Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar Hassam Mussa Yussuf , akimtambulisha Mgombea wa Chadema kwa Wananchi wa Jimbo la Kiembesamaki Ndg. Hashim Issa Juma, wakati wa kampeni za Chama hicho zilizofanyika katika viwanja vya bustanini kiembesamaki.
Naibu Katibu Mkuu wa Chadame Zanzibar Hassan Mussa Yussuf, akitowa Sera za Chama chake katika mkutano wa kumnadi Mgombea wao kuwania Jimbo la Kiembesamaki, katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya kiembesamaki Zanzibar.
Mgombea Uwakilishi kupitia Chama cha Chadema Ndg. Hashim Issa Juma akijinadi kwa Wananchi wa Jimbo la Kiembesamaki wakati wa kampeni zake kuomba kura kwa Wananchi wa Jimbo hilo katika Mkutano wa Kampeni uliofanyika viwanja vya kiembesamaki Zanzibar.
Mgombea wa Chadema Ndg. Hashim Issa Juma akiomba Kura kwa Wananchi wa Jimbo la Kiembesamaki. katika mkutano wake wa Kampeni.
Meneja Kampeni wa Mgombea wa Chadema Said Juma, akimnadi mgombea wake katika viwanja vya kampeni vya kiembesamaki wakiwa katika harakazi za mikutano hiyo.
Mzee wa Chadema Zanzibar akitowa Sera za Chama chake na kumuombea kura Mgombea wao Ndg. Hashim Issa Juma
Mbunge wa Nafasi za Wanawake kupitia Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Maryam Salum Msabaha, akitowa Sera za Chama chake na kumuombea kura Mgombea wao wa Nafasi ya Uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar, katika mkutano wa kampeni ya Uchaguzi Mdogo wa Jibola Kiembesamaki .
Mbunge wa Chadema kupitia Nafasi za Wanawake Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar Mhe. Abama, akimnadi mgombea wake.
Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mjini Magharibi Bi. Rufaa Mohammed Bakari, akihutubia katika mkutano wa Kampeni ya Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya kiembesamaki.
Katibu wa Chadema Mjini Ndg. Yussuf Khatib, akimwaga sera za Chama chake kwa Wananchi waliohudhuria Mkutano wa kampeni katika viwanja vya kiembesamaki.
Wananchi wakifuatilia mkutano wa Kampeni wa Chadema Mwanachama wa Chadema akiwa na baskeli yake ikiwana bendera ya Chadema, akifuatilia mkutano wa kampeni ya Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki.