Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Dk:Shein akemea wafanyabiashara · Awataka waache kutumia vibaya vibali

$
0
0
Na Mwantanga Ame
RAIS wa Zanzibarna Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, amewataka wafanyabiashara kuacha kutumia vibaya vibali wanavyopewa kwa kusafirisha biashara mbaya zinazoitia aibu nchi.

Aliyasema hayo wakati akifungua tamasha la biashara Zanzibar, ikiwa ni sehemu ya kuadhikisha miakia 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliofanyika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar.

Alisema inasikitisha kuona katika siku za hivi karibuni kumekuwepo  taarifa zinazolitia aibu taifa, kutokana  na baadhi ya wafanyabiashara kutumia vibaya vibali wanavyopewa kwa kusafirisha  bidhaa haramu.

Alisema kumekuwa na ongezeko kubwa la watu kukamatwa ndani na nje ya nchi wakijihusisha na zisizoruhusiwa kisheria.

“Napenda kutabanaisha  kuwa vitendo hivyo vinavyofanywa na wafanyabiashara wachache vinaathiri na kuharibu kwa kiasi kikubwa maendeleo ya biashara nchini na kuitia doa nchi yetu pamoja na kujenga mazingira magumu kwa wafanyabiashara wengine na wananchi kwa jumla hasa wanaposafiri nje,” alisema.


Alisema vitendo hivyo vinaiharibia sifa nchi hii, kwani vinaweza kuyafanya mataifa wanayoyatumia kutowaamini pale watapopeleka biashara zao.

Alisema serikali haiwezi kuacha hali hiyo iendelea na itahakikisha inavisimamia vyema vyombo vya ulinzi ili kuwakabili  watu hao kabla ya hawajaondoka nchini.

Alisema nia ya serikali ni kuona wafanyabiashara wanaopewa vibali wanafuata taratibu za kisheria pahali popote.

Alisema serikali imeandaa  mazingira mbali mbali ya kufanya biashara, ili kuwawekea unafuu wananchi, lakini moja ya tatizo kubwa linaloendelea ni kwa baadhi ya watu kushindwa kuwatendea haki wananchi kutokana na kuwaongezea bei.

Alisema hali hiyo inasababisha kuwapo mfumko wa bei unaojitokeza mara kwa mara hasa katika mwezi wa Ramadhani, licha ya serikali kupunguza ushuru kwa baadhi ya bidhaa.

Alisema hali hiyo inachangia kuharibu uhusiano mabaya kati ya wananchi na serikali yao, na ni vyema wafanyabishara wakazingatia maadili mema, uadilifu na sheria ziliopo.

Akizungumzia hali ya biashara nchini, alisema kumekuwa na mabadiliko mwaka hadi mwaka, kwani usafirishaji wa bidhaa umeongezeka kutoka bidhaa zenye thamani ya shilingi 21,177.7 milioni kwa mwaka 2007, na kufikia shilingi 67,390.5 milioni kwa mwaka 2012 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 318.2.

Alisema usafirishaji huo, umeongezeka zaidi katika zao la karafuu na mwani, huku upande wa uagizaji bidhaa zenye thamani ya shilingi 271,273.1 milioni kwa mwaka 2012, kutoka bidhaa zenye thamani ya shilingi 107,689 milioni kwa mwaka 2007 ikiwa ni sawa na asilimia 251.9.


Kutokana na ahali hiyo, alisema ipo haja kwa wazalishaji wa ndani kujitahidi zaidi kuzalisha bidhaa mbali mbali zikiwemo za viungo ili kuyafikia masoko ya nje badala ya kuendelea na utaratibu wa sasa wa kuwa waagiziaji zaidi.

Alisema serikali katika kuandaa mazingira bora ya biashara tayari imefanya mabadiliko mbali mbali ya sheria ikiwemo ya mwaka 1989 na sheria ya leseni  na kuanzisha mfumo wa nambari za utambulisho wa bidhaa ambao ni muhimu kwa ushindani wa masoko ambao tayari unaongezeka duniani.

Alisema kwa vile katika maonyesho hayo kuna ushiriki wa mataifa mbali mbali duniani ni vyema wananchi walioshiriki kuyatangaza maeneo yao ya biashara.

Alisema kazi kubwa wanayotakiwa kuifanya ni wanawapa maelezo sahihi washiriki hao ikiwa ni hatua itakayotanua wigo na ushirikiano huku wakikumbushana  wajibu wa wafanyabiashara kuimarisha uchumi wa nchi.

Alizishukuru baadhi ya nchi zilizojitolea kushiriki maonesho hayo kwani zitasaidia kuifanya Zanzibarkujifunza mengi ikiwa na pamoja kuzalisha bidhaa bora.

Nae Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko, Mhe. Ahmeid Nassor Mazrui, alisema maonesho hayo yametoa mwamko mkubwa kwa wananchi kutokana na idadi kubwa ya washiriki wanaojitoleza.

Alisema hapo awali walipanga washiriki wa maonesho hayo watakua 120 lakini hadi jana walifikia 160, wakitoka mataifa mbali mbali duniani ikiwemo Syria, Kenya, Indonesea, Uturuki na Tanzania Bara.

Alisema ushiriki huo umeiwezesha Wizara hiyo, kuona umuhimu wa kuandaa maonesho hayo kila mwaka, ikiwa ni hatua itayosaidia kukuza masoko ya wafanyabiashara.

Nae Mkurugenzi TANTRADE, Nd.Jaquiline Maleko, alisema taasisi yao imeamua kufungua tawi Zanzibar ili kuhakikisha inawapatia fursa wananchi kuweza kuimudu vyema sekta ya biashara ndani ya nchi na duniani.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara, Nd. Julian Rafael, alisema maonesho hayo ni sehemu itayokuza utalii na yanapaswa kuendelezwa kama inavyofanyika katika mataifa mengine duniani ikiwemo Dubai.

Tamasha hilola biashara limewashishirikisha viongozi mbali mbali wa Serikali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi, ambapo Dk. Shein, na viongozi hao walitembelea na kukagua bidhaa mbali mbali za wafanyabiashara hao.


Maonyesho hayo yanatarajiwa kufungwa Januari 13, mwaka huu. 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>