Na Mwandishi wetu, Zanzibar
CHAMA cha Wandishi wa habari za Michezo Zanzibar (Zanzibar Sports Writer Association-ZASWA) kupitia klabu yao ya ZASWA FC, juzi waliwakumbuka wadau wa michezo wakiwemo wandishi na wadau wengine waliotangulia mbele za hakim, akiwemo Sikilo.
Tukio hilo lilifanywa na ZASWA FC wakati wa mchezo wao waliokipiga na Melisha FC, ambao ulikuwa maalum kutambulisha jezi yao mpya itakayokuwa ikitumiwa kwenye michezo ya nyumbani ya timu hiyo sambamba na kuwakumbuka wanamichezo waliotangulia mbele za haki.
Kabla ya mchezo huo kuanza, Wachezaji wa timu zote mbili walisimama kwa dakika moja kuwakumbuka wadau hao wa michezo ambao pia walikuwa mchango mkubwa kwa vyombo vya habari katika kuliendeleza soka visiwani humo na Tanzania kwa ujumla.
Akizungumza na wandishi wa habari, Mjumbe wa Kamati Tendaji wa ZASWA FC ambaye pia ni Kocha mchezaji, Ali Bakari Cheupe alisema walitambulisha jezi yao hiyo iliyozaminiwa wadhamini wao Zanzibar Group Hotel ikiwemo hoteli za Zanzibr Ocean View, Pemba Misali Beach, Amaan Bungalows,m yenye rangi nyekundu na ufito mweupe, aliwashukuru wadau hao sambamba na mgeni rasmi ambaye ni Rais wa Chama cha Soka visiwani hapa ZFA, Ravia Idarous Faina.
“Tunashukuru kwa jezi hii maaklum ya michezo ya nyumbani, pia tunaendelea kuwaomba wadau kuendelea kujitokeza kwa wingi kusaidia ZASWA. Pia mchezo huo ulikuwa maalum kuwakumbuka wenzetu, akiwemo Maulid Hamad Maulid aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa TASWA Visiwani hapa kabla ya kubadilishwa na Aliyekuwa mweka Hazina wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Sultan Sikilo, aliyefariki hivi karibuni” alisema Cheupe
Na kuongeza kuwa, ZASWA itaendelea kuwakumbuka wenzao hao, mara kwa mara huku kwa marehemu Sikilo likiwaumiza sana kutokana na ndiye aliyetoa wazo la kuanzishwa kwa ZASWA FC.
“Marehemu Sikilo ndiye aliyeshahuri tuanzishe ZASWA FC na wazo hilo alilitoa mwishoni mwa mwaka jana alipotmbelea visiwani hapa na tulilifanyia kazi, Desemba 24, tukafanikiwa kusajiri rasmi chama ZASWA, lakini mwanzilishi wa wazo ndiyo hivyo Mungu alimchukua ni pigo sana kwetu” alisema Cheupe.
Aidha, alisema kuwa, ZASWA FC itaendelea na mazoezi mbalimbali ikiwemo maandalizi ya kombe la NSSF 2014. “Pia tutaendelea na maandilizi ya kuona juu ya ushiriki wa michuano ya NSSF kwa mwaka huu. Ambapo kwa miaka ya nyuma huwa ilikuwa ikija timu ya Habari Zanzibar Fc, hivyo sasa tunajiandaa rasmi nasi kushiriki” alisema Cheupe.