Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Uvumi wa kuwepo Tsunami wakanushwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa

$
0
0

Kuna taarifa inayosambazwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu za mkononi (SMS) kuhusiana na TMA kutoa tahadhari ya Tsunami

Taarifa hizo sio za kweli, uionapo ujumbe huu upuuzie kwa kuwa sio taarifa sahii, ni taarifa ya upotishaji

Taarifa rasmi ni kama ilivyotumwa awali kuhusiana na upepo mkali kwa Ukanda wa Bahari ya Hindi na Mvua kubwa.


Ujumbe huo unasomeka kama hivi:

TAHADHARI ya Tsunami: Kuanzia saa moja usiku Tsunami itafika Tanzania na mawimbi yatakuwa makubwa kuanzia muda huo. Taarifa zaidi itatolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania wakati wowote kuanzia sasa, kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agness Kijazi.

Tunapenda kuwataarifu wadau wetu kuwa ili kutoa taarifa sahihi ni vizuri kuwasiliana na Ofisi zetu kwa maelezo ya kina zaidi kuepusha mkangamanyo kwa wananchi

Asante tena kwa ushirikiano wako,

Nakutakia Sikukuu njema ya Maulid,

Monica Mutoni
Ofisi ya Uhusiano
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>