Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Maalim Seif azifariji familia ajali ya boti,zilizopoteza makazi Micheweni

$
0
0
Na Khamis Haji, OMKR
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amezifariji na kuzipa mkono wa pole familia za wananchi waliokumbwa na maafa kutokana na ajali ya boti ya Kilimanjaro II na wale nyumba zao zilizoteketezwa na moto kisiwani Pemba mapema mwaka huu.
Akizifariji katika maeneo tafauti, amezitaka kuwa na subira kutokana na maafa yaliyowakuta kwa sababu matukio kama hayo yanaweza kumkuta binadamu yoyote bila ya kutarajia.
Akizungumza na familia ya Nd.  Khamis Issa Mohammed katika mtaa wa Mbuyu Mnne Unguja, ambayo imepoteza watoto watatu katika ajali ya boti iliyotokea Januari 5 katika eneo la mkondo wa Nungwi, alisema serikali na jamii nzima iko pamoja nao katika wakati huu mgumu wa maombolezi.
Familia ya Khamis Issa ilipoteza watoto watatu ambapo mmoja, Nasba Khamis Issa aliweza kuokolewa. 
Wakati huo huo, alipongeza mshikamano uliooneshwa na wananchi wa Shumba Mjini na Maziwa Ng’ombe baada ya kutokea maafa ya moto mapema mwezi huu.
Alisema mshikamano na umoja uliooneshwa na wananchi hao kwa kusahau tafauti zao zote wakati wa maafa hayo ni mkubwa na hauna budi kuendelezwa katika maeneo mengine yanapotokea maafa.
Alisema hayo wakati akizungumza na wananchi na watu walioathiriwa na maafa ya nyumba zao kuteketea kwa moto katika vijiji vya Shumba Mjini na Maziwa Ng’ombe.

Alisema mshikamano wa aina yake uliooneshwa na wananchi hao katika kuzima moto pamoja na kuepusha usisambae na kusababisha maafa zaidi ni wa kupigiwa mfano na wananchi wa maeneo mengine waige mfano wa watu wa Shumba na Maziwa Ng’ombe.
Moto mkubwa uliozuka Januari 3 na 4 katika vijiji hivyo ulisababisha hasara kubwa kwa baadhi ya nyumba kuteketea kabisa na vitu vyote vilivyokuwemo na zaidi ya familia 50 zimeathirika.
“Nimekuja kuwapa mkono wa pole wote waliokutwa na maafa haya, lakini pia kuwapongezeni wananchi wa maeneo haya kwa mshikamano wa aina yake mliouonesha baada ya kutokea maafa yale,” alisema alipokuwa akiwahutubia wananchi wa maeneo hayo.
Alisema wananchi wote wa maeneo hayo walisahau tafauti zao na kuhakikisha moto huo hauendelei kusababisha maafa zaidi, baada ya kuwepo hatari ya kuteketea sehemu kubwa zaidi ya maeneo hayo.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mhe. Dadi Faki Dadi, amempongeza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, kutokana na moyo wake wa kuwafariji na kuwapa mkono wa pole wananchi hao, ambao hivi sasa wanakabiliwa na wakati mgumu kutokana na maafa hayo.

Alisema Serikali kwa jumla imekuwa karibu na wananchi hao na imeonesha moyo wa imani na huruma kutokana kutoa misaada mbali mbali kwa wananchi hao, tokea yalipotokea maafa hayo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles