Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Mashindano ya Quran Afrika Mashariki Zanzibar

$
0
0

 Viongozi wa Dini ya Kiislam Zanzibar wakifuatilia mashindano ya Kuhifadhi Quran Juzuu 30 kwa Vijana wa Afrika Mashariki yaliofanyika katika Masjid Afraa Kidongochekundu.

WANAFUNZI mbali mbali waliohudhuria mashindano ya Kimataifa ya kuhifadhi Kur an juzuu 30 kwa Nchi za Afrika mashariki na kati wakiwasikiliza washindananaji wa mashindano hayo yaliyofanyika katika msikiti Afraa Kidongo chekundu jana
 Mshindi wa kwanza wa kuhifadhi juzuu 30 kutoka Zanzibar Nassor Hamad Kombo (17)  yaliofanyika katika msikiti Afraa Kidongo chekundu










AMIR Mkuu wa Jumuia ya Kuhifadhisha kur an Zanzibar, Maalim Suleiman  Omar Ahmad akitoa nasaha zake kabla ya kumkaribisha mgeni Rasmi katika mashindano ya Kimataifa ya kuhifadhi kur an kwa wanafunzi wa juzuu 30 yaliofanyika msikiti Afraa Kidongo chekundu jana.
MWANAFUNZI, Abdillah Yussuf Ismail kutoka Kenya (kulia) akipokea zawadi zake kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha vyuo vya Kur an na Madrasa kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya amali Zanzibar, Sheikh Khamis Abdul hamid baada ya kutokea mshindi wa tano katika mashindano ya Kimataifa juzuu 30
Mkuu wa kitengo cha vyuo vya Kur an na Madrasa kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Sheikh Khamis Abdul hamid (kushoto) akimkabidhi zawadi mwanafunzi, Abbas Ahmad Ali kutoka Tanzania bara baada ya kutokea mshindi wa sita katika mashindano ya kuhifadhi kur an juzuu 30.
MSHINDI wa Kwanza katika mashindano ya kuhifadhi Kur an juzuu 30 kwa Afrika Mashariki, Nassor Hamad Kombo (17) kutoka Zanzibar (kulia) akipokea zawadi yake kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha vyuo vya Kur an na Madrasa kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya amali Zanzibar, Sheikh Khamis Abdul hamid. Katikati Amir Mkuu wa Jumuia ya Kuhifadhisha Kur an Zanzibar, Maalim Suleiman Omar Ahmad. Mashindano hayo yalifanyika katika msikiti Afraa Kidongo chekundu jana.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>