa Jimbo la Mahonda.
Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balaozi Seif akikagua maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Skuli ya Msingi ya Kiomba Mvua unafanywa na Wananchi wenyewe.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Na.Othman Khamis OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameonya kwamba Serikali haitosita kumuwajibisha na hata kumpelekea Mahakamani Mtendaji ye yote wa Halmashauri ya Wilaya atakayebainika kuhusika na ubabaishaji wa matumizi ya Fedha za Mfuko wa Jimbo zinazotengwa kwa ajili ya kuendeleza Miradi ya Wananchi.
Alisema zipo hitilafu zinazojitokeza kuzorotesha uendelezaji wa Miradi ya Wananchi Majimboni ambazo husababishwa na baadhi ya Watendaji wa Halmashauri za Wilaya zikionyesha kuzunguukwa na mazingira ya utapeli hasa katika matumizi ya Fedha.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa onyo hilo wakati alipozindua Rasmi Mradi wa Maji safi na salama katika Skuli ya Msingi Mangapwani ambao pia utasaidia kusambaza huduma hiyo katika vijiji jirani vinavyoizunguuka Skuli hiyo.
Alisema wapo baadhi ya Watendaji ndani ya Halmashauri za Wilaya wakionyesha udhaifu wa kuzorotesha Miradi ya Wananchi waliyoianzisha ilhali fedha zinazotengwa kuitekeleza Miradi hiyo huwa tayari zimeshaidhinishwa na kutiwa saini na Viongozi wanaouhusika.
Balozi Seif alisema kuanzia sasa atalazimika kufuatilia changamoto zote anazowasilishiwa zinazohusiana na kadhia hiyo na hatosita kumchukulia hatua za kinidhamu mtendaji atakayebainika kuhusika na hadaa yoyote hasa ile inayohusiana na masuala ya Fedha.
Aliwataka Wananchi wa Mangapwani kutoa taarifa mapema pale yanapojitokeza matatizo ya kiufundi katika uendeshaji wa Mradi huo wa Maji safi na salama na kuacha tabia ya kuwatumia Mafundi wa vichochoroni wanaoweza kuleta athari zaidi ya kiufundi kwenye mradi huo muhimu kwa ustawi wa Jamii.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza na kuwashukuru Wananchi wa Vijiji vya Mangapwani, Kiomba Mvua, Vuga Mkadini na Matetema kwa jitihada zao za kujisogezea huduma mbali mbali za Kijamii na Maendeleo kwenye maeneo yao.
Katika ziara hiyo Balozi Seif akiwa pia Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda alipata wasaa wa kukagua Mradi wa Kisima cha Maji safi kilichochimbwa kupitia Fedha za Mfuko wa Mbunge hapo Mangapwani, Jengo linalotarajiwa kuwa Skuli ya Msingi la Kiomba Mvua, Jengo la Skuli ya Msingi Vuga Mkadini pamoja na Mradi wa Umeme uliopo katika Kijiji cha Matetema.

Mfuko wa Khalifa Fund Kuwawezesha Vijana wa Zanzibar Katika Kupata Utaalam na Masuala ya Kiufundi Ili Kuweza Kujiajiri.

$
0
0

Mkurugenzi wa Mfuko wa Khalifa Fund, wenye Makao Makuu ya Nchini Abu Dhabi UAE.Ndg. Nizar Cheniour, akizungumza na Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar,kwa ziara ya Siku Tatu Nchini Zanzibar.

MKURUGENZI wa Mfuko wa ‘KhalifaFund’ Naizar Cheniour, amesema mfuko huo umeazimia  kuwawezesha vijana wa Zanzibar katika nyanja mbali mbali za kiuchumi ili kuweza kujiajiri na kuinua hali zao za maisha.

Mkurugenzi huyo amesema hayo leo wakati  alipozungumza na waandishi wa habari, mara baada ya ujumbe wa Mfuko huo ulipowasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.

Ujumbe huo upo nchini kwa ziara maalum, ikiwa ni muendelezo wa mazungumzo na Serikali, yenye lengo la kufanikisha utekelezaji wa programu mbali mbali katika sekta za biashara, ujasiriamali, miundombinu na nyenginezo.

Alisema Mfuko umelenga kuwawezesha vijana wa Zanzibar katika upatikanaji wa rasilimali fedha, utaalamu na masuala ya kiufundi ili waweze kujiajiri kupitia shughuli za ujasiriamali na hivyo kuweza kujitegemea.

Aliwataka vijana na Wazanzibari kwa ujumla kutarajia mafinikio makubwa kutokana na  program mbali mbali zitakazotekelezwa kupitia Mfuko huo.

Alisema mfuko wa KhalifaFund, una uzoefu mkubwa katika utekelezaji wa programu za maendeleo na shughuli za kiuchumi, ambapo umekuwa ukifanya kazi hizo katika nchi mbali mbakli duniani.

Mapema, Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Viwanda,Ndg.Juma Ali Juma alisema ujio wa Viongozi wa Mfuko wa’ KhalifaFund’  umelenga kukamilisha mazungumzo yaliofikiwa katika kikao kilichopita ili kuwa tayari kwa utekelezaji wa yale yalioafikiwa.

Alisema mfuko huo wa kifedha, wenye makao makuu yake Abu Dhabi ,UAE utatowa msukumo mkubwa  katika utekelezaji wa program mbali mbali za kimaendeleo na kiuchumi, sambamba na kuwawazesha vijana kupitia kazi za ujasiriamali.

Alisema wakati ukiwa nchini utakutana na kufanya mazungumzo na taasisi mbali mbali za Serikali pamoja na kutembelea maeneo tofauti.

Hii ni mara ya pili kwa viongozi wa Mfuko wa ‘KhalifaFund’ kuja nchini kwa ajili hiyo, ambapo kabla ulipata fursa ya kutembelea sekta tofauti za maendeleo na kiuchumi Unguja na Pemba.

Aidha, ujio wa mfuko huo unafutia ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein aliyoifanya Umoja wa nchi za Falme ya Kiarabu (UAE) Januari mwaka uliopita. 

Abdi Shamnah, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777476982. Fax: 024 2231822 
 E-mail: abdya062@gmail.com

Ujumbe wa Mfuko w Khalifa Fund wa Abu Dbabi Wawasili Zanzibar Kwa Kutekeleza Programu Mbalimbali za Kimaendeleo na Kuwawezesha Vijana Kupata Kazi za Ujasiriamali.

Ujumbe wa Mfuko wa Khalifa Fund wa Abu Dhabi UAE Watembelea Kikundi cha Ushirika cha Faki Milling Enterproses Kisongoni Zanzibar.

$
0
0

Mkurugenzi wa Ushirika wa Fakirice Milling Enteprises Kisongoni Wilaya Kaskazini B Unguja. Ndg Yussuf Faki Yussuf, akitowa maelezo ya Ushirika wao unaojishughulisha na usagaji wa mazao ya nafaka na mpunga, kwa Ujumbe wa Mfuko wa Khalifa Fund, uliotembelea Ushirika huo kuona maendeleo yake, wakiwa katika ziara yao Zanzibar. 


Ujumbe huo ukiongozwa na viongozi mbali mbali wa Serikali, ulifanya ziara ya kukitembelea kikundi cha ushirika cha ‘Tusizembee Cooperative’ kiliopo Kinaysini Kisongoni kinachojishughulisha na  usagaji wa nafaka (mpunga).

Katibu wa Kikundi hicho Yussuf Faki Yussuf alisema ushirika huo hununuwa mpunga kutoka kwa wakulima na kuusaga na hatimae kuuza katika hoteli na maduka mbali mbali baada ya kufungwa vizuri katika mifuko maalum.

Alisema kwa wastani husambaza tani kumi (10) za mchele kila mwezi katika maduka hayo.

Alisema changamoto kubwa inayokabili ushirika huo ni ukosefu wa mtaji wa kuwezesha kununuwa kiwango  kikubwa cha mpunga kutoka kwa wakulima.

Ujumbe huo uilipata fursa ya kuangalia jinsi mashine hizo za kusaga zinazofanyakazi pamoja na ubora wa mchele unaotolewa..

Viewing all 35828 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>