Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

UVCCM wampongeza Dk. Shein kufanikisha mapinduzi

$
0
0
Khamisuu Abdallah na Salum Simba, MUM
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar, Nd. Vuai Ali Vuai, amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na ya Jamuuhuri ya Muungano wa Tanzania zinategemeana katika kulinda na kudumisha muungano.

Alisema Zanzibar na Tanzania Bara zimekuwa zikitegemeana katika masuala mbalimbali yakiwemo biashara, ulinzi,elimu na mambo mbalimbali ya kijamii hivyo si vyema kwa baadhi ya watu kusema muungano huo upo kwa ajili ya sehemu moja tu.

Aliyasema hayo wakati akizungumza na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) baada ya kupokea maandamano ya vijana yaliyoanzia Amani hadi  Mwembekisonge.

Alisema Muungano wa Tanzania ni kupigiwa mfano kwani umeleta maelewano na kukuza udugu uliopo.

Akizungumzia rasimu ya pili ya katiba,alisema chama cha Mapinduzi bado kinaamini kuwepo serikali mbili kwani ndizo zinazowasaidia Watanzania.


Hata hivyo, alimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein kwa kufanikisha sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiwemo kujenga mnara wa kumbukumbu katika maeneo ya Muembekisonge.

"Nampongeza sana Rais Shein kuibua wazo la kujenga mnara wa kumbukumbu hapa Kisonge pamoja na kutoa kitabu rasmi kinachoelezea historia ya Zanzibar japo kuwa kuna watu wanaosema mnara huu unaitia hasara serikali,” alisema.

Hivyo aliwasihi wananchi hasa vijana kutoona tabu  kuendelea kudumisha muungano na kuyalinda Mapinduzi kwani ndio yaliyowafikisha katika hatua mbalimbali za maendeleo .

Sambamba na hayo aliwataka vijana kujitokeza kwa wingi kwenda kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili waweze kupata haki yao ya msingi.


Nae Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Nd. Sadifa Juma Khamis, alisema wameamua kufanya matembezi hayo kwa ajili ya kumpongeza Rais  kwa hutuba yake  aliyoitoa katika sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>