Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Achomwa kisu akigombea mwanamke

$
0
0
Na Kadama Malunde,Shinyanga
MCHIMBA madini ya dhahabu aliyejulikana kwa jina la  Emmanuele Chacha (29), ameuawa kwa kuchomwa kisu kifuani na mwanamme mwenzie katika ugomvi wa kugombea mwanamke uliotokea kijiji cha Kalole kata ya Lunguya wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Kwa mujibu wa taarifa ya kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, SACP Evarist Mangala  kwa vyombo vya habari, tukio  hilo limetokea  Januari 10 mwaka huu saa tano usiku.
 Alisema marehemu ambaye ni mchimbaji mdogo wa madini aina ya dhahabu mkazi  Nyangalata wilayani Kahama mwenyeji wa Tarime mkoani Mara,  aliuawa kwa kuchomwa kisu kifuani na mchimbaji mwenzake, Cosmas Mazigo (23) wakati wakigombea mwanamke mmoja.
Kamanda Mangala alikitaja chanzo cha mauaji hayo kuwa ni ugomvi wa kugombea mwanamke ambaye bado hajafahamika, kitendo ambacho kilisababisha marehemu kuchomwa kisu kifuani.
Wakati huo huo katika kijiji cha Mwendakulima wilayani Kahama mwendesha pikipiki maarufu bodaboda  aliyejulikana kwa jina la Ally Tibaijuka (25), mkazi wa Nyasubi mjini Kahama amenusurika kufa baada ya kupigwa risasi moja ya bega la kulia na mteja wake aliyemfahamu kwa sura.
Kamanda Mangala alisema, tukio hilo limetokea Januari 11 mwaka huu saa 10 alfajiri baada ya mteja huyo kumwomba mwendesha pikipiki huyo ampeleke kijiji cha Mwendakulima kutoka eneo la klabu ya usiku iitwayo Social Club lakini ghafla mtu huyo alimpora pikipiki hiyo yenye namba za usajili T515 CFZ aina ya SANLG yenye rangi nyekundu mali ya Rashid Ramadhan.

Alisema mbali na kumpora pikipiki pia alipora fedha taslimu shilingi 25,000 pamoja simu moja aina ya TECNO yenye thamani ya shilingi 75,000 na kuongeza kuwa katika eneo la tukio imeokotwa bastola moja aina ya browning yenye namba A558563 ikiwa na risasi moja ambayo imesajiliwa nchini kwa namba TZ CAR 95579.

Kamanda huyo alisema chanzo cha tukio hilo ni kuwania mali na kwamba  majeruhi  amelazwa hospitali ya wilaya ya Kahama na hali yake ni mbaya na juhudi za kumtafuta mtuhumiwa zinaendelea.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>